Eneo gani la Finland ambalo Russia alimega? USSR alipigwa na Finland akafanya withdraw, kama unabisha leta facts zako mezani sijui utazitoa wapi nami nilete za dunia ambazo hata Russia wenyewe wanajua.
Kuna interesting tactic walitumia Finland, walikuwa wakipata intelligence information kwamba ndege za adui zinakuja kufanya bombing raids mji mkuu wao pendwa wa Helsinki wanatangaza kuzima taa zote mjini kisha mapori yaliyo karibu na mji wanapanga mistari ya taa za barabarani ionekane ni mitaa. Usiku bombing raids kipindi kile hazina navigation nzuri walikuwa wanatafuta kwenye taa nyingi ndio inaonekana mitaa yenye majengo mazuri na muhimu. Warusi wanadondosha mabomu porini kisha wanarudi. Finland mpaka vita inaisha mji mkuu umesimama wima.
Snipers wa Finland hao ndio usiseme walikuwa hatari sana. Kupigana kwenye snow ndio kipaji chao, vifaru vya Urusi vilifeli mbele ya spirit ya watetezi wa taifa lao. Finland wana msemo wanasema nchini kwao kuna wanajeshi wengi wa Urusi ila wamejificha ardhini chini ya mita tano wakimaanisha waliofia vitani