PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

Mbona ni nyingi tu?
Syria anapopigwa na Nyau yeye ameruhusu ardhi yake itumike vibaya na Iran kupeleka silaha kwa makundi ya ki gaidi hivyo Lebanon ameruhusu Hezbollah kutumika ardhi yake basi Lebanon Iko vitani na Israel hiyo Iko hivyo
 
Unafananishaje nguvu ya rais wa taifa la watu milioni 150 na milioni 07!!!?? Na unafananishaje Rais Dikteta asiye na ukomo wa kutawala na waziri mkuu wa nchi yenye bunge lenye mamlaka ya kumuondoa waziri mkuu anayechaguliwa kidemokrasia!!!
 
Tatizo una maelezo mengi wakati hoja ni ndogo Sana khs uwezo wa kijeshi wa wahasimu na jinsi wanavyoonyesha uwezo vitani , uwanja ndio unao toa fact sio maneno
tunaona Israel ikikomboa mateka wote Gaza na hao Hamas Hezbollah na babao Iran wana poteana tu sasa
Lete ushahidi mkuu wa mateka kukombolewa.
Maana ripoti inasema takriban mateka 129 bado wapo mikononi mwa Hamas.
Kaskazini mwa Israel raia wamehama hapakaliki kwa vurugu za Hizbollah.
Sasa mkuu unayoyasema mbona yanakinzana na uhalisia!?
 
Asee Putin ni fundi wa kujibu maswali ya ovyo ya media za kimagharibi. Ni hatari mtafute.
Mwanahabari akiuliza swali la ovyo Putin hujibu swali Hilo bila jazba akiwa na tabasamu kuu usoni.
Ajabu zaidi akikujibu swali lako muuliza swali lazima ajione kuku wa kisasa
 
Hapa wafia dini ile akina brazaj wote watamsifia Putin na kumponda Netanyahu, ila ukweli unajulikana, ujuha wa Putin umesababisha malaki wa Urusi kufia nchi ya watu na mpaka leo ameshindwa kufumua hako ka-Ukraine.
Lakini upande wa pili Netanyahu anapambana, na magaidi wa kiislamu ambao wameaminishwa kuifuta Israel, wanajificha kwenye watoto na kina mama, amefumua Gaza na kuifanya shamba, ametuheshimisha.

Unapambanaje na majitu yameaminishwa akili kama hizi, eti analinda dushe lisiharibiwe ili likatumie kugegeda mabikira

View: https://twitter.com/gokulnair/status/1723692097650200995

F-vI1AQXsAAIYZ9

Mada ni ya mwamba Putin na mchumba wake Netanyahu. Usijifiche kwenye udini.

Duniani kuna watu wakristo original kabisa, lakini wanaipinga Israel hii iliyojaa wazungu wa Uingereza, Marekani, Ufaransa, Ujeruman nk kwa sababu ya vitendo vyake vya kikatili. Wao Israel hawaichukulii kwa mlengo wa dini kama unavyofanya wewe mlokole wa tandahimba, bali wanaichukulia kwa matendo yake na kuichukia kwa sababu hizo. Tena wakristo hao ambao wanaichukia Israel kwa vitendo vyao ni wengi ambao wengine hata wewe unawafaham kina hayati mwl J. Nyerere, Mandela, bishop Desmond Tutu (huyu ashaenda mpaka Israel mara kibao tu) , senetor Bernie wa Marekani ambae ni mzungu na mkristo original tofauti na wewe ambae ukristo umeletewa ili iwe rahisi kutawaliwa, kukandamizwa, kuibiwa resource zako, na kufanywa mtumwa.

Ukiangalia hizo picha hapo chini, na kutumia akili yako vizuri kufikiri hiki nilichoandika hapa kwenye comment yako utakubaliana na mimi kuwa hakuna cha taifa teule wala cha dini ya Mungu. Zote zimeletwa na wajanja kwa malengo yao maalum kwa waafrika ambao 99% ni wapumbavu na wajinga.

Tukija kwa upande wa nchi Hispania ni moja ya nchi zenye wakristo wengi katika dunia, lakini leo hii zinaamua kuitambua Palestina kama taifa huru na kuilaani Israel kwa ukatili na ushenzi wake inaofanya kwa watoto na wanawake wasiokuwa na hatia. Hapo bado sijaitaja Ireland, Brazil, Norway nk. Hizo zote ni miongoni mwa nchi za wazungu ambao walikuletea dini uhangaike nayo huku wao wakiwa busy kufanya mambo mengine yenye maana kwa nchi zao.

Tukija kwa waislam kuna nchi nyingi tu za kiislam zinaiunga mkono Israel kama vile Jordan, Saudia nk. So kinachoendelea sasa sio swala la dini au uarab na uyahudi. Bali ni swala la mipaka kati ya Eneo la Israel na lile linajulikana kuwa na mamlaka ya Palestina. Kila mtu aheshim mipaka ya mwenzake, sio kutuma askari kuingia katika ardhi ya wapalestina huko West Bank (ukingo wa magharibi) kuwabaka watoto wa kike, kuwatoa watu katika nyumba zao, kuwafungulia kesi zisizo na mashiko, kuwatesa, kuwapiga na kuwa ua et kisa wewe unapewa silaha na nchi za Magharibi. Halaf na wao wakitumia njia nyingine ambayo wanaona inafaa na wewe kukupa maumivu kama unayowapa wao huko ukingo wa magharibi uanze kuwaita et ni magaidi na kuomba misilaha mikubwa mikubwa upambane nayo.

Ni ujinga na upumbavu kuuchukulia mgogoro wa mashariki ya kati kidini. Maana tumeona dini za kikristo zikiwa upande wa waarab ambao wengi ni waislam na za upande wa kiislam zikiwa upande wa wayahudi ambao wewe unawachukulia kama wakristo.

Sisi wengine tumetumia akili zetu ku reject dini zilizoletwa na meli. Najua Mungu yupo kama walivyokuwa wanajua mababu zetu kabla ya kuja wakoloni. Mungu huyu hana dini, hana nchi au kundi la watu maalum kama wanavyojaribu kutudanganya wayahudi na hata upendeleo wa aina yoyote. Nchi zote ni za kwake na waliopo katika nchi hizo ni viumbe wake wenye haki sawa kwake as long as umefanya yale mema na mazuri hapa duniani.

Hakuna mzazi anaeweza kuwa na watoto kumi. Watoto wampende na kumnyenyekea mzazi wao, alaf yeye aanze kuwanyanyapaa wengine na kusema kuwa anampenda mtoto mmoja tu hata kama mtoto huyo haoneshi upendo kwake. Tumia akili kijana achana na mihemko ya kidini haitokusaidia kitu.

Hoja yetu ni nani ni mwamba wa kweli kati ya Putin na Netanyahu?

Jibu swali.. acha kuzunguka zunguka mbuyu.
 

Attachments

  • FB_IMG_17118944407352949.jpg
    FB_IMG_17118944407352949.jpg
    55.7 KB · Views: 1
  • 13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    13820411_474e176b5f9b4f73a0efd5c863b1537b_jpeg9007ab240faecd3b84b2d425535ccbd1.jpeg
    107.9 KB · Views: 1
Nchi ya Israel ni numbers 8 kwa technology USA ni 2
na Germany ni 4,hapo Rusia Yuko nyuma huko na Iran hawamo kwenye top ten

Hivyo Rusia Iran
hawana ubavu kwa Nyau watulie ,
 
Tuongee yote Putin yuko calm sana kihisia, ni mara chache sana kumuina amepanick au anabwata ovyo...Huwa nawaza huyu jamaa ana roho gani, utafikiri hana hisia.
Yaani mtu anapigwa spana ulimwenguni kote, viongozi wote wa Ulaya, Biden, Trump, Macron wotee ni Putin..Putin, lkn yeye ndo kwanza anatime zake tu...
Netanyahu analialia sana na kutafuta kuonewa huruma ovyo - hii ya ICC tayari kaishaongea mashairi kama yote - kajitetea weee..
Putin hata kujibu hakujibu kuhusu ICC watu ndo walikuwa wanajikanyaga kumchokonoa ...
Watu wenye akili kama wewe ndo mnatakiwa m'comment kwenye huu uzi, sio hawa wengine mtu anaulizwa habari ya Putin na Netanyahu yeye anaruka ruka katika habari zingine utafikiri kuku aliekatwa kichwa alaf akaachiwa akimbie.
 
Netanyahu hashindwi hivyo vita. Shida ni kuwa hamas wamejichanganya na raia na huvaa kiraia pia, jambo ambalo humfanya Netanyahu apate wakati mgumu kumtandika hamasi.
Mkuu umeishia darasa la ngapi?

Mbona mada inahusu Putin na Netanyahu nani zaidi alaf wewe unaleta taarifa za Hams?

Kuna swali nililouliza kuhusu Netanyahu na Hamas?
 
Lete ushahidi mkuu wa mateka kukombolewa.
Maana ripoti inasema takriban mateka 129 bado wapo mikononi mwa Hamas.
Kaskazini mwa Israel raia wamehama hapakaliki kwa vurugu za Hizbollah.
Sasa mkuu unayoyasema mbona yanakinzana na uhalisia!?

Mkuu umeishia darasa la ngapi?

Mbona mada inahusu Putin na Netanyahu nani zaidi alaf wewe unaleta taarifa za Hams?

Kuna swali nililouliza kuhusu Netanyahu na Hamas?
nimejibu angalia
 
Nchi ya Israel ni numbers 8 kwa technology USA ni 2
na Germany ni 4,hapo Rusia Yuko nyuma huko na Iran hawamo kwenye top ten

Hivyo Rusia Iran
hawana ubavu kwa Nyau watulie ,
Where's the facts?
 
Putin ananunua silaha Iran na China tu.
India anatumia sana Israel made weapons,Russia hajawahi kuzitumia wala kununua usitudanganye.
Ila Israel USA ilipeleka mpaka jeshi limsaidie dhidi ya Hamas.
Umemjibu vizuri.. Akija mtandike tena mpaka uzi aukimbie 😂😂
 
Shida ya watoto wa 2000 hawajui hata historia, ndo maana wanaongea kitu wasichokijua, miaka ya 1990 Iraq ikiwa na nguvu sana chini ya Sadam Huseni aliwahi kuipiga Israel na makombora ya Scurd yaliyotengenezwa Rusia, alifanya hivyo hivyo kama Iran ilivyofanya na Israel yakirudisha hata kidogo lakini kilichokuja kutokea Iraq wote tukijua mpaka leo ni failed state, Iran na Israel wako vitani hata kama vita haijatangazwa, tutaona mengi halafu mwisho wa siku tutapata majibu.
Mkuu maliza kwanza kushusha zigo la n'nya hapo chooni halaf ndo usome tena kilichoandikwa na ku comment.

Haiwezekani kani unauliza kati ya Putin na Netanyahu nani ni mwamba wa kweli, alaf wewe unakuja na uharo wako unaozungumzia habari sijui za Iran na Israel.

Hizo mada za Iran na Israel zipo upande mungine ukizitafuta utazipata.

Hapa uzi ni kati ya Putin na Netanyahu basi..

Mbona ulichoandika kishaonesha kuwa wewe ndio wa 2000. Maana haujui hata uelekeo wa mada unasemaje!
 
Nchi ya Israel ni numbers 8 kwa technology USA ni 2
na Germany ni 4,hapo Rusia Yuko nyuma huko na Iran hawamo kwenye top ten

Hivyo Rusia Iran
hawana ubavu kwa Nyau watulie ,
Mkuu kwa technology ipi unazungumzia!?
Hizi tech zina matabaka mkuu.
Ukisema teknolojia ya kilimo Israel ndio taifa la kwanza kuongoza katika teknolojia ya kilimo.
Ukija katika criticak techs China ndio wa kwanza.
Sasa tech ipi unayosema Israel ni ya 8!?
Tutabanaishie usiweke general implication.
 
Unafananishaje nguvu ya rais wa taifa la watu milioni 150 na milioni 07!!!?? Na unafananishaje Rais Dikteta asiye na ukomo wa kutawala na waziri mkuu wa nchi yenye bunge lenye mamlaka ya kumuondoa waziri mkuu anayechaguliwa kidemokrasia!!!
Una uhakika Israel kuna demokrasia!?
Hivi unajua kama Netanyahu anatumia nguvu ya ziada kukaa madarakani!?
Kama kuna demokrasia kwanini raia wanaandamana kuhusu vifungo vya sheria vya uhamisha wa mamlaka!?
 
Hapa wafia dini ile akina brazaj wote watamsifia Putin na kumponda Netanyahu, ila ukweli unajulikana, ujuha wa Putin umesababisha malaki wa Urusi kufia nchi ya watu na mpaka leo ameshindwa kufumua hako ka-Ukraine.
Lakini upande wa pili Netanyahu anapambana, na magaidi wa kiislamu ambao wameaminishwa kuifuta Israel, wanajificha kwenye watoto na kina mama, amefumua Gaza na kuifanya shamba, ametuheshimisha.

Unapambanaje na majitu yameaminishwa akili kama hizi, eti analinda dushe lisiharibiwe ili likatumie kugegeda mabikira

View: https://twitter.com/gokulnair/status/1723692097650200995

F-vI1AQXsAAIYZ9

Ni ukichaa kumlinganisha putin na takataka.kwanza ameshinda vita ya Ukraine Mbele ya nato pia ametengeneza nchi imara ndo maana hata wakiweka sanction hazifanikiwi.
 
Niaje waungwana

Leo nimeamua nilete kwenu uzi huu ili tumalizie ubishi uliopo mtaani kwetu kwa muda wa week tatu sasa bila kumpata mshindi wa kweli, huku kila kundi likivutia kamba upande wake.

Ubishi wenyewe unahusu miamba miwili yenye roho ngumu, maamuzi mazito na misimamo mikali isiyoyumba, wala kuyumbishwa na watu wengine. Na miaka hiyo sio mingine isipokuwa ni raisi wa Russia Vladimir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu.

Kwanza kabla ya watu wengine hawajaingia hapa kutoa maoni yao kuhusu nani bora kati ya raisi Putin na waziri mkuu Netanyahu, naomba kwanza na mimi na mimi nitoe maoni yangu juu ya nani zaidi ya mwenzake.

1. Nikianza na raisi Vladimir Putin, huyu kwangu ni mwamba kweli kweli ambae kumlinganisha na bwege mpenda kulia lia kama Netanyahu ni kumkosea heshima Putin. Netanyahu ni mchumba na hawezi kufit kwa Putin hata kwa nusu ya sifa zake.

Putin ni kiongozi makini, mwenye akili kubwa, misimamo thabiti na intelejensia kali kuliko Netanyahu. Kwa kuthibitisha hili angalia uchaguzi wa uraisi wa 2016 alivyoweza kupachika vijana wake katika mifumo ya Marekani ili wamletee raisi anaemtaka yeye. Ni nani mwengine katika dunia ya leo mwenye uwezo wa kufanya kile alichofanya Putin, tena ndani ya ardhi ya Marekani na mifumo imara ya Marekani? Ni nani mungine?

I hope jibu hakuna maana hata China imeshajaribu kutuma mpaka maputo ili na yenyewe ifanye yake lakini yote yakashushwa. So Putin yeye aliweza tena kwa kuingilia mifumo ya ndani ya nchi bila kugundulika mpaka pale mission yake ilipokamilika, ndo alipokuja kushtukiwa ila akawa ashafanikiwa kwa 100%.

Tukija kwenye misimamo thabiti, jamaa amesimamia kile anachoamini yeye tu, bila kujali vitisho, vikwazo na kelele za nchi za magharibi including NATO. Ameingia nchini Ukraine kukamilisha mission zake bila kujali kelele za mtu yoyote. Si Marekani, NATO wala Umoja wa Ulaya aliethubutu kuingiza jeshi lake Ukraine kupambana na uvamizi wa Russia. Sana sana wameishia kutuma visilaha tu ili kujaribu kudhoofisha mission zake bila mafanikio.

Putin hajawahi kulia hadharani kuwa kaishiwa silaha au mbinu za kijeshi, NEVER. Yeye ni kutoa dozi tu na kusonga mbele daima, huku Marekani na washirika wake wakiendelea kuangamiza silaha zao kuipa Ukraine ili iizuie Ruusia kusonga mbele bila mafanikio.

Putin yeye anapambana na nchi kamili yenye raisi wake, serikali yake, jeshi lake (lenye mamilioni ya wanajeshi), silaha zake (za zamani na kisasa), ulinzi wake (juu na ardhini) Lakini bado haoneshi kushindwa wala kurudi nyuma. Nchi yake bado imeendelea kuogopwa hata na nchi zinazojifanya ni watemi wa dunia. Pia maangamizi yake yamekuwa yakiwalenga zaidi adui zake (wanajeshi na viongozi wa serikali) ikitokea raia ameuwawa basi ni kwa bahati mbaya ile tunaita ajali kazini. Ndiomaana toka vita vianze wanajeshi waliouwawa na wengi kuliko raia wa kawaida.

Putin pamoja na kuwa katika vita vinavyoshirikisha mataifa kibao ya Ulaya kuwa upande wa adui yake, lakini bado economic yake ipo imara mno, na ni nchi ya tatu kwa bajeti kubwa ya kijeshi duniani baada ya Marekani na China. Nchi yake haitegemei bajeti ya kijeshi kutoka nchi yoyote ile hapa duniani. Inajisimamia yenyewe miaka yote ya utawala wa Putin.

2. Tukija kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu, huyu kwangu ni mchumba tu mbele ya Putin, kwa sababu maamuzi yake hutegemea misimamo ya magharibi inasemaje. Yani inaonesha wazi kuwa huwa anapewa maelekeza ya nini cha kufanya na wakubwa zake kutoka huko West, na haswa Marekani.

Kila analolifanya Netanyahu sio ni la kwake bali ni la waliomtuma. Ndomaana wanapocheleweshaga kumtumia silaha za kufanikisha mission aliyopewa, hukimbilia katika vyombo vya habari na kuanza kulalamika kuwa wanamtelekeza na kumuacha apambane kivyake bila msaada wao.

Tukiachana na lile tukio la Oktoba 7, huko nyuma kabla ya Oktoba 7 jeshi la Netanyahu lilikuwa linatumika kwenda kuvamia makazi ya raia wasiokuwa na hatia, wala silaha yoyote zaidi ya mawe huko WEST BANK (katika ardhi inayokaliwa kimabavu na Israel) kuwachomoa watu katika nyumba zao, kuwapiga, kuwakata, kuwatesa na wengine kuwaua. Halafu nyumba zilizovamiwa walipewa waisrael waziishi. Sasa kiongozi (Netanyahu) unakuaje mahiri kwa kuongoza jeshi linalovamia tu raia na kuua ua hovyo eti kisa waliovamiwa wameokota mawe kuwarushia ili kupinga uvamizi?

Netanyahu na jeshi lake lenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na wengine wa akiba wamekuwa wakitumia vifaru, meli za kivita, ndege zisizokuwa na rubani pamoja na silaha zingine nyingi za kisasa wanazopewa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Canada kufanya mashambulizi ya kupambana na kundi la vijana elf 20 wa Hamas ambao wanatumia silaha za kawaida zilizoundwa kienyeji na wenyewe ili kujilinda. Lakini mpaka sasa Netanyahu amekuwa akionekana kuua watoto wengi na wanawake wasiokuwa na hatia bila kufikia lengo alilolipanga Netanyahu la kuhakikisha mateka wote wamepatikana katika muda mfupi aliopanga.

Netanyahu bado anategemea hela za bajeti ya jeshi, na uchumi wake zitoke katika mataifa mengine ya Ulaya ili aweze kuwalipa wanajeshi wake, kuongeza baadhi ya silaha na zingine ziishie katika tumbo lake na team yake.

So kumfananisha Putin na Netanyahu ni sawa na kumlinganisha hayati mwl Nyerere na bwana mdogo Pole pole hata kama Pole pole anajaribu kuvaa uhalisia wa mwl Nyerere.

Toa na wewe maoni yako, nikatawakilishe mtaani kwa kuangalia wingi wa comment zinazomkubali mmoja wapo ili tumalize ubishi na kufunga mjadala.

Karibuni sana...
Nchi ngumu sana hii

Yaani mtu ana muda wa kuhangaika na watu wasio na mpango wowote naye

Tutabaki nyuma tu kwenye maendeleo Kama vijana wetu ndio hawa
 
Back
Top Bottom