PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

Iran yeye alikuwa na Rusia noth Korea Hezbollah Hamas Syria Iraq Yemen na wengine game ni team , ww unaficha ukweli Nyau angeamua kulipa sawasawa angewafanya ila kapiga kichwa eneo lenu la Ulinzi mnaojisifia ndo maana hamkujibu tena ,
Ndugu tunachoshindwa kuelewana ni kimoja. Wewe unaandika mambo yako kihisia bila kuweka ushahidi. Mimi naandika na kuweka ushahidi. Sasa hapo unafikiri nani anaeweza kushinda kesi mahakamani?

Kila mtu ukiwepo wewe mwenyewe uliona jinsi Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Saudi Arabia, Jordan na Israel yenyewe zilivyohangaika kuzuia makombora yaliosafiri kwa mwendo wa takriban Kilometres 2000 bila mafanikio.

Lakini hizi habari zako ni za hisia tu maana hata wewe mwenyew hapo nikikuomba ushahidi uuweke hapa hauna.

Russia yupo vitani mwaka wa 2 huu aache kupambana na maadui zake aje apambane na maadui wa mwenzake inaingia akilini kweli. Kumbuka Iran ndio inayompa Mrusi baadhi ya silaha ili kuwaangamiza mashoga wa NATO huko Ukraine.

North Korea pia anavikwazo lukuki na nchi yake ni taaban kiuchumi, sasa inawezaje kukimbilia kumsaidia mwenzake badala ya kujisaidia kwanza yenyewe.

Hao kina Hezbulla wanaichapaga Israel toka zamani, acha kujificha kwenye hiki kipigo cha juzi cha Iran.
 
Ni ukichaa kumlinganisha putin na takataka.kwanza ameshinda vita ya Ukraine Mbele ya nato pia ametengeneza nchi imara ndo maana hata wakiweka sanction hazifanikiwi.
Netanyahu juzi kanyimwa mabomu ya kilo 900 na Biden kaanza kulia na kulalamika mpaka dunia nzima ikajua. Je akiwekewa vikwazo kwa kuda wa miezi mi5 tu si ndo ataitoroka nchi kabisa kuhofia kushambuliwa bila kuwa na silaha za kujilinda.
 
Niaje waungwana

Leo nimeamua nilete kwenu uzi huu ili tumalizie ubishi uliopo mtaani kwetu kwa muda wa week tatu sasa bila kumpata mshindi wa kweli, huku kila kundi likivutia kamba upande wake.

Ubishi wenyewe unahusu miamba miwili yenye roho ngumu, maamuzi mazito na misimamo mikali isiyoyumba, wala kuyumbishwa na watu wengine. Na miaka hiyo sio mingine isipokuwa ni raisi wa Russia Vladimir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu.

Kwanza kabla ya watu wengine hawajaingia hapa kutoa maoni yao kuhusu nani bora kati ya raisi Putin na waziri mkuu Netanyahu, naomba kwanza na mimi na mimi nitoe maoni yangu juu ya nani zaidi ya mwenzake.

1. Nikianza na raisi Vladimir Putin, huyu kwangu ni mwamba kweli kweli ambae kumlinganisha na bwege mpenda kulia lia kama Netanyahu ni kumkosea heshima Putin. Netanyahu ni mchumba na hawezi kufit kwa Putin hata kwa nusu ya sifa zake.

Putin ni kiongozi makini, mwenye akili kubwa, misimamo thabiti na intelejensia kali kuliko Netanyahu. Kwa kuthibitisha hili angalia uchaguzi wa uraisi wa 2016 alivyoweza kupachika vijana wake katika mifumo ya Marekani ili wamletee raisi anaemtaka yeye. Ni nani mwengine katika dunia ya leo mwenye uwezo wa kufanya kile alichofanya Putin, tena ndani ya ardhi ya Marekani na mifumo imara ya Marekani? Ni nani mungine?

I hope jibu hakuna maana hata China imeshajaribu kutuma mpaka maputo ili na yenyewe ifanye yake lakini yote yakashushwa. So Putin yeye aliweza tena kwa kuingilia mifumo ya ndani ya nchi bila kugundulika mpaka pale mission yake ilipokamilika, ndo alipokuja kushtukiwa ila akawa ashafanikiwa kwa 100%.

Tukija kwenye misimamo thabiti, jamaa amesimamia kile anachoamini yeye tu, bila kujali vitisho, vikwazo na kelele za nchi za magharibi including NATO. Ameingia nchini Ukraine kukamilisha mission zake bila kujali kelele za mtu yoyote. Si Marekani, NATO wala Umoja wa Ulaya aliethubutu kuingiza jeshi lake Ukraine kupambana na uvamizi wa Russia. Sana sana wameishia kutuma visilaha tu ili kujaribu kudhoofisha mission zake bila mafanikio.

Putin hajawahi kulia hadharani kuwa kaishiwa silaha au mbinu za kijeshi, NEVER. Yeye ni kutoa dozi tu na kusonga mbele daima, huku Marekani na washirika wake wakiendelea kuangamiza silaha zao kuipa Ukraine ili iizuie Ruusia kusonga mbele bila mafanikio.

Putin yeye anapambana na nchi kamili yenye raisi wake, serikali yake, jeshi lake (lenye mamilioni ya wanajeshi), silaha zake (za zamani na kisasa), ulinzi wake (juu na ardhini) Lakini bado haoneshi kushindwa wala kurudi nyuma. Nchi yake bado imeendelea kuogopwa hata na nchi zinazojifanya ni watemi wa dunia. Pia maangamizi yake yamekuwa yakiwalenga zaidi adui zake (wanajeshi na viongozi wa serikali) ikitokea raia ameuwawa basi ni kwa bahati mbaya ile tunaita ajali kazini. Ndiomaana toka vita vianze wanajeshi waliouwawa na wengi kuliko raia wa kawaida.

Putin pamoja na kuwa katika vita vinavyoshirikisha mataifa kibao ya Ulaya kuwa upande wa adui yake, lakini bado economic yake ipo imara mno, na ni nchi ya tatu kwa bajeti kubwa ya kijeshi duniani baada ya Marekani na China. Nchi yake haitegemei bajeti ya kijeshi kutoka nchi yoyote ile hapa duniani. Inajisimamia yenyewe miaka yote ya utawala wa Putin.

2. Tukija kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu, huyu kwangu ni mchumba tu mbele ya Putin, kwa sababu maamuzi yake hutegemea misimamo ya magharibi inasemaje. Yani inaonesha wazi kuwa huwa anapewa maelekeza ya nini cha kufanya na wakubwa zake kutoka huko West, na haswa Marekani.

Kila analolifanya Netanyahu sio ni la kwake bali ni la waliomtuma. Ndomaana wanapocheleweshaga kumtumia silaha za kufanikisha mission aliyopewa, hukimbilia katika vyombo vya habari na kuanza kulalamika kuwa wanamtelekeza na kumuacha apambane kivyake bila msaada wao.

Tukiachana na lile tukio la Oktoba 7, huko nyuma kabla ya Oktoba 7 jeshi la Netanyahu lilikuwa linatumika kwenda kuvamia makazi ya raia wasiokuwa na hatia, wala silaha yoyote zaidi ya mawe huko WEST BANK (katika ardhi inayokaliwa kimabavu na Israel) kuwachomoa watu katika nyumba zao, kuwapiga, kuwakata, kuwatesa na wengine kuwaua. Halafu nyumba zilizovamiwa walipewa waisrael waziishi. Sasa kiongozi (Netanyahu) unakuaje mahiri kwa kuongoza jeshi linalovamia tu raia na kuua ua hovyo eti kisa waliovamiwa wameokota mawe kuwarushia ili kupinga uvamizi?

Netanyahu na jeshi lake lenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na wengine wa akiba wamekuwa wakitumia vifaru, meli za kivita, ndege zisizokuwa na rubani pamoja na silaha zingine nyingi za kisasa wanazopewa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Canada kufanya mashambulizi ya kupambana na kundi la vijana elf 20 wa Hamas ambao wanatumia silaha za kawaida zilizoundwa kienyeji na wenyewe ili kujilinda. Lakini mpaka sasa Netanyahu amekuwa akionekana kuua watoto wengi na wanawake wasiokuwa na hatia bila kufikia lengo alilolipanga Netanyahu la kuhakikisha mateka wote wamepatikana katika muda mfupi aliopanga.

Netanyahu bado anategemea hela za bajeti ya jeshi, na uchumi wake zitoke katika mataifa mengine ya Ulaya ili aweze kuwalipa wanajeshi wake, kuongeza baadhi ya silaha na zingine ziishie katika tumbo lake na team yake.

So kumfananisha Putin na Netanyahu ni sawa na kumlinganisha hayati mwl Nyerere na bwana mdogo Pole pole hata kama Pole pole anajaribu kuvaa uhalisia wa mwl Nyerere.

Toa na wewe maoni yako, nikatawakilishe mtaani kwa kuangalia wingi wa comment zinazomkubali mmoja wapo ili tumalize ubishi na kufunga mjadala.

Karibuni sana...
Aisee kwa knowledge hii natamani uendelee kutiririka mkuu, madini matupu haya.

Japo kwa uchache tu maoni yangu hii competition tayari ni Void maana unalinganisha watu wasio na Uzani sawa.

Yaani ingekuwa ni kwenye boxing basi ni sawa na kumchukua Mwakinyeo akapigane na AJ pale England kitu ambacho kinawezekana lakini ki-status inakua si fair kwa AJ.

So tafuta Mwamba sahihi kumlinganisha na Putin.
 
Aisee kwa knowledge hii natamani uendelee kutiririka mkuu, madini matupu haya.

Japo kwa uchache tu maoni yangu hii competition tayari ni Void maana unalinganisha watu wasio na Uzani sawa.

Yaani ingekuwa ni kwenye boxing basi ni sawa na kumchukua Mwakinyeo akapigane na AJ pale England kitu ambacho kinawezekana lakini ki-status inakua si fair kwa AJ.

So tafuta Mwamba sahihi kumlinganisha na Putin.
Haya mkuu nimekuelewa 😂😂😂
 
ww unanijua history na unaijua Israel ,na huyu hajui kuwa Iran ndio head of the snake ndio mfadhili wa Hamas Hezbollah houth Yemen n.k

na sio mgambo Hilo ni jina tu ni majeshi Yale sababu hwavai gwanda
Mkuu nafahamu Iran ndiye muanzilishi wa AXIS OF RESISTENCE MIDDLE EAST.
Na unapotaja hiko kitu lazima uitaje Hizbollah,Hamas,Islamic Jihad,Houthi.
Na baba yao Iran kiongozi alikua Qassem Soleiman Mungu amrehemu.
Houthi ni wanamgambo sio jeshi kamili.
Hamas wanamgambo.
Hizbollah wanamgambo.
Na ngojea nikuletee gwanda zao.
Je unataka kusema kuwa M23 ni wanajeshi kisa wanavaa gwanda!?
 
Umemjibu vizuri.. Akija mtandike tena mpaka uzi aukimn
Mkuu umeishia darasa la ngapi?

Mbona mada inahusu Putin na Netanyahu nani zaidi alaf wewe unaleta taarifa za Hams?

Kuna swali nililouliza kuhusu Netanyahu na Hamas?
Huwezi kuacha kuwaunganisha mateka wao n

Mkuu nafahamu Iran ndiye muanzilishi wa AXIS OF RESISTENCE MIDDLE EAST.
Na unapotaja hiko kitu lazima uitaje Hizbollah,Hamas,Islamic Jihad,Houthi.
Na baba yao Iran kiongozi alikua Qassem Soleiman Mungu amrehemu.
Houthi ni wanamgambo sio jeshi kamili.
Hamas wanamgambo.
Hizbollah wanamgambo.
Na ngojea nikuletee gwanda zao.
Je unataka kusema kuwa M23 ni wanajeshi kisa wanavaa gwanda!?
Ww ni mmbobezi kwenye tasnia hii Sina ubishi , ila jina mgambo ni kutofautisha vikosi lakini magereza maliasili mgambo polisi wetu wote wanapitia jeshi ,tofauti ni duets,form six unapita jeshini unajifunza jeshi hivyo wale ni wanajeshi sababu ya mafunzo ya jeshi siyo sawa?
 
ww unanijua history na unaijua Israel ,na huyu hajui kuwa Iran ndio head of the snake ndio mfadhili wa Hamas Hezbollah houth Yemen n.k

na sio mgambo Hilo ni jina tu ni majeshi Yale sababu hwavai gwanda
*Jeshi kaka command centre yake haiwezi kuwa nje ya taifa lake.
Jeshi command centre yake ni katika NCHI YAKE MAMA.
Ikiwa tofauti na hapo hao ni millitias au millitants tu.
Hizi za kwanza nyeusi ni Islamic Jihad hawa ni sehemu ya wanamgambo wa Hamas.wanavaa mavazi meusi yasiyo na mabaka baka,pia hawa mara nyingi huvaa kiraia na wakiwa na silaha kama hivyo,ndio maana watu husema eti wanajichanganya kiraia au hawana gwanda,ila noop hawajichanganyi na raia na mavazi yao mostly ni hivyo.
Screenshot_2024-05-23-13-21-55-36_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg


Hii ya pili ni gwanda ya AL QUDS,sehemu ya wanamgambo wa Hamas pia.
Screenshot_2024-05-23-13-22-58-79_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg


Hii ya tatu hao ni AL QASSAM brigades,sehemu ya wanamgambo wa hamas,na Al qassam ndio brigade mama ya HAMAS au tuseme ndio Hamas wakuu.Hata kipindi cha kubadilishana mateka wao ndio walihusika.
Screenshot_2024-05-23-13-20-57-70_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg


Hawa wanne ndio wazee wa kazi Houthi Yemeni rebels,hata walivyopigana na Saudi Arabia walipigana wakiwa wamevaa hivi hivi na hata msemaji wa Yahya nae huvaa hivi hivi nitaleta gwanda zake.
Screenshot_2024-05-23-13-20-08-86_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg


Hawa ndio HIZBULLAH Lebanon.
Hata wakipigana huvaa hivi hivi.
Screenshot_2024-05-23-13-18-25-47_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg


Kiufupi ambao huvaa mara nyingi nguo za kiraia ila lazima uwakute na bunduki ama bullet proof ni PIJ.
 

Attachments

  • Screenshot_2024-05-23-13-18-25-47_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
    Screenshot_2024-05-23-13-18-25-47_81b5f59f81a9801c9f112972edbe649b.jpg
    243.7 KB · Views: 1
ww hiyo simu yako unaangalizia bongo movie tu ,hili nalo hujui lilitokea ,hakuna silaha zinazoingia Israel marekani ka goma ,Uk Israel anatengeneza silaha na anauza nje na akiba ipo mwendo wa kipondo tu hao marekani wanajipendekeza tu kwa Nyau Israel Yuko vizuri kipato chake ni kuuza technology na matunda nikusaidie kujua Hilo pia ndio mwamba wa technology duniani kaa kwa kutulia Sasa utizame game , ameza kushikilia mifumo ya anga la Irani mwenzio huyo ,hukumsikia gentamicin alichosema
Mkuu unamshambulia hadi Netanyahu mwenzako, kweli leo umeamua kuwa pinga pinga wa kila kitu 😂😂😂
 
Usichokijua Yahudi Anaitawala Russia!
Wataalamu woote wa viwanda vya Silaha ni maYahudi!
Nikumegee kiduchu vita zote za warabu walizo PIGANA na Yahudi muwezeshaji wa Silaha na mbinu za Medani ni mrusi!
Kwa Nini Yahudi aliendeleza Ushindi!
Clinton Alitaka kumgeuzia kibao Yahudi akakumbwa na kashfa kubwa ya ya Uadilifu wake Hadi chupi yake yenye Yenye manii yake ilipelekwa mahakamani kama Ushahidi!
Usicheze na Yahudi.....
 
Ww ni mmbobezi kwenye tasnia hii Sina ubishi , ila jina mgambo ni kutofautisha vikosi lakini magereza maliasili mgambo polisi wetu wote wanapitia jeshi ,tofauti ni duets,form six unapita jeshini unajifunza jeshi hivyo wale ni wanajeshi sababu ya mafunzo ya jeshi siyo sawa?
Kwa nifahamuvyo bro.

*Jeshi ni kundi kubwa la watu waliopokea mafunzo ya mapigano na wenye zana za kivita ambao wako chini ya mamlaka ya kidola/serikali kwa jukumu la kutekeleza maagizo ya dola/serikali husika pamoja na kutetea ama kulinda dola/serikali husika.
Unapotaja jeshi unataja mamlaka yanayotambulika ya kidola.
Mfano JWTZ ya serikali ya Tanzania,IDF ya serikali ya Israel.

*Mgambo ni watu wanaopokea mafunzo ya utumiaji silaha na upiganaji.
Hapa katika mgambo wapo sasa ambao huingizwa katika jeshi kwasababu wao wamepokea mafunzo ya upiganaji na silaha.
Ila wapo wanaoachwa japo wamepokea mafunzo ya upiganaji na silaha.
Mfano walinzi wa SUMA JKT wale ni mgambo.Hawajala kiapo cha jeshi hata mmoja pale.

Sawa na Hizbullah na Hamas.
Hizbullah mamlaka yake ni kundi la Hizbullah sio serikali/dola ya Lebanon.
Al qassam/Alquds mamlaka yake ni kundi la Hamas sio serikali ya Palestina.
Ndio maana ukiulizwa Hizbullah inatumikia serikali gani mkuu unaweza ukajibu!?
Ila ukiulizwa IDF(Israel Defence Force) inatumikia serikali gani unajibu directly serikali ya Israel.
JWTZ inatumikia serikali ipi jibu ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ndio maana Hizbullah au Houthi wakishambulia utasikia wakiripoti Houthi Millitant group/kundi la wanamgambo la Houthi,kwanini hawasemi Houthi Army/jeshi la Houthi??


Kama unafahamu tofauti mkuu utufahamishe.
 
Israel anauza silaha nje alafu ashindwe kujlinda nikwambie Sasa marekani na nchi nyingine za ulaya wanategemea Wana sayansi wa Israel ktk technology ya kisasa wao ndio wanajipeteka Israel kuwekeza na kutoa Fedha by the way Israel ni chaguo la Mungu hivyo ndio unaona unalia kuwa anapewa misaada ni Mungu amesema hivyo ,ww mkataze Mungu awambie wadau wasitoe msaada ,na hata wasipotoa Mungu mwenyewe amesimama na Israel ,mlitegemea Israel ifutike siku Iran kanyesha makombora ? lakini si uliuona mkono wa Mungu kupitia wanadamu alivyozuia makombora
ama ww ni mpagani
Huu uongo ni wa miaka 70 iliyopita. Sasa hivi tunataka ulete uongo mpya angalau unaoweza kufanana na ukweli ndo kidogo tutakuelewa. Ipo wazi kuwa hao unaozungumzia hapa ni wazungu sio waisrael au wayahudi wenyewe wanaofahamika toka miaka hiyo.

Tatizo hamjui kutofautisha kati ya mzungu na myahudi wa kiisrael. Wewe ukiona mzungu kafuga midevu au kavaa kikofia cha nusu kichwa tayari kishipa kishagonga unajua myahudi wa Israel 😂😂😂

Obvious sikatai kuwa hizo nchi za Ulaya na Marekani zina raia wayahudi wenye asili ya Israel. Ni sawa pia zina raia waarab wenye asili ya nchi za kiarab, wahindi wenye asili ya India na mpaka wachina. Ila sasa sio kila mzungu aliefuga midevu akitengeneza ndege tayari mnakimbilia kusema myahudi. Mbona kuna mainjinia wengi tu Marekani wana asili ya China lakini hawapigi kelele, kuna madaktari bingwa kibao Marekani na Ulaya wana asili ya Kihindi lakin hawapigi kelele kwa watu. Lakini nyinyi mkiona mzungu kafuga ndevu tu tayar mshakimbilia katika vyombo vya habari kudai myahudi fulan kafanya hiki na kile utafikiri nyinyi ndio wazazi wa huyo mzungu ambae mwenyew anajua asili yake.

Halaf huu ujinga ni wa miafrika tu lakini weupe wenyewe wala hawana muda na ujinga huo.
 
Kwa nifahamuvyo bro.

*Jeshi ni kundi kubwa la watu waliopokea mafunzo ya mapigano na wenye zana za kivita ambao wako chini ya mamlaka ya kidola/serikali kwa jukumu la kutekeleza maagizo ya dola/serikali husika pamoja na kutetea ama kulinda dola/serikali husika.
Unapotaja jeshi unataja mamlaka yanayotambulika ya kidola.
Mfano JWTZ ya serikali ya Tanzania,IDF ya serikali ya Israel.

*Mgambo ni watu wanaopokea mafunzo ya utumiaji silaha na upiganaji.
Hapa katika mgambo wapo sasa ambao huingizwa katika jeshi kwasababu wao wamepokea mafunzo ya upiganaji na silaha.
Ila wapo wanaoachwa japo wamepokea mafunzo ya upiganaji na silaha.
Mfano walinzi wa SUMA JKT wale ni mgambo.Hawajala kiapo cha jeshi hata mmoja pale.

Sawa na Hizbullah na Hamas.
Hizbullah mamlaka yake ni kundi la Hizbullah sio serikali/dola ya Lebanon.
Al qassam/Alquds mamlaka yake ni kundi la Hamas sio serikali ya Palestina.
Ndio maana ukiulizwa Hizbullah inatumikia serikali gani mkuu unaweza ukajibu!?
Ila ukiulizwa IDF(Israel Defence Force) inatumikia serikali gani unajibu directly serikali ya Israel.
JWTZ inatumikia serikali ipi jibu ni ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kama unafahamu tofauti mkuu utufahamishe.
Uko sahihi Sana mm Sina swali nadhani wengi wamefaidika na mjadala huu hivyo tuendelee kupata changes na ndivyo unaleta fafanuzi nzuri za kielimu
✅✅✅ Big up
 
Vp Hadi Leo Putin haja hukua Ukraine baada 72 hrs ,shida ni nn,lakini pia tunaona Zelensk naye anaharibu na kupunguza uwezo wa Putin pa kubwa tu Hadi kuomba silaha noth Korea ,china ,na Iran
Unazungumziaje hii Mtaalamu !
 
Israel anauza silaha nje alafu ashindwe kujlinda nikwambie Sasa marekani na nchi nyingine za ulaya wanategemea Wana sayansi wa Israel ktk technology ya kisasa wao ndio wanajipeteka Israel kuwekeza na kutoa Fedha by the way Israel ni chaguo la Mungu hivyo ndio unaona unalia kuwa anapewa misaada ni Mungu amesema hivyo ,ww mkataze Mungu awambie wadau wasitoe msaada ,na hata wasipotoa Mungu mwenyewe amesimama na Israel ,mlitegemea Israel ifutike siku Iran kanyesha makombora ? lakini si uliuona mkono wa Mungu kupitia wanadamu alivyozuia makombora
ama ww ni mpagani
Huu uongo wa mungu kuacha kukubariki wewe mgogo na badala yake ambariki myahudi tu peke yake ndo sitaki kuusikia.

Ikiwa hivyo basi Mungu atakuwa hana sifa ya uungu. Atashindwa hata na binadam ambae hawezi kupenda mtoto mmoja na kuchukia wengine na wakati amewazaa mwenyewe.

Kwa akili hiyo ndomaana walisema kuwa waafrika wa zamani walikuwa manyani, maana yaliamini kila yalichoambiwa kwa faida ya wale waliowaambia.

Mchina aliukataa huu upumbavu sasa hivi yuko mbali kiuchumi, kiteknolojia, kijeshi, kibiashara na mambo kibao na wakati miaka 70 iliyopita waafrika wengi tulikuwa tunalingana nae uchumi.

Sisi tumekumbatia fupa la dini linalotulemaza akili na kutufanya tuamini kuwa nchi au mtu mwenye uwezo wa kuendesha dunia ni muisrael peke yake, huku mwenzetu mchina akikwepa fupa hilo na kuingia chimbo kuangalia ni jinsi gani anaweza kuubadilisha uchumi wa nchi yake kutoka katika uchumi wa dunia ya tatu hadi kuwa nchi ya pili kwa uchumi duniani. Kazipita nchi zote za Ulaya, za Asia, za Afrika, za Amerika (ukitoa marekani tu).

Kwa hiki ulichoandika, nimeamini kuwa mpaka sasa bado Afrika kuna ilement za unyani nyani.

Mimi ndio maana naamini katika Mungu, lakini siamini katika dini. Hakuna cha yesu wala mwamed wote ni usanii mtupu uliotumika kutufumbaza waafrika tuibiwe vizuri.

Nasisitiza tena Mungu hana dini na hizo story zako za vitabu vya dini hazina uhalisia wowote. Tujikite katika kuzungumzia yale tunayoyaona yakifanyika sasa hivi. Hayo ya kwenye dini yaliandikwa na wajanja wachache huku sisi tukiwa hatujazaliwa na hakuna ambae anakwenda na kurudi kutupa facts ya vilivyoandikwa katika vitabu vya dini zenu.
 

Attachments

  • FB_IMG_17118944407352949.jpg
    FB_IMG_17118944407352949.jpg
    55.7 KB · Views: 1
  • 13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    107.9 KB · Views: 1
Makombora haijarushwa na serikali ya Iraq bali kundi la kijihadi la Iraq ndio lilirusha.
Nikikwambia huna unalojua utakataa!?
Kuna kundi la Al Quds pale Iraq ndio lilirusha makombora,ila sio serikali ya Iraq kijana.
Huyo myahudi wa dodoma anashindwa hata kujua kwamba hiyo serikali yenyewe ya Iraq iliwekwa na Marekani baada ya kumtoa Sadam Hussein. Sasa watu waliowekwa na Marekani wanawezaje kurusha makombora kuwapiga waliowaweka?
 
Rudia kusoma vizuri ,nimesema ni dhambi Gani Israel ikisaidiwa na magharibi ? mbona Iran inasidiwa na Rusia noth Korea china Hamas Hezbollah houth Yemen na iraq na wengine unawajua ww ndio hoja Sasa we umeleta kitu lingine tofauti
Kijana inaonekana ulokole umeondoka na akili yako kama alivyosema raisi wa China. Kule juu ulisema Urusi inasaidiwa silaha na Iran katika vita vyake.

Hapa tena unabadisha unasema Iran ndo inasaidiwa na Urusi. Mimi naona kuendelea kubishana na wewe ni kupoteza muda. Maana wewe unabisha kwa wazo la kwenda kuonana na yesu mbinguni ndo maana mishipa ya shingo imekushika kupinga kila linaloandikwa liwe la kweli au sio kweli.

Sisi wengine kama ulivyoniita huko juu kuwa ni mpagani (kwa vile sio tusi nakubali) tunapinga na kuongea kwa facts kuhusu kile kinachoendelea katika dunia ya leo na uongo wa wazungu na wayahudi wao wa mchongo pale Mashariki ya kati unaenda kufika mwisho.

Wamefanya kosa kubwa kuuza sim na kusaidia watu wengi kupata taarifa za uhakika kiganjani. Tofauti na zamani jitu linakwambia Israel ndio taifa teule ili wewe ukahiji kwao wao waingize maelfu ya dola kwa njia ya viza na mambo mengine. Au jitu likwambie kuwa myahudi pekee kabarikiwa na Mungu ili popote utapomuona ujihisi wewe ni daraja la pili au tatu kwake. Huu ni utumwa na ujinga wa akili. Mungu hana nchi maalum wala kundi maalum. Nchi zote ni zake na watu wote ni wake. So ubora unaweza kuupata kutokana na matendo yako mazuri kwake. Sio kina Netanyahu wanakubali kutoa vijambio (ushoga) halaf Mungu awaone bora mbele yake. Huyo sio Mungu wa kweli anaepingana na dhambi.

Shtuka mkuu, umeshadanganywa vya kutosha, sasa ni muda wa kushtuka na kutafuta ukweli kupitia akili yako, sio akili ya kina Netanyahu na wahuni wenzake. Wataendelea kukutumia hadi mwisho wa maisha yako bila faida yoyote.
 
Hebu angalia mwaka ambao jamaa walikamatwa na mwaka ambao uchaguzi ulifanyika.

Jamaa wamemuweka Trump mwaka 2016, FBI na CIA wakaja kushtuka mwaka 2018 ishakuwa too late kijana.

Vijana wamefanya kosa kubwa kumfananisha Putin na kibaraka wa wamarekani (Netanyahu)
Speculations hizo;

Mwaka 2016, kabla ya uchaguzi, niliangalia mdaharo kati ya Trump and Hillary Clinton ambapo Hillary alikuwa akimtuhumu Trump kuwa na uhusiano wa Karibu na Putin. Hilary akimtuhumu Trump kuwa kibaraka wa Putin.
Trump alikana Kwa hasira kwamba yeye Hana uhusiano wowote na Putin na Wala hakuna remote yoyote kutoka Moscow ya kuhakikisha Trump anaukwaa uraisi.
Hilary na Trump walikuwa wakirushiana maneno juu ya U-puppet wao (Hilary anamwambia Trump wewe ni puppet wa Putin na wakati huo huo naye Trump akimrudushia maneno makali Hilary kwamba yeye ndiye puppet).

Tafsiri yake nini: kitendo Cha Hilary kuibua shutuma za U-puppet wa Trump = Allegation. FBI & CIA wasingepotezea Kwa kuamini kwamba ule ni mdaharo tu.

Video ni ndefu, labda nikipata wasaa nitakata kipande kinachozungumzia malumbano ya kuhusu Putin intervention.
 
Ebu tutajie hiyo teknolojia iliyo gunduliwa na Israel.
Marekani imeendelea kitekinolojia hata kabla ya Israel haijafikiriwa kuanzishwa saa nyingine mpunguzage ujinga.
Vijana wa 2000 hao, eti na wao wanajiona wayahudi 😂😂😂
 
Back
Top Bottom