tatizo ni kwamba ata iyo asilimia ukipiga bado ni zaidi ya iyo 14% wao wanapiga vipi?
Vyama vya upinzani vikiingia madarakani vitachukua hatua gani ya kupunguza kodi??? Au unatutaka tuindoe madarakani serikali ya CCM lakini huko mbele tusijue kutakuwa na nini? Unataka kutuhamasisha kama ilivyokuwa enzi za uhuru kisha tukahamakika (tukahamasika) kumng'oa mkoloni lakini tusijue akiondoka nchi tutaiendeshaje? Unataka kutusababishia matatizo bila ya kutupa ufumbuzi wa matatizo hayo? Tueleze sasa......kamba vyama vya upinzani kwa mfano mishahara itakuwa shilingi ngapi? Ukabila utashughulikiwaje, ubaguzi wa kikabila utashughulikiwaje, mikataba itakuwaje na uchumi utakuwaje na wao watatumia mbinu gani tofauti na zilizopo katika kumkwamua mtanzania kutokana na ujinga (kama huu wa kushabikia kitu usichokijua) na umasikini? Wao wakiingia watatumia sarafu gani? hii ya sasa ama watatumia dola? Na maswali mengi tu. Wajibie ama jibu wewe mwenyewe hapa JF ili tuwe na uhakika.
Wewe unayekataa upinzani kuchukua nchi na kutaka tuendelee na hao mafisi wa CCM ndiye unayepaswa kusema uzuri wa CCM dhidi ya ule wa upinzani. Usiwe na mawazo ya kihafidhina kihivyo! Upinzani bado haijaingia madarakani. Itakuwaje udai utawala wao utakuwa sawa na wa CCM? Na kama hauridhiki na utawala wa CCM na pia huutaki upinzani uchukue nchi, unachotaka ni nini hasa? Hujitambui au nini? Kwani wapinzani wenyewe wakichukua madaraka halafu waendelee na madudu kama ya CCM unaona ugumu gani kuwaondoa madarakani kwa kura? Don't be so rigid and conservative. Tuambie hao CCM unaowakumbatia wamefanya nini kwa miaka 50 waliyokuwa madarakani, ukilinganisha na utajiri wa rasilimali tulizo nazo, sio unakaa kubwabwaja tu bila kusema unachotaka ni nini!!!!
Naona una excercise theory ulioyoipata wakati unasoma ka kozi kako ka kuungaunga kwa super glue......Hata hivyo umejitahidi kubwabwaja bila ya kujibu hoja zangu. Hebu taja mazuri ya wapinzani japo mawili tu kabla sijakutajia mazuri elfu moja ya CCM!!!! Na kama hutapata mazuri ya wapinzani basi huna hoja....Na hatuwezi kufanya majaribio ya watawala kwa kisingizio eti tutakuja kuwatoa kwa kura....Haitawezekana maana wao yaelekea wana uchu wa madaraka sana watataka wakae miaka 100 ili waibe.
Au kwa kifupi nitajie barabara yenye urefu wa nusu kilometa tu walioijenga wao kwa ushawishi ama hata harambee ya kuchangishana then mimi kuanzia leo nitajiunga nao. ninao ushahidi mkuwa sana kwamba hawako kama tunavyowafikiria ndo maana nakusihi uendelee kuingunga mkono CCM. Au nikupe ushahidi kwamba hata ukiomba scholarship kwa serikali ya wapinzani huwezi kujibiwa maombi yako? Ni heri anayekujibu kwa kukukatalia kuliko anayekaa kimya....Poleni m,naodhani wapinzani watakuja kuinua maisha yenu.....
Naona naongea na robot au msukule. Kwa hivyo wewe unavyoona hayo mazuri 1000 ya CCM unayoyafahamu wewe (na mkeo/mumeo?) yanalingana na utajiri wa rasilimali tulizo nazo? Hebu yataje basi. Na unapoongelea kuhusu kuomba scholarship kwa wapinzani unamaanisha nini? Kwani UPINZANI ni SERIKALI? Napoteza muda bure kubishana na msukule!
Mkuu..serikali zote duniani zinatoza PAYE.. Hata kama misamaha ya kodi kwenye madini itafutwa bado Paye itaendelea kutozwa kwa viwango vya kulalamikiwa
Waziri wa fedha ndio anatolea ufafanuzi ila anasema serikali itaendelea kadri ya mapato yanavyopatikana kwa hiyo asilimia imebakia kama ilivyo !Kama kawaida ccm kwa usanii imepunguza kwa asilimia moja tu