Kuna ugumu kidogo kuacha vitu ambavyo vina 'addiction', ni sawa na mlevi kuacha pombe, mvutaji kuacha sigara/bangi, teja kuacha unga etc.. Ni kitu amabcho kinawezekana lakini kinahitaji committment. Mara nyingi kuacha si kazi sana, bali kujizuia kurudia ndio huwa tatizo kubwa sana.
Katika case yako hii nachelea kuamini kuwa unapiga sababu upo mbali na mkeo, kwani ni tabia umekuwa nayo kwa miaka 14 hata wakati mkeo alikuwepo..kwa hiyo uwepo wa mwanamke (awe mkeo au nyumba ndogo) hautakuzuia kupiga punyeto.
Usahuri wangu ni kuwa..utakapojiskia ashki na kutaka kupiga puchu basi fanya kitu/kazi nyingine yeyote mbadala. Mazoezi ni njia nzuri zaidi, waweza kwenda jogging, au kutembea tu umbali mrefu, kubeba vyuma, au kazi yeyote ya nguvu mpaka uchoshe mwili. Kama una tabia ya kuangalia sinema/porn au kusoma majarida ya ngono inabidi uache...kama una DVDs/VCDs/CDs/Majarida ya aina hizo ziharibu kabisaaa.
Epuka vipindi vya television au movies zenye mahadhi ya ngono, na mazingira mengine ambayo huwa yanakushtua upige punyeto. Kama kuwa peke yako nyumbani pia kunakupulekea hali basi jaribu kuepuka mazingira hayo na kujaribu kuwa na watu/marafiki/ndugu pindi unapoona unaelekea kuvutiwa kupiga punyeto.
NB: Punyeto ina madhara kwa kiwango/uwezo wako wa kumridhisha mkeo/mwanamke ikiwa utakuwa unafanya sana (kama unavyofanya wewe), hivyo epuka mapema. Raha ya maisha kwa mwanaume ni kuwa rijali..hata uwe tajiri vipi. Tunza urijali wako!