Putin; Maadui zetu mjifikirie mara mbili kwa hili bomu

Tangu Hitler afariki,
German walifilisika Sana kijeshi,

Na kingine ujue mpaka Leo hii ujerumani bado analipa madeni ya kivita kwa hasara alizosababisha HITLER nchi nyingi Sana ulaya nzima.

Kujijenga kijeshi ujerumani atahitaji muda sana
 
The way una explain utadhani Russia is Alpha na Omega in this World[emoji846]
 
UK,GERMAN,&FRANCE hawana jipya ,walijisahau kwa kuvimbiwa na legancy ya ku concur dunia enzi za the scramble for Africa,na Berlin conference ,walijua dunia imesimama ,kumbe inazunguka ,wanakuja kushtuka wako outdated kitambo,waliahajikatia tamaa kwenye medani ya kivita wameamua kutulizana walee familia zao tu.sasa hivi hawanajipya hao.hata NORTH KOREA hawamfikii ,sembuse Russia!!!
 
Mzee nuclear warhead hazina range...chenye range ni delivery system hapa unaongelea suala la missile na aircraft mfano b2 au tuplov za russia...na changamto kubwa kwenye nuclear warfare ni namna utakavoweza kuzi lunch hizo missiles kwa adui zako na ndio maana mara nyingi north korea anacho test ni missile sio nuclear explosions..so ukija katika teknolojia ya missile urusi kawaacha western mbali sana.
 
Putin akili kubwa. Amefanya jaribio hilo muda muafaka kwani ktk mgogoro huu na Ukraine kuna wabwekaji wengi sana sasa alikuwa anajaribu kuwakumbusha kuwa wanadili na mtu hatari sana.

Hapa picha iliyopo ni kama hivi unapita kitaa na unakutana na kundi kubwa la mbwa. Mbwa wanaanza kukubwakia kwa nguvu sana, wewe unachofanya ni kuokota jiwe tu, mbwa wengi watakimbia watakaobaki ni wachache sana na watakuwa wanabweka kwa mbali kwa machale na hofu kubwa imewajaa maana watajua mjamaa anaweza rusha jiwe mda wowote. SHIKAMOO PUTIN
 
Sikuelewi unaposema nyuklia warhead haina range na kama ni hivyo ina maana haisafiri basi na sio kwamba nyuklia warhead zote zinarushwa na ndege, kuna zinazorushwa kutoka kwenye meli na zingine toka kwenye stationary launch pads.

Hakuna uthibitisho kwamba Russia kawaacha nchi za magharibi mbali kwenye teknolojia ya makombora na naona huelewi kwamba ni Marekani na Russia tu ndizo zenye uwezo wa kurusha kombora na likatua sehemu yoyote duniani.

Russia sawa na nchi zingine za kikomunisti zina tabia ya kishamba ya kuonyesha silaha zao hadharani kama njia ya kutisha wananchi wao na mataifa ya nje ili zisikemee tawala zao za kiimla.
 
Wewe 'ujuaye' kila kitu na 'mtaalamu wa silaha' hebu tuonyeshe hata baruti yako uliyotengeneza mwenyewe,tusije kuwa tunabishana tu hapa kwa maneno matupu ya kugoogle kwa kutumia tech ya Mmarekani kupata hata hizo data tunazotambiana hapa.
Kwa wewe taarifa ulizonazo chanzo chako ni nini.
 
Germany imebaki kua nchi ya amani na kwa sasa hawatengenezi kwa wingi tena silaha kama enzi ya ww2
 
Reactions: Tsh
Ndio umeandika nn !!!??
 
Kinachompa jeuri sababu yeye kila silaha lazima aitangaze? Anaamini nchi kama UK, German hawana hivyo vyombo? Usikute vya wenzake ni imara zaidi, maana hata kikawaida tu, bidhaa za ulaya ni jiwe haswa kuliko za asia.
Mkuu, hivi unafikiri wangekuwa na silaha wangemwachia Putin atambe atakavyo, thubutu!
 
Unaandika simple sana utadhani Nuclear war ni vita ya majimaji, wanaoelewa madhara yake kamwe hawawezi kuandika kitu kama hichi.

United States walitumia nuclear weapons kwa hiroshima na nagasaki na hakuna nchi yoyote iliyomgusa.
Na Russia pia wanaweza kutumia nuclear weapons popote na hakuna atakaye mgusa sababu kila mtu anapenda amani nchini kwake na maisha ya wananchi wake.

Kama Russia wakianzisha vita ya nuclear mataifa mengine ni lazima yakae kimya ili kuepusha Nuclear holocaust ambayo itaangamiza dunia nzima, na hakuna mtu mwenye ubavu wa kuanzisha hicho kitu.
Ni afe mmoja au tufe wote na mpaka sasa putin ndio mtu pekee anayeonekana kuwa na will ya kudeploy nuclear na wala hajali chochote zaidi ya maslahi yake.
Mambo ya nuclear sio rahisi hivyo kwamba mimi nikipiga basi kila mtu anapiga kama manati, na kusema kwani nani hana mawe!

Hapa tunaongelea mwisho wa maisha duniani kwa ujumla au baadhi ya sehemu za dunia kuwa uninhabitable kwa mamia na maelfu ya miaka au extinction ya baadhi ya races.
 
Sio wajinga kiasi hicho mtu anakuonesha rungu na AK 47 iko ndani au anakuambia specifications fake za uwezo wa kombora lake ili usijue ukweli lkn pia yale maonesho ya siraha ni taarifa kwa wananchi una ulimwengu kuwa hatujalala bali tumefikia hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…