Punda wa Tanzania hawana mtetezi?

Baiskeli zinajaliwa kuliko punda. Baiskeli ikishindwa kupanda mlima, mwendeshaji anashuka na kuangalia sababu. Lakini punda akionekana kupunguza Kasi ya kupanda mlima, huzawadiwa "mijeledi".

Hawajui kuwa hata punda nao nguvu zao zina ukomo?
 
Kuna watu ni washenzi balaa, wanapiga fimbo nyingi punda huku amebeba mizigo mizito. Mbaya zaidi punda anapigwa mpaka anachanika ngozi. Punda anachibuliwa ngozi yake na mizigo hawekewi kitu kinachozuia msuguano kama wanavyowekewa ngamia na farasi huko ng'ambo. Punda wetu hawajaliwi japo wanabebeshwa mizigo mizito
 
Unashangaa kupigwa. Kuna wengine wanaingiliwa kimwili,
 
Usicheze na wasukuma wewe.
Hivi punde nimepewa na mwenyeji wangu taarifa inayotia moyo kidogo.

Inasemekana, Serikali ya kijiji huku niliko muda huu imepiga marufuku punda kufanyishwa kazi siku nzima bila kupumzishwa. Kwa Asubuhi, mwisho wa kufanya kazi ni saa tano Asubuhi. Awamu ya pili ya kazi ni kuanzia sasa kumi Jioni. Mtu akionekana akimtumikisha punda nje ya huo muda hukamatwa.

Kwenye eneo la kufanyishwa kazi muda mrefu, punda wa huku wamepata utetezi, lakini kipigo kipo pale pale.
 
Niliona jinsi wanavyobeba mawe plus mikwaju.
Duuuhh Shinyanga noma
 
Niliona jinsi wanavyobeba mawe plus mikwaju.
Duuuhh Shinyanga noma
Sijui kama wa Shinyanga wanateseka kama wa Geita Vijijini.

Wanabebeshwa mizigo mno, na mapigo juu.

Mawe, matimba (magogo ya kujengea mashimo ya migodi ya dhahabu) n.k. na vipigo visivyo na vipimo.
 
Piga picha za kutosha zitunze kwa ajili ya baadaye, zitaleta mrejesho.
 
Kwa nini siyo ng'ombe au mbuzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…