"Powers" ndicho kitu kikubwa kabisa duniani kuliko kitu kingine chochote! . God is Power, yaani Mungu ni nguvu, hakuna kitu chochote kinachoonekana kwa macho kumhusu Mungu, bali ni powers zake tuu za mambo Mungu anayoyafanya ndizo zinazoonekana. Chochote mtu atakachokiona kuhusu Mungu iwe ni kwenye mawazo, kwenye maneno, kwenye matendo, kwenye mahubiri, kwenye ndoto, kwenye unabii, kupitia Roho Mtakatifu au kupitia Malaika wake, it's just the manifestation of God's power kwa sababu God is a spirit of power ambazo zinafanya mambo mazuri, doing good.
Powers ndio kila kitu. Watu wote wenye nguvu ni powers, spiritual powers kwa watu wa imani, political powers kwa wanasiasa, economical powers kwa matajiri, social powers kwa wenye vipaji mbalimbali. Everything thing is about powers na mafanikio yoyote katika kila kitu ni jinsi watu wanavyo master hizi powers.
Kitu chenye nguvu kabisa katika mwili wa binadamu ni power ambayo ni nguvu inayoitwa "Will Powers" ambayo kila binadamu, anazaliwa nayo, ila wengine wanabahatika kwa nguvu hizo kujionyesha bayana, huku wengine wengi wakiwa nazo zikiwa zimejificha bila kujijua kuwa wanazo hizo nguvu.
Matumizi ya nguvu hizo, yanapotumika kutenda mema, huitwa nguvu za "Mungu", "Yesu", au "Roho Mtakatifu", "Powers of Light", nguvu za Mwanga, na nguvu hizo zinapotumika kutenda maovu kama uchawi, majanga, magonjwa, etc huitwa "Nguvu za Shetani" powers of the darkness, nguvu za giza, evil spirits etc.
Kwa vile nguvu hizi kila mtu anazo, hata hao wanaofanya miujiza ya uponyaji, wanachofanya ni kufungua tuu milango, ili nguvu zilizo ndani yako, ziweze kutenda hiyo miujiza, na ukipona, kilichokuponya sio huyo mponyaji, wala lile jina la Yesu, au jina Mungu, bali ni nguvu zilizo ndani yako!, "the powers from within!". Hivyo hata usipotumia jina la Mungu au jina la Yesu na ukatumia neno jingine lolote lenye powers vibrations kuzifungulia nguvu hizi zilizo ndani yako, nguvu hizo hufunguka, ndio maana watu wa dini zote hutumia.
Hatua ya kwanza ya kufungua nguvu hizi ni "imani" kuamini kuwa "you have the powers" and that "you can do anything!", or "you can be anybody". Kuamini Mungu, Yesu, Mtume, Allah, Roho Mtakatifu, Bikira Maria, Watakatifu, Wachungaji, Wahubiri, Baba Mtakatifu, Sangoma, Sheriffu, Mlingotini, Chini ya Mti, Chini ya Mbuyu, Mlimani, Pangoni, Kisimani, Mtoni, Ziwani, Kwa Mganga, Vitabu Vitakatifu etc, ni njia rahisi ya kuanzia kufungua milango ya "higher power" to open up your doors for powers from within!" to act on you for you!.
"I know I can, be what I wanna be!"
Psychic Powers- ni nguvu za kufanya miujiza ambazo wengi wanazo bila kujitambua!, swali ni jee wewe unazo?!,
Take time kujitambua kuwa you have the powers,
Nitakusaidia website za kukuelekeza ufanye nini kuhusu hizo powers ulizo nazo zikuletee mafanikio!.
Watu wote wenye mafanikio, wameisha jitambua, ila wengi wanafanya siri!.
Hii ni fursa kwa wewe kujitambua, kuzitumia powers ulizo nazo, kubadili maisha yako!,
NB. Hili ni muhimu sana kuzingatia, mzingi mkuu wa mada hii ni kujitambua, self awareness, kwa vile nimesema Mungu ni Nguvu za kutenda mema, God is Powers of Lightness, na Shetani ni nguvu za kutenda maovu, is powers of darkness, the dividing line between hizi powers ni very thin. Shetani is very clever, ni imposter, ana penda kuji disguise as Mungu, hivyo kuna mambo mengi ikiwemo miujiza ya uponyaji inayofanyika kwenye dunia hii, huku watu wakidhani ni kazi ya Mungu, kumbe sio kazi ya Mungu, ni kazi ya shetani. Hivyo be very careful.
Karibu tujadiliane!.
Paskali