PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

PUTIN vs NETANYAHU: Njooni tumalize ubishi wa miamba hii miwili ya dunia

Hezbollah ,na Hamas boss wao ni Iran hivyo ukisema hawana military base ,Wala commanding center sio kweli ,kwani Iran ndio commanding center ,na military base yao ndo maana Israel anapiga kila shehena ya silaha inayotua pale Syria air port inayotoka Iran Hadi hapo hujui command center na military base Hezbollah Hamas Iko wapi ?
Unachanganya mambo bro.
Huo ni uleaji wa kundi la washika silaha.
Leo hii Iran aseme anaacha kufadhili hao watu na Syria iache kutumika na hayo makundi ushajiuliza kitatokea nini!?
 
😂😂😂😂😂😂Mkuu uko serious!?
Mbona unajikanganya!?
Yani ni sawa kusema kuwa kwasababu Hizbollah iko ndani ya Lebanon basi Israel inapigana na Lebabon!?
Iran ndiyo taifa pekee linalofadhili makundi ya washika silaha.
Na hayo makundi yana authority yake tofauti na mataifa yake.
Hapa huna hoja bro hili limeisha.

Tuoneshe sasa hizo technology Israel alizouza kwa USA?
👆👆👆👆👆
Kakwambia nani Lebanoni nchi maskini inakifadhari kikundi cha Hezibollah?
Mfadhari mkuu wa silaha wa Hezibollah ni Iran!
Iran ndiye hasimu mkubwa wa Israel kwa sababu ndiye mfadhiri mkuu wa vikundi hivyo ikiwemo Hezibollah!
Nchi za Qatar,UEA,Uturuki,nk ni moja ya mataifa yanayofadhiri vikundi hivyo.
 
Bado umejibu ukiwa na chuki dhidi ya Israel! Mtaji wa Israel ni ubongo,tecknology nyingi duniani zimebuniwa na Israel!
Marekani ni taifa lenye nguvu kijeshi na kiuchumi lakini bila Israel hana kitu.
Harafu inaonekana hata hujui vikundi vya Hamas,Hezibollah,nk vinafadhiriwa kifedha na silaha na mfadhiri mkuu ni Iran.
Ukitaka kujua haya mambo usiwe mshabiki wala usiegemee upande wo wote.
Ebu tutajie hiyo teknolojia iliyo gunduliwa na Israel.
Marekani imeendelea kitekinolojia hata kabla ya Israel haijafikiriwa kuanzishwa saa nyingine mpunguzage ujinga.
 
Mkuu bishana kwa fact sio kiushabiki.
Isfahan Israel alilenga kushambulia kinu cha nuclear cha Iran ambacho kipo karibia na airbase ya Iran ila shambulio likafeli na mlipuko kutokea katika eneo la wazi la jeshi la anga la Isfahan.
Kuhusu Syria nilishaeleza bro s300 zilizowekwa pale na hizo s400 ni kwaajili ya kulinda kambi ya Russia.
Na mwaka 2022 zilikuwa activated ukanda mzima wa Syria Israel alipoteza fighter jets tatu kwa mpigo.
Nenda kafuatilie habari.

Iron dome haina uwezo kama unaosemea,nenda kafuatie ripoti ya oktoba 7 Hamas aliporusha roketi kwenda Israel.
Hamas alirusha roketi 5000+ hesabu zimedhihirisha roketi 2300+ zilipenya na zilizobaki ndio zikadunguliwa na iron dome.
Iron dome guided rockets/missiles haiwezi kuzuia,hilo limeonekana kaskazini mwa Israel Hizbullah karusha guided missiles na hakuna hata moja Iron dome ilizuia na zote zilileta madhara.

Unapoizungumzia Germany unazungumzia critical technologies mzee.
Kuna gari la Israel we unalipanda!??
Jibu NO.
Ila Tanzania mmezijaza MERCEDES BENZ za kutosha products ya Germany hiyo.
RENAULT pia bila shaka product ya Germany hiyo.
Leta critical technology anazoongoza Israel??
👆👆👆👆Nakuomba hapo tu unijibu mkuu.
Gari ni vitu vidogo dogo,
haijalishi iron dome imepangua makombora mangapi Bado Ina Baki kuwa ya ki pekee duniani nani anayo zaidi ya Israel na vipi isingekuwepo hayo makombora yote yakashuka humo ingekuwa je ,hivyo ukweli unabaki pale Israel ni bingwa wa tech ,japo una fact nyingi za kweli Bado Israel ni mzuri zaidi ktk tech swala la kuunda ndege ni maamuzi tu ,si kwamba hawezi
 
Shida yenu mnaokoteza vitaarifa vya uongo ambavyo CIA na KBG wanatoa ili kuhadaa dunia iamini pumba badala ya ukweli.
Naona umejitutumua wee kuwasifia mashoga, lakini bado kujitutumua kwako hakujasaidia lolote katika mjadala wetu.

Sisi ni watu wazima, na hapa ni JF sio FB wala whatspp. Hivyo unapotoa hoja ya kupinga ukweli nilioandika, unatakiwa uambatanishe na ushahidi ambao unaonesha kuwa Russia haikufanya kile nilichoandika. Mimi nimeweka ushahidi kupitia taarifa zao wenyewe FBI na CIA (pichani), hivyo wenye akili wengi tuliopo humu tulitegemea na wewe ungekuja na ushahidi wa wazi kama huo nilioweka mimi ambao unapinga kile nilichokiandika. Kwa kiswahili chepesi wanasema ushahidi wa maandishi hupingwa kwa ushahidi wa maandishi, sio mipasho mitupu kama hii uliyoandika hapa ambayo mtu yoyote anaweza kukaa chooni kwake akaiandika na kuituma humu.

Haiwezekani Mmarekani mwenyew akubali kuwa vijana wa Putin waliingia Marekani kufanya yao, halaf wewe mgogo wa bongwe uje upingane nao huku ukiwa kijijini kwenu bongwe unalima pili pili.
1. Rusia kuingilia uchaguzi wa USA ni uongo ili kuaminisha wananchi wa USA kuwa Rusia ni ni nchi adui wa USA.
Hili nishajibu hapo juu 👆
2. Matajiri wakubwa, scientists na politician , majenerali wa jeshi la USA na Russia ni wayahudi( waisrael)
Acha ujinga kijana. Dunia ya leo bado unakubali kulishwa propaganda na wachovu wachovu wasioweza kulinda hata mipaka yao wenyewe. Kwa zamani sawa maana sim na mitandao vilikuwa hakuna. Ila kwa leo mtu kudanganywa na waisrael ni ujinga wa hali ya juu maana kila kitu kipo wazi na kinaonekana.

Huwezi kusema et matajiri wakubwa, majenerali wa jeshi na political wa USA na Russia ni waisrael wakati hiyo Israel yenyewe ndio inategemea matajiri wa kizungu kutoka USA, UK, Ufaransa, Ujerumani na nchi zingine za Ulaya waisaidie kijeshi, kiuchumi, kiteknolojia nk.

Kama Israel ingekuwa na uwezo huo wa kutengeneza matajiri na watu wenye uwezo mkubwa wa kijeshi kama unavyosema basi hizo nchi nilizotaja ndio zingekuwa zinahitaji msaada wa kijeshi, kifedha na kiteknolojia kutoka nchi Israel. Lakini badala yake tunaona waisrael ndio wanaowategemea wazungu kwa kila kitu. I mean wanashindwa hata na North Korea wanavikwazo lakini wanajitegemea wenyewe kwa kila kitu. So hizi pumba zako ubaki nazo huko huko kwenu bongwe. Hapa kuna watu wenye akili kukushinda, ambao hatuamini habari kwa kuokoteza vijipropaganda kutoka Sunday school au vijiwe vya kahawa.
3. Israel ni nchi ambayo imezungukwa na maadui pande zote lakini kila nchi ya kiarabu inaiogopa, ina silaha za nyuklia.
Mada inahusu Putin vs Netanyahu

Hao waarab wamekujaje hapa, au ndo kuchanganyikiwa mpaka haujiamini kuandika ukweli kuhusu nani bora kati ya mwamba Putin na mchumba Netanyahu?
4. Netanyahu ana nguvu kubwa za kisiasa kuliko Putin, Israel ni nchi ya kidemokrasia ushindani unakuwa mkubwa sana lakini kwa upande wa Putin anabebwa na mifumo ya nchi ya kiujamaa.
Nguvu kubwa ya kupewa bunduki na mabwana zake ili atumie jeshi lenye wanajeshi zaidi ya milioni 1 kupambana na wanamgambo elf 20 tu ambao hawana ndege wala kifaru cha kivita?

Juzi bwana ake Biden alimtishia kumnyima vibomu kidogo, jamaa kalalamika mpaka koo likakauka mate.

Tukija kwa Putin jamaa anajulikana dunia nzima. Mpaka Tanzania ashafika. Jamaa ni jeshi la mtu mmoja lakini anapigana na nchi zaidi ya 10 huko Ukraine na bado hawajafanikiwa kumnyang'anya maeneo alioyateka 😂😂😂

Ni mwendo wa kuwatembezea vichapo mpaka wanatafutana. Kawekewa vikwazo vya kila aina na marafiki zake mali zao huko Magharibi zimezuiwa lakin mtemi bado hajarudishwa nyuma na wala uchumi wake haujaanguka kama walivyotarajia.
5. USA na Russia wote wanamuogopa Israel, Putin akichanganya kwa Israel unaweza shangaa anaondoka madarakani, ndo maana pale Syria ndege za Israel zinaingia na kutoka na wakati kuna S-300 na S-400 .
6. MOSSAD ni bora kuliko CIA na KBG, ukifuatilia mission ambazo Mossad wamefanya kote dunia ni kali sana.
7. Vita ya 11 ya Dunia USA ndo alimaliza vita baada ya kuipiga Japani na kupeleka ndege na wanajeshi Ujerumani, Poland ndo Rusia walipata nguvu ila jeshi la Russia lilikuwa hoi vibaya.
8. Israel ni nchi ndogo sana ambayo ni sawa na mkoa wa Kilimanjaro lakini haijawahi kushindwa kwenye vita yoyote tangia taifa lao lianze 1948, hiyo ya 2006 kati ya Lebabon na Israel, vita hiyo Israel ilishinda , kupigana na vikundi wanaojificha ndani ya raia siyo jambo jepesi, ndoa maana nchi kama Nigeria wameshinda kuondoa boko haramu.
9. Putin alikuwa kachero ,Netanyahu alikuwa pia kachero wote walikuwa kwenye vikosi vya ELITE Soldiers, Netanyahu amepigana vita na kufanya operation mbalimbali.
10. Uchumi wa Russia na Israel hauwezi kuwa Stable vita ni hasara, ni suala la muda tu uchumi utaporomoka sana tu, ndo maana USA anakwepa vita za nyumbani, ndo maana China anakwepa vita sana hata kama amechokozwa.
Mengine uliyoandika hapa chini ni ujinga na uharo mtupu ambao hata wayahudi wenzako wa bongwa wanaona aibu kuusoma.

Hapa tunahitaji facts kama hizo. Mambo ya mipasho peleka kwa FB au kwa mzee Isufu
 

Attachments

  • Screenshot_20240522-161920.jpg
    Screenshot_20240522-161920.jpg
    274 KB · Views: 1
  • Screenshot_20240522-162029.jpg
    Screenshot_20240522-162029.jpg
    464.3 KB · Views: 1
Niaje waungwana

Leo nimeamua nilete kwenu uzi huu ili tumalizie ubishi uliopo mtaani kwetu kwa muda wa week tatu sasa bila kumpata mshindi wa kweli, huku kila kundi likivutia kamba upande wake.

Ubishi wenyewe unahusu miamba miwili yenye roho ngumu, maamuzi mazito na misimamo mikali isiyoyumba, wala kuyumbishwa na watu wengine. Na miaka hiyo sio mingine isipokuwa ni raisi wa Russia Vladimir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu.

Kwanza kabla ya watu wengine hawajaingia hapa kutoa maoni yao kuhusu nani bora kati ya raisi Putin na waziri mkuu Netanyahu, naomba kwanza na mimi na mimi nitoe maoni yangu juu ya nani zaidi ya mwenzake.

1. Nikianza na raisi Vladimir Putin, huyu kwangu ni mwamba kweli kweli ambae kumlinganisha na bwege mpenda kulia lia kama Netanyahu ni kumkosea heshima Putin. Netanyahu ni mchumba na hawezi kufit kwa Putin hata kwa nusu ya sifa zake.

Putin ni kiongozi makini, mwenye akili kubwa, misimamo thabiti na intelejensia kali kuliko Netanyahu. Kwa kuthibitisha hili angalia uchaguzi wa uraisi wa 2016 alivyoweza kupachika vijana wake katika mifumo ya Marekani ili wamletee raisi anaemtaka yeye. Ni nani mwengine katika dunia ya leo mwenye uwezo wa kufanya kile alichofanya Putin, tena ndani ya ardhi ya Marekani na mifumo imara ya Marekani? Ni nani mungine?

I hope jibu hakuna maana hata China imeshajaribu kutuma mpaka maputo ili na yenyewe ifanye yake lakini yote yakashushwa. So Putin yeye aliweza tena kwa kuingilia mifumo ya ndani ya nchi bila kugundulika mpaka pale mission yake ilipokamilika, ndo alipokuja kushtukiwa ila akawa ashafanikiwa kwa 100%.

Tukija kwenye misimamo thabiti, jamaa amesimamia kile anachoamini yeye tu, bila kujali vitisho, vikwazo na kelele za nchi za magharibi including NATO. Ameingia nchini Ukraine kukamilisha mission zake bila kujali kelele za mtu yoyote. Si Marekani, NATO wala Umoja wa Ulaya aliethubutu kuingiza jeshi lake Ukraine kupambana na uvamizi wa Russia. Sana sana wameishia kutuma visilaha tu ili kujaribu kudhoofisha mission zake bila mafanikio.

Putin hajawahi kulia hadharani kuwa kaishiwa silaha au mbinu za kijeshi, NEVER. Yeye ni kutoa dozi tu na kusonga mbele daima, huku Marekani na washirika wake wakiendelea kuangamiza silaha zao kuipa Ukraine ili iizuie Ruusia kusonga mbele bila mafanikio.

Putin yeye anapambana na nchi kamili yenye raisi wake, serikali yake, jeshi lake (lenye mamilioni ya wanajeshi), silaha zake (za zamani na kisasa), ulinzi wake (juu na ardhini) Lakini bado haoneshi kushindwa wala kurudi nyuma. Nchi yake bado imeendelea kuogopwa hata na nchi zinazojifanya ni watemi wa dunia. Pia maangamizi yake yamekuwa yakiwalenga zaidi adui zake (wanajeshi na viongozi wa serikali) ikitokea raia ameuwawa basi ni kwa bahati mbaya ile tunaita ajali kazini. Ndiomaana toka vita vianze wanajeshi waliouwawa na wengi kuliko raia wa kawaida.

Putin pamoja na kuwa katika vita vinavyoshirikisha mataifa kibao ya Ulaya kuwa upande wa adui yake, lakini bado economic yake ipo imara mno, na ni nchi ya tatu kwa bajeti kubwa ya kijeshi duniani baada ya Marekani na China. Nchi yake haitegemei bajeti ya kijeshi kutoka nchi yoyote ile hapa duniani. Inajisimamia yenyewe miaka yote ya utawala wa Putin.

2. Tukija kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu, huyu kwangu ni mchumba tu mbele ya Putin, kwa sababu maamuzi yake hutegemea misimamo ya magharibi inasemaje. Yani inaonesha wazi kuwa huwa anapewa maelekeza ya nini cha kufanya na wakubwa zake kutoka huko West, na haswa Marekani.

Kila analolifanya Netanyahu sio ni la kwake bali ni la waliomtuma. Ndomaana wanapocheleweshaga kumtumia silaha za kufanikisha mission aliyopewa, hukimbilia katika vyombo vya habari na kuanza kulalamika kuwa wanamtelekeza na kumuacha apambane kivyake bila msaada wao.

Tukiachana na lile tukio la Oktoba 7, huko nyuma kabla ya Oktoba 7 jeshi la Netanyahu lilikuwa linatumika kwenda kuvamia makazi ya raia wasiokuwa na hatia, wala silaha yoyote zaidi ya mawe huko WEST BANK (katika ardhi inayokaliwa kimabavu na Israel) kuwachomoa watu katika nyumba zao, kuwapiga, kuwakata, kuwatesa na wengine kuwaua. Halafu nyumba zilizovamiwa walipewa waisrael waziishi. Sasa kiongozi (Netanyahu) unakuaje mahiri kwa kuongoza jeshi linalovamia tu raia na kuua ua hovyo eti kisa waliovamiwa wameokota mawe kuwarushia ili kupinga uvamizi?

Netanyahu na jeshi lake lenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na wengine wa akiba wamekuwa wakitumia vifaru, meli za kivita, ndege zisizokuwa na rubani pamoja na silaha zingine nyingi za kisasa wanazopewa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Canada kufanya mashambulizi ya kupambana na kundi la vijana elf 20 wa Hamas ambao wanatumia silaha za kawaida zilizoundwa kienyeji na wenyewe ili kujilinda. Lakini mpaka sasa Netanyahu amekuwa akionekana kuua watoto wengi na wanawake wasiokuwa na hatia bila kufikia lengo alilolipanga Netanyahu la kuhakikisha mateka wote wamepatikana katika muda mfupi aliopanga.

Netanyahu bado anategemea hela za bajeti ya jeshi, na uchumi wake zitoke katika mataifa mengine ya Ulaya ili aweze kuwalipa wanajeshi wake, kuongeza baadhi ya silaha na zingine ziishie katika tumbo lake na team yake.

So kumfananisha Putin na Netanyahu ni sawa na kumlinganisha hayati mwl Nyerere na bwana mdogo Pole pole hata kama Pole pole anajaribu kuvaa uhalisia wa mwl Nyerere.

Toa na wewe maoni yako, nikatawakilishe mtaani kwa kuangalia wingi wa comment zinazomkubali mmoja wapo ili tumalize ubishi na kufunga mjadala.

Karibuni sana...
Mmoja anatafutwa na ICC, mwingine bado Majaji wa ICC wanajadili hatima yake.
 
Mbona unaropoka bwana mdogo!?
Israel inasaidiwa kijeshi na USA.
Putina kapigana na Ukraine ikiwa imepatiwa msaada wa kijeshi na mercenaries kutoka NATO na bado Putin anaimudu vita.
Ilhali hiyo Israel Hizbollah tu ya Lebanon inamtoa jasho.
Huyo kijana alikuwa anaandika comment yake akiwa chooni ana nnyaa. Sasa hapo unategemea ataandika kipi cha maana 😂😂.
 
Kakwambia nani Lebanoni nchi maskini inakifadhari kikundi cha Hezibollah?
Mfadhari mkuu wa silaha wa Hezibollah ni Iran!
Iran ndiye hasimu mkubwa wa Israel kwa sababu ndiye mfadhiri mkuu wa vikundi hivyo ikiwemo Hezibollah!
Nchi za Qatar,UEA,Uturuki,nk ni moja ya mataifa yanayofadhiri vikundi hivyo.
Unazunguka na maneno yako mwenyewe.
Embu karudie kusoma nilichoandika huwenda hausomi kwa kuelewa.
Qatar,Turkiye,UAE hawana muunganiko na Hizbullah.
Tena hasa hasa UAE,maana UAE ni rafiki wa USA na Israel.
Na hizbullah ni mashia muarabu sunni/salafi,hawezi kuharibu hela kufadhili wapiganaji wa kishia.
 
Technology zinazidiana hivyo sipingi kuwa German hawana technology nzuri ni wapi ww hujaelewa ww uweke fact hizo tuone kwani mda Gani si uingie google tu upime Israel na German

Duniani Kuna technology anayotumia Israel kama iron dome nani anayo zaidi ya Israel ,Hadi hapo unabishaje kwamba Israel hayupo mbele zaidi ki technology,Iran ilipigwa military air base pamoja na S400 ya Putin ikiwa imeshangaa tu inafyatuka wakati mzigo ushatua
hapo Syria zipo S400 air defense lakini Kila uchao Israel anashinda hapo kupiga airport huyu Nyau ana nn Cha ziada ? ni kwa technology yake Iko anga za mbali Sasa utakuwa umerlewa hapo sija google ni open fact
iron dome imetengenezwa kwa ubia kati ya Marekani na Israel na sio teknolojia ya Israel.
 
KuaEbu tutajie hiyo teknolojia iliyo gunduliwa na Israel.
Marekani imeendelea kitekinolojia hata kabla ya Israel haijafikiriwa kuanzishwa saa nyingine mpunguzage ujinga.
Kuanza technology sio kwamba utabaki kuwa mbele ,china na usa nani alianza na china anaenda mpita usa hiyo siyo hoja
Israel Bado ni bingwa kwani takwimu hamzioni tuzo 9 kati ya kumi Wana sayansi Bora zimeenda Israel
unasemaje Israel Yuko nyuma ktk technology
 
Marekani yy ni kutoa pesa tu akiona una kitu kizuri anajichomeka indeed ni Israel ndio kichwa hapo
 
Gari ni vitu vidogo dogo,
haijalishi iron dome imepangua makombora mangapi Bado Ina Baki kuwa ya ki pekee duniani nani anayo zaidi ya Israel na vipi isingekuwepo hayo makombora yote yakashuka humo ingekuwa je ,hivyo ukweli unabaki pale Israel ni bingwa wa tech ,japo una fact nyingi za kweli Bado Israel ni mzuri zaidi ktk tech swala la kuunda ndege ni maamuzi tu ,si kwamba hawezi
😂😂😂😂😂😂😂😂Mkuu mbona unafurahisha!?
Unaitaje iron dome tech ya hali ya juu ilhali haiwezi kupangua maroketi kiukamilifu!?
Hizo zilizopenya ni roketi tena zenye ufanisi mdogo sana.
Uliwahi kujiuliza kama ingepigwa Ballistic missile yenye ujazo wa nusu tani tena ni guided ballistic missile nini kingetokea!?
Iron dome inamfaa tu Israel.
Ndio maana nchi ilizonunua iron dome ni chache ikiwemo India.

Gari sio vitu vidogo mkuu,TOYOTA jiulize anaingiza mapato kiasi gani kwa uuzaji magari.
Muulize Elon Musk tesla inamuingizia kiasi gani kwa magari ya umeme.
 
Aisee mkuu mleta mada umemkosea sana Putin kwa kumletea uwiano na Netanyahu.
Netanyahu tulitakiwa tumletee uwiano na Hassan Nasrallah.

Rais Vladimir Putin ni bora kwa sababu zifuatazo;
1)Ni miongoni mwa marais wa Russia walioleta mageuzi ya kiuchumi Russia.Miongoni mwa nyakati Russia imepiga hatua kiuchumi basi ni kipindi cha Vladimir Putin.
2)Ni rais mwenye msimamo na maono makubwa katika sera za kijamii,kiuchumi na kisiasa.
3)Ni rais mwenye msimamo na kile anachokisimamia,sio tu mwenye msimamo lakini pia mwenye kujua nini anasimamia na kwa namna gani atakisimamia.
Mathalan tutizame kupinga kwake kutanuka kwa NATO Ulaya mashariki,hili lilipelekea yeye kuingia vitani na Ukraine ila alisimama na msimamo wake,pia alijua namna ya kuchanga karata zake vizuri mpaka sasa mwaka wa pili yuko vitani na uchumi haujaporomoka na wala hafadhiliwi na mtu licha ya vikwazo vyote alivyowekewa.
4)Vladimir Putin ni rais mbabe mwenye jeshi imara,nahisi labda kwasababu na yeye alikua kamanda wa jeshi.Sote tumeona Russia haipigani tu na Ukraine bali na NATO members.Ila imesimama imara kiasi imeteka mpaka silaha za NATO zilizotumwa na NATO Ukraine.
Pia kwa dunia ya sasa hivi mataifa yenye veto power UN moja wapo ni Russia ukiachana na USA,France,Uk,China.
Pia miongoni mwa mataifa yenye usuper power ukiondoa USA,UK na China basi ni Russia.
Russia pia ni taifa tishio ulimwenguni kijeshi.
Hii haiji bila ya kuwa na raisi mwerevu na mwenye misimamo na sera bora kama VLADIMIR PUTIN.

Netanyahu sijaona ubora wake kwasababu ya madhaifu yake yafuatayo;
1)Ana sera bomovu badala ya jengefu,yani ni mtu wa kuwaza matumizi ya nguvu kuliko diplomasia.
Mfano kipindi Netanyahu anakabiliwa na mashitaka ya rushwa aliyekaimu nafasi yake alikua Yair Lapid,huyu Lapid aliweka sera nzuri zilizowaunganisha wayahudi na wapalestina kiasi waisrael waliwekeza biashara kubwa kubwa Gaza na hakukuwa na vurugu.
Ila aliporudi Netanyahu alirudisha mtindo wa kubomoa makazi ya wapalestina ili kupanua makazi ya walowezi wa kiyahudi,ambayo ndio yamechagiza vita ya oktoba 7 2023.
2)Hana sera nzuri za kijamii,kisiasa na kiuchumi,kijamii mfano ni uenezi wa chuki dhidi ya dini tofauti na uyahudi,mfano wa kisiasa ni kutumia kauli za kibabe azungumzapo na mataifa mengine pale yanapompinga,mfano wa kiuchumi ni kuwa yeye amekua waziri kwa muda mrefu Israel lakini alishindwa kuleta sera za kupunguza utegemezi wa kiuchumi nchi ya USA.
3)Mdini.
4)Mbaguzi wa asili.

Kumfananisha Vladimir ma Netanyahu ni sawa na kufananisha perfume na ushuzi.
Dah i feel ya mkuu. Lakini sikumaanisha kumdhalilisha mwamba Putin kwa kumfananisha na mchumba wake Netanyahu. Ni kwa sababu ya ubishi mkubwa uliotokea kitaa mpaka watu wakasema nije nilete hoja hiyo JF ili tupate majibu ya uhakika ya kwenda kumaliza ubishi mtaani.

Kila mtu anafaham kuwa JF ina watu wenye upeo na uwezo mkubwa wa kujua mambo kuliko wa mitaani, japo wajinga wajinga kadhaa waliovamia jukwaa nao wapo, ila haiondoi ukweli kuwa jukwaa bado lina azina kubwa ya watu wenye uelewa mkubwa kama vile wewe, mimi na wengine wengi tu mkuu.
 
Kuanza technology sio kwamba utabaki kuwa mbele ,china na usa nani alianza na china anaenda mpita usa hiyo siyo hoja
Israel Bado ni bingwa kwani takwimu hamzioni tuzo 9 kati ya kumi Wana sayansi Bora zimeenda Israel
unasemaje Israel Yuko nyuma ktk technology
Tutajie teknolojia zilizo gunduliwa na Israel acha kupindisha maneno
 
Hukumsikia Nyau ,tunafanya maamuzi yetunaqq ,akaamsha kipigo Iran ,Kisha kamalizia rapha kakomboa na mateka wote ww uko sitimbi ipi maana unauliza vitu watu wamesha Amina matanga
Una matatizo ya akili au kiswahili kinakupiga jenga?
Umeelewa nilichouliza?
 
Unazunguka na maneno yako mwenyewe.
Embu karudie kusoma nilichoandika huwenda hausomi kwa kuelewa.
Qatar,Turkiye,UAE hawana muunganiko na Hizbullah.
Tena hasa hasa UAE,maana UAE ni rafiki wa USA na Israel.
Na hizbullah ni mashia muarabu sunni/salafi,hawezi kuharibu hela kufadhili wapiganaji wa kishia.
Kuna mahali nimetaja quatary
Unazunguka na maneno yako mwenyewe.
Embu karudie kusoma nilichoandika huwenda hausomi kwa kuelewa.
Qatar,Turkiye,UAE hawana muunganiko na Hizbullah.
Tena hasa hasa UAE,maana UAE ni rafiki wa USA na Israel.
Na hizbullah ni mashia muarabu sunni/salafi,hawezi kuharibu hela kufadhili wapiganaji wa kishia.
Sijataja Quatary ,use, turkey kuwa Wana muumgano na Hezbollah Hamas

hiyo unasema ww
 
😂😂😂😂😂😂Mkuu uko serious!?
Mbona unajikanganya!?
Yani ni sawa kusema kuwa kwasababu Hizbollah iko ndani ya Lebanon basi Israel inapigana na Lebabon!?
Iran ndiyo taifa pekee linalofadhili makundi ya washika silaha.
Na hayo makundi yana authority yake tofauti na mataifa yake.
Hapa huna hoja bro hili limeisha.

Tuoneshe sasa hizo technology Israel alizouza kwa USA?
👆👆👆👆👆
Mbona ni nyingi tu?
 
Tatizo una maelezo mengi wakati hoja ni ndogo Sana khs uwezo wa kijeshi wa wahasimu na jinsi wanavyoonyesha uwezo vitani , uwanja ndio unao toa fact sio maneno
tunaona Israel ikikomboa mateka wote Gaza na hao Hamas Hezbollah na babao Iran wana poteana tu sasa
 
Back
Top Bottom