Putin anaonya nchi za Magharibi: Urusi itaibuka kama taifa lenye nguvu zaidi

Watu wa JF ukiwafuatilia sana utazani wana uchumi kumzidi Russia, wakati wenzetu wanajitegemea kwa kila kitu. Leo sis ndio tuwe na ufaham mwingi kuwazidi wao hahahaha.
 
Yaani kichwa cha habari hakiendani na content.
Inabidi tuwe wapenzi wasomaji wa comment tu hapa,lakini uhalisia wenyewe anaujua Putin na wanaomzunguka ndiyo maana kageuka kuwa motivational Speakaer kujaribu kuwaondolea hofu wananchi wake kwa kile kinachokuja mbele yao.Vita na iishe hata kesho,Putin aikalie Ukraine ikiwezekana halafu sasa tutarudi kwenye uhalisia tuone nani atakuwa mshindi wa hii vita.
 
Kweli.
 
Hali ilishakuwa mbaya huko!!na wananchi wake wameshaanza kumkataa!!na zamu hii atapata shida sana
Halafu watu tuko hapa tunadharau vikwazo utadhani waliovibuni viwepo walikuwa wajinga.Tungekuwa na uwezo kama tunaouonyesha katika hii mijadala wa kudharau waliotuzidi Tanzania ingekuwa Ulimwengu wa kwanza ki uchumi na katika nyanja mbali mbali,lakini kwakuwa tumejaliwa midomo tu ya kuongea basi tutaendela kuwa hivi hivi tulivyo kizazi hadi kizazi.
 
Naona ndo anawapa moyo watendaji wake wasikate tamaa.
Hata yeye anajua hofu kuu waliyonayo lakini pia deep down hana amani,huwezi watawala watu waliojawa na hofu ya nini hatma yao ya kesho na hasa watu wenyewe ni kama hao ambao tayari walishaonja matunda ya kuishi na kula bata kibepari.Mtu kazoe kwenda kushop kwa LV,GUCCI,PRADA and the likes leo hii anaona hakuna tena maduka kama hayo achilia mbali wenye maisha ya kawaida ambao ni wengi zaidi wataumia
 
Reactions: Tsh
Watu wa JF ukiwafuatilia sana utazani wana uchumi kumzidi Russia, wakati wenzetu wanajitegemea kwa kila kitu. Leo sis ndio tuwe na ufaham mwingi kuwazidi wao hahahaha.
Na wale wanaodharau Upande wa pili je?
 
Rais wa Russia Comrade Vladmir Putin Amesema Nchi hiyo inakwenda kuwa Nchi Imara na yenye Uchumi Mzito kuliko ilivyo Leo kinyume na Maadui zake wanavyojidanganya.

Putin aliyasema hayo Alhamis alipokuta na Baraza la Uongozi la Russia kwenye Kikao ambacho kilikuwa Live kwenye Radio na TV, na kuonyeshwa Live na TV na Radio zaidi ya 420, kwenye Mataifa Mbali mbali yenye Uhuru wa kuonyesha Habari kutoka Urusi.

"Lazima Mjuie, Tulijua kuwa watakuja na silaha hii butu, kwa sababu najua hawawezi kutupangia njia za kujilinda dhidi ya hatari tunayoiona, Nimeamua kufanya Operation ya Kijeshi kwa Serikali ya Kyiv kwa sababu za Usalama wa Russia na vizazi vyake vya kesho" Hakuna wa kunizuia, hakuna wa kutupinga, na hata wakiweka Vikwazo mara elfu moja, bado tuna Haki ya Kusimama Kulinda usalama wetu"..Na sasa Maumivu waliyotaka kwetu yamerudi milango mwao.

"Ni Wapuuzi kabisa, na hivyo vikwazo vyao mmeona matokeo yake, Sasa Nauli za Ndege kwenda Hanoi ama Macau zimekuwa mara Mbili na zaidi, lakini kwa Vile Mataifa hayo yanaongoza Vipofu yamezuia kutolewa habari hizo, Viongozi wao wanaendelea kufanya Mzaha na kujaribu kuwafumba watu wao"

"Nilipokea siku hiyo hiyo waliposema Russia isisafirishe Mafuta kwa Nchi za America, Ajabu siku tatu Baadae wamelalamika Bei za Mafita zimekuwa karibu mara mbili, na Mfumuko wa Bei za Bidhaa zao Hazielezeki kabisa, Ni Kichaa tu anayeweza kusema Eti Tunaumia sisi kuliko Ambaye Bidhaa zake zimepanda kwa 170.6%.

"Kwa sasa katika Ulaya Nzima penye Unafuu wa Maisha ni Russia tu, Wengine hata Gesi Imegeuka dhahabu, hupati gesi, watawala wao wamejipiga shaka kwa kujaribu kupambana na Russia"...Rais putin alinukuliwa akisema.

"Walitaka tukubali kuhatarisha usalama wetu kisa manufaa Kiduchu ya kiuchumi, Haiwezekani, hatukubali na siku yoyote ikiwa hivyo tutajibu vikali zaidi kuliko Operation ya Ukraine ".
 
Mpaka Putin anaingia vitani, haya yote alishayabaini na kuyafanyia mahesabu. Si mjinga. Vikwazo vinawaumiza wote, wa nje tena zaidi. Kila mtu, popote pale, atajikuta analipia gharama za kushupaza huku shingo.

Unabana kumkomoa Putin huku mzigo unarudi kutesa raia wako wanaotegemea gesi na mafuta 'rahisi' kutoka hukohuko ulipobana.

Kiburi cha Putin ni kuamini Ulaya inamhitaji yeye zaidi kuliko anavyoihitaji.
 
The last kick of a dying donkey.

Russia imekua kama kisiwa, hakuna ndege wala meli inayoweza kwenda ama kutoka Russia.

Hii ni failed state after 2 months ahead
Mpaka Putin anaingia vitani, haya yote alishayabaini na kuyafanyia mahesabu. Si mjinga. Vikwazo vinawaumiza wote, wa nje tena zaidi. Kila mtu, popote pale, atajikuta analipia gharama za kushupaza huku shingo.
 
Anaongea kwa mtazamo kwamba wao pamoja na wamagharibi watasota kiuchumi nani ataibuka kwanza. Wamagharibi pamoja na makelele mengi hawakutegemea huyu jamaa ataenda kijeshi chap ivo na hawakuwa tayari. Aidha wangeshajiandaa mambo ya mafuta nk
... na sisi vitawi vya pembeni ndo tutaenda kwa upepo tukishikilia mkuti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…