Punda wa Tanzania hawana mtetezi?

Punda wa Tanzania hawana mtetezi?

Nimeona Misungwi mkoani Mwanza na Geita Vijijini mkoani Geita!

Akiwa amebeba mizigo, anapigwa!

Akiwa analimishwa, anapigwa!

Akiwa anakokota mkokoteni, bado anapigwa!

Ni kama vile "lugha" pekee wanayoijua ni kipigo!

Utakuta wengine migongoni mwao kuna michubuko iliyotokana na ama kubebeshwa mizigo mizito au vipigo vya binadamu "wajinga"

Kwani haiwezekani kutumia njia nyingine kumfanya afanye kazi bila kujeruhiwa?

Kwani kipigo ndiyo njia pekee ya kumfanya punda kutimiza matakwa ya mmiliki wake?

Mbona kwa nchi zingine, hata tembo wanatumiwa kwa shughuli za kibinadamu katika mazingira rafiki tofauti na inavyotendeka kwa punda wa Tanzania?

Je! Punda amemkosa mtetezi? Simba, tembo, chui, fisi, mpaka na nyoka, wote hao wanalindwa na Serikali. Punda hana maslahi kwa Serikali?

Tanzania haina watetezi wa wanyama, au utetezi wao unaishia kwa nyangumi?

Kwa nini isijitokeze taasisi itakayotoa Elimu kwa wamiliki wa punda ili wajue jinsi ya kuwatumia kwa manufaa bila kuwasababishia mateso?
nenda kawatetee wewe mwenzao aisee. muunde na chama kabisa.
 
Chukua tairi ya baskeli kubwa (phoneix) kata sehemu moja halafu unganisha upande mmoja na kijiti kiwe kama mshukio.
Hapo unapata mjeledi mmoja matata sana
 
Kwa maeneo niliyofika Tz hii punda wanaokula bata naona ni Karatu tu. Nimekaa miezi miwili kule sikuwahi kuona wanapigwa wala kubebeshwa mzigo wa suluba. Maeneo mengi usukumani ndo wanakuwa wakatili sana kwa punda. Mnyama unamtegemea kurahisisha kazi zako ila humjali na bado vipigo kila dk, huwa sielewi logic ya hiki kitu
 
Watu wa huo ukanda watakuwa "wameelimika"
 
Mkaldayo acha tu huku mbwa ni mwanafamilia. Mbwa anathamani kuliko mwafrika. Mbwa analala ndani. Mbwa ana passport. Mbwa ana fungu lake kabisa kwenye bajet.
Halafu mgalatia punda ni mnyama mwenye akili sana
Kwetu kijijini tulikuwa tukiwatumia kuongoza ng'ombe machungani.

Yaani kama anaijua njia basi anawachunga ng'ombe nyie mnafuata nyuma tu anawafikisha nyumbani.

Pia kama kuna hatari labda porini mnyama mwitu punda ni mwepesi kujua na kuwapa alert.

Anaenda mashineni na kama ni karibu njia anaijua haitaji viboko wala manyanyaso .

Wanyama Sana hisia kama zetu ukiwapenda nao wanakupenda zaidi, huwa nikienda kijijini mifugo zizini inakufata mfano ng'ombe anagusa gusa shingo yake kwako umkune kama huwa humpigi pigi, hata punda pia.

Tusiwapige pige mkaldayo
 
Na mwingine ukimkasirisha, anakutukana, "mbwa wewe!"
Punda ni kiumbe mwenye akili sana sio kama tunavyodhani.
Watu wanakariri ukimpiga basi ndo anaenda muda mwengine shambani anavuta plaugh akichoka analala wanatandika viboko anagoma wanachukua majani makavu wanawasha mgongoni mwake ndo anaamka .huo ni ukatili

Punda anaenda mpaka mashineni kusaga kama anapajua anafika wewe nyuma yeye mbele haina haja ya kumpiga piga ukimfanya rafiki utapenda
Porini kuchunga ng'ombe punda anaongoza ng'ombe wengine pia kama kuna hatari ya mnyama mwitu punda anatoa alert .

Kama humnyanyasi basi unakuta umekaa anakuja anagusa gusa shingo yake miguu kwako umshike .

Hata ng'ombe pia ukimpenda unakuta akiwa na shida ya kusaidiwa kujifungua anakusogelea unaona hana amani kabisa anageuka kukuonyesha utaona kabisa kuwa anakaribia ndama kutoka mnamsaidia .tumefanya sana utotoni ila ukimpiga piga mnyama hakusogelei kamwe.
 
👏👏👏🙏🙏🙏
 
Mkuu, umeandika kwa hisia sana. Natamani hii Elimu ingewafikia wale wote wanaowakatili punda.

Ujinga ni mzigo mzito sana. Isingelikuwa ujinga, "wajinga" wasingewakatili wanyama wasio na hatia.
 
Wanyama nao wana hisia kwa sisi tulikuliaga makabila ya wafugaji tunaelewa.
Punda ukiwa unampiga piga akiwa na mimba utashangaa ghafla siku nxima anapotea anarudi mwenyewe ukichunguza kumbe kajifungulia porini kaacha mtoto huko ..!

Ila ukimpenda na kumjali anakuja mwenyewe analala chini umsaidie kuvuta mtoto the same to ng'ombe ..

Unakuta mzee akiingia zizini wanyama wote wanamfuata..! Wanampenda
 
Umenikumbusha mbali!

Nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikisikia watu wakisimulia kuwa ukimbebesha mzigo mtoto mdogo wa punda, mamaye hugomea kazi. Hatakubali hata ukimpiga. Hatakubali abebe mzigo na mwanaye mdogo.

Ili kuonesha mgomo wake, hulala chini. Piga jinsi unavyoweza lakini hanyanyuki mpaka uuondoe mzigo mgongoni mwa mtoto wake.

Kama hizo stori zilikuwa kweli, basi hao wafugaji walielewa kuwa punda yupo radhi ateseke yeye lakini hayupo tayari kumshudia mtoto wake akiteseka.
 
Nimeona Misungwi mkoani Mwanza na Geita Vijijini mkoani Geita!

Akiwa amebeba mizigo, anapigwa!

Akiwa analimishwa, anapigwa!

Akiwa anakokota mkokoteni, bado anapigwa!

Ni kama vile "lugha" pekee wanayoijua ni kipigo!

Utakuta wengine migongoni mwao kuna michubuko iliyotokana na ama kubebeshwa mizigo mizito au vipigo vya binadamu "wajinga"

Kwani haiwezekani kutumia njia nyingine kumfanya afanye kazi bila kujeruhiwa?

Kwani kipigo ndiyo njia pekee ya kumfanya punda kutimiza matakwa ya mmiliki wake?

Mbona kwa nchi zingine, hata tembo wanatumiwa kwa shughuli za kibinadamu katika mazingira rafiki tofauti na inavyotendeka kwa punda wa Tanzania?

Je! Punda amemkosa mtetezi? Simba, tembo, chui, fisi, mpaka na nyoka, wote hao wanalindwa na Serikali. Punda hana maslahi kwa Serikali?

Tanzania haina watetezi wa wanyama, au utetezi wao unaishia kwa nyangumi?

Kwa nini isijitokeze taasisi itakayotoa Elimu kwa wamiliki wa punda ili wajue jinsi ya kuwatumia kwa manufaa bila kuwasababishia mateso?
Mm nadhani Tanzania sisi elim Bado ndogo sana na hata viongozi wetu wanaangalia masilahi Zaid mfano mtu anaefuga PUNDA kwaajili ya shuguli zake Kuna wakati zinafeli kutokana na majerlah ambayo anampa yule PUNDA maana PUNDA anapokuwa na mazingira rafiki atawez kufanya kazi Kwa ufasaha kabisa na ww utamtumia PUNDA yule Kwa manufaa ya mda mlefu,, pia serikali yetu Kuna baadhi ya wanyama hawana haki wanaamua kuachia wananchi wenyew ndo watoe haki, na pia serikali inafanya Kwa wanyama waalibifu ndo ambao wanapewa haki na Sheria kali sana na hat katika utalii n kujinufaisha Zaid maana akuna mtu anatoka ulaya kuja kuangangalia PUNDA ama mbuzi hizo zingne wapeni haki nyie wenyew viumbe WA mhimu ni vya serikali
 
Nimeona Misungwi mkoani Mwanza na Geita Vijijini mkoani Geita!

Akiwa amebeba mizigo, anapigwa!

Akiwa analimishwa, anapigwa!

Akiwa anakokota mkokoteni, bado anapigwa!

Ni kama vile "lugha" pekee wanayoijua ni kipigo!

Utakuta wengine migongoni mwao kuna michubuko iliyotokana na ama kubebeshwa mizigo mizito au vipigo vya binadamu "wajinga"

Kwani haiwezekani kutumia njia nyingine kumfanya afanye kazi bila kujeruhiwa?

Kwani kipigo ndiyo njia pekee ya kumfanya punda kutimiza matakwa ya mmiliki wake?

Mbona kwa nchi zingine, hata tembo wanatumiwa kwa shughuli za kibinadamu katika mazingira rafiki tofauti na inavyotendeka kwa punda wa Tanzania?

Je! Punda amemkosa mtetezi? Simba, tembo, chui, fisi, mpaka na nyoka, wote hao wanalindwa na Serikali. Punda hana maslahi kwa Serikali?

Tanzania haina watetezi wa wanyama, au utetezi wao unaishia kwa nyangumi?

Kwa nini isijitokeze taasisi itakayotoa Elimu kwa wamiliki wa punda ili wajue jinsi ya kuwatumia kwa manufaa bila kuwasababishia mateso?
Hujui kuwa punda hasongi bila mijeledi?
 
Sisi Wasukuma tunafuata maneno ya wahenga waliposema " Punda haendi Ila Kwa mjeledi"

Punda mwenyewe inasemekana Shukran yake ni mateke
Waliosema hivyo wamemsingizia punda. Punda ndiyo wenye haki ya kulalamika na siyo binadamu wanaowatesa. Pengine, inawezekana huwa wanaambizana, "PAMOJA NA KUTUTUMIKISHA SANA, SHUKRANI PEKEE TUNAYOPEWA NA WANADAMU NI MAJERAHA"
 
Umenikumbusha mbali!

Nilipokuwa mdogo, nilikuwa nikisikia watu wakisimulia kuwa ukimbebesha mzigo mtoto mdogo wa punda, mamaye hugomea kazi. Hatakubali hata ukimpiga. Hatakubali abebe mzigo na mwanaye mdogo.

Ili kuonesha mgomo wake, hulala chini. Piga jinsi unavyoweza lakini hanyanyuki mpaka uuondoe mzigo mgongoni mwa mtoto wake.

Kama hizo stori zilikuwa kweli, basi hao wafugaji walielewa kuwa punda yupo radhi ateseke yeye lakini hayupo tayari kumshudia mtoto wake akiteseka.
Ndio ni kweli kabisa
Kwanza akiona unamfanyia jambo mtoto wake anakuja mwenyewe uone sasa.
Kuna punda wengine akili zao nusu ukimkoroga mbona utaeleza achilia mbali kumbebesha mtoto wake mzigo.
Kuna jamaa alitandikwa teke la kwenye goti mpaka Leo anachechemea mzee
 
Nimeona Misungwi mkoani Mwanza na Geita Vijijini mkoani Geita!

Akiwa amebeba mizigo, anapigwa!

Akiwa analimishwa, anapigwa!

Akiwa anakokota mkokoteni, bado anapigwa!

Ni kama vile "lugha" pekee wanayoijua ni kipigo!

Utakuta wengine migongoni mwao kuna michubuko iliyotokana na ama kubebeshwa mizigo mizito au vipigo vya binadamu "wajinga"

Kwani haiwezekani kutumia njia nyingine kumfanya afanye kazi bila kujeruhiwa?

Kwani kipigo ndiyo njia pekee ya kumfanya punda kutimiza matakwa ya mmiliki wake?

Mbona kwa nchi zingine, hata tembo wanatumiwa kwa shughuli za kibinadamu katika mazingira rafiki tofauti na inavyotendeka kwa punda wa Tanzania?

Je! Punda amemkosa mtetezi? Simba, tembo, chui, fisi, mpaka na nyoka, wote hao wanalindwa na Serikali. Punda hana maslahi kwa Serikali?

Tanzania haina watetezi wa wanyama, au utetezi wao unaishia kwa nyangumi?

Kwa nini isijitokeze taasisi itakayotoa Elimu kwa wamiliki wa punda ili wajue jinsi ya kuwatumia kwa manufaa bila kuwasababishia mateso?
Punda huwa hawatumiwi kulima ndugu.
 
Back
Top Bottom