Sijui ubora na ushujaa wa magufuli unatokana na nini, kwangu yeye ni worst president ambae hajawahi tokea Nchini mwetu, Yes ana mazuri yake ila mabaya ni mengi kuliko mazuri.
Mtu alieharibu mfumo wote wa ajira Nchi hii anakuwaje mzuri? Kipindi cha Mzee Nyerere hadi Kikwete hakukuwa na tatizo la ajira kiasi hiki, Nakumbuka walimu,manesi,wauguzi na madaktari walikuwa wanaajiliwa moja kwa moja baada ya kumaliza elimu zao na kupangiwa vituo vya kazi. Baada ya kuingia yeye huu mfumo wote aliuua na mpaka leo imekuwa kilio kwa vijana wengi, Kama watangulizi wake waliweza yeye alishindwa nini kuendeleza mazuri ya watangulizi wake?
Kuua sekta binafsi (Azasi) hapa ndio aliboronga zaidi, Sekta binafsi ndio msingi bora zaidi wa upatikanaji wa ajira Duniani ila yeye alihakikisha kuwa sekta binafsi anaziua kabisa badala ya kuzipa nguvu, nadhan alisahau kuwa watu wengi wameajiliwa na sekta binafsi, kwa ambao hatukuajiliwa serikalini basi hizi sekta binafsi zilituokoa sana, Firm nyingi sana za utafiti zilikufa na baadhi kufungwa kipindi cha Jiwe, Dodoso muhimu sana kwenye utafiti alizuia, Nadhan mtakuwa mnakumbuka Aidan Ayakuze wa Twaweza alichopitia na tafiti ya Sauti za Wananchi.
Kuua Upinzani ndani ya ccm na nje ya ccm, Jiwe alihakikisha anakuwa malaika au Mungu mtu, hakutaka kukosolewa wala kusahihishwa na makosa aliofanya, mtu au kikundi chochote kilichothubutu kumkosoa basi kiliipata, Refer ya Nape mnauye, January makamba n.k na kwa wapinzani ilikuwa ni balaa tupu, ukiachana na ya Ben saanane na Lissu, kuna kundi kubwa sana la vijana kuuawa kwa kujaribu kumkosoa.
Mtu asiezingatia utawala bora hawezi kuwa shujaa wa Taifa, aliapa kuilinda katiba yetu so kama mwenyewe alishiriki kuisigina katiba basi hafai kuwa bora miongoni mwa walio bora. Dead and gone, Mungu amlaze panapostahili
Kwa hiyo kwa sasa kuna ajira ?
Huwezi ukakopa ulaya kwa mashoga halafu utumie pesa za mikopo kuajiri wetu serikalini .
Ni upumbavu mkubwa.
JK alikopa pesa nyingi nje na mikataba ya kipumbavu halafu aauajiri wafanyakazi wa serikali kwenye nchi yenye madini mengi baada ya Kongo . Ni upumbavu wa hali ya juu.
Ni lazima kwanza ujenge mifumo bora ya kiuchumi kwa wazawa na serikali iwe na mifumo imara ya kudhibiti upotevu wa fedha za umma .
Ajira zipi unazosema zilikuwepo za wizi na ufisadi wa mali za umma.?
Yaani nchi yenye ardhi kubwa kama hii unategemea kukopa ili uajiri walilu wapumbavu na Machawa ?
Hivi walimu Kumi wa masomo ya Hesabu ,Phisics ,Jiografia ,Bialojia ,Chemia , Historia ,Civics, kiswahili, Bible knowledge ,Islamic Knowledge , Book keeping na Commerce wanashindwa kutafuta chumba kimoja wakaanzisha shule yao hata chini ya mnazi kama kweli wapo wana uwezo wa kufundisha ?
Baada ya miaka saba wangekua wanamiliki shule yao binafsi na kuunda body yao wenyewe na kuajiri walimu wengine . Sasa ajira za shule iliyoanzishwa na mama wa nyumbani aliyeanza na watoto wa kuvalishwa pampus .
Hivi China yenye watu bilion 1.5 inaweza kuajiri watu wote kwa kutegemea madili ya kuifilisi serikali kama Tanganyika .
Ni lazima iondoe mitandao ya kifisadi inayodhoofisha uwezo wa serikali kuajiri watu wenye uwezo na uzalendo.
Mifumo ya Kibepari inafeli kote duniani kwa sababu ya kutawaliwa na ubinafsi matokeo yake mataifa kama China ,India ,Pakistan , Indonesia ,Brazili na sasa Urusi inaonekana itakua mbali miaka michache ijayo kwa sababu ya kuweza kudhibiti uholela wa kutawanya rasilimali zake kupitia mikataba ya hovyo na ufisadi.
Ni wazi Wafanyabiashara wengi wakubwa wanakwepa kodi kwa kiwango cha juu sana . Matokeo yake wanyonge wanalimbikiziwa maushuru ,tozo , na vikokotoo.
Sasa kuna faida gani ya kuwaumiza mimilioni ya watu kwa sababu ya mafisadi wasiozidi hata elfu tano na wasiolipa kodi ipasavyo . Hao ni bora hata kuwanyongelea mbali.
Huruma ya JPM ilimponza maana mafisadi ni watu hatari kwa kununua wapambe wa kudhoofisha serikali.
Fika mikoa ya Tanga ,Arusha Musoma,Mwanza , Mbeya,Morogoro n.k. Viwanda vingi vya kuzalisha vilikufa kutokana na mafisadi wa chache kutothamini mali za umma. Mpaka leo Vyama vya ushirika vinakufa bila sababu za msingi .Mfano Kwa nini vyama vya ushirika vya mikonge vinakufa wakati mkonge una soko kubwa Asia . Nani anahujumu kama sio wasomi wanaokosa mtu imara wa kuchukua hatua kama JPM .
Hivi miradi ya bomba la mafuta ,SGR , Bwawa la Mwalimu Nyerere ,madaraja ,jiji la Dodoma ,mabarabara ,mahospitali , Upanuzi wa Bandari ,viwanja vya ndege kama Chato ,masoko makubwa ,stand za kisasa havikutoa ajira ?
Hamuoni kuwa kwa sasa hiyo miradi mingi imesimama ?
REA imeongeza gharama za umeme kwa sababu ya matakwa ya Majizi kuumiza wanyonge bila faida kwa serikali . Pamoja na kuongeza matozo na gharama za umeme lakini bado umeme inakatika kama nyoka aliyekatwa mkia .
Halafu mnamlinganisha JPM na watu wenye uwezo wa kuongoza sawa na monita wa darasa la sita.
Au mnafurahia pesa za taasisi za mashoga ,Magaidi na mikataba ya wauza madawa ndio mnaona nchi inapiga hatua kama Colombia ?
Tuliletewa mpaka pesa za Shetani kwa Mujibu wa waziri Membe wakati huo alidai pesa tutazitafuta hata kama zinatoka kwa shetani alimradi zisaidie matokeo yake wakaja na mpango wa kujiunga na jumuia ya nchi za kiislam na kuleta mtafaruku uliokuja kuzaa viashiria vikubwa vya ugaidi na vituo vya polisi kuvamiwa na askari kuuawa kwa kasi kubwa . Yote ni utawala wa hovyo usioweka misingi imara ya kitaasisi na kiuchumi .
JPM sikupenda kwa sababu sijawahi kuipenda CCM na ufisadi wa CCM wakati wa uchaguzi kama sasa wameanza ufisadi wa TANESCO . Tanesco yaney wateja zaidi ya mili 5 lakini bado haiwezi kujiendesha kutokana na ufisadi mkubwa .
Tanesco ikibinafsishwa akapewa Mhindi au Mwarabu itasifiwa kwa kukusanya pesa nyingi kuliko kampuni zote Tanzania .
Mfano tu Tanesco inauwezo wa