Toka vita inaanza Putini amekuwa mtu wa maonyo halafu anatulia zake kwa mfano alisema:-
1) Finland na Sweden wakijaribu kujiunga na nato atapiga nuclear kwenye moyo wa nchi za ulaya.
3) Alisema akigundua nchi inaisaidia Ukraine silaha ataishambulia on the spot, na hii Marekani walimjibu live kwamba wanaisaidia ukraine silaha na wataendelea kuisaidia duniani na mbinguni mpaka ukraine ibaki salama na mipaka yake alijibiwa ni Waziri wa Mambo Ulinzi na Usalam wa Marekani.
4). Alionya Ukraine wasijaribu kujiunga na Umoja wa Ulaya, lakini tumeona live Ukraine walijaza form live pale Kyiv na kuzikabidhi kwa Rais wa umoja wa Ulaya yule mwanamama.
5) Putini aliwaonya Jeshi la Ukraine wasalimu amri mara mbili na akawapa na masaa Ukraine wakakataa na sasa hatukuona chochote badala yake, wanaume wako kazini
Ulaya na Marekani wamejuwa weaknesses za Putini mara elfu 1 zaidi hivyo ni kama vile wanafanyia visa kwa fujo ili wapate kumtibua halafu hana lolote., kwamfano leo Spain wamentangaza kupeleka mitambo Ukraine ya kuzuia zile long range missiles
Putini bora angetulia dunia bado ingekuwa inamuhofia kwamba yeye ni strong kuliko alivyovamia Ukraine na kwa muda mfupi ulimwengu kupata majibu ya madhaifu yake., bongo wanamuita Putini wa Mchongo