Niaje waungwana
Leo nimeamua nilete kwenu uzi huu ili tumalizie ubishi uliopo mtaani kwetu kwa muda wa week tatu sasa bila kumpata mshindi wa kweli, huku kila kundi likivutia kamba upande wake.
Ubishi wenyewe unahusu miamba miwili yenye roho ngumu, maamuzi mazito na misimamo mikali isiyoyumba, wala kuyumbishwa na watu wengine. Na miaka hiyo sio mingine isipokuwa ni raisi wa Russia Vladimir Putin na waziri mkuu wa Israel Benjamini Netanyahu.
Kwanza kabla ya watu wengine hawajaingia hapa kutoa maoni yao kuhusu nani bora kati ya raisi Putin na waziri mkuu Netanyahu, naomba kwanza na mimi na mimi nitoe maoni yangu juu ya nani zaidi ya mwenzake.
1. Nikianza na raisi Vladimir Putin, huyu kwangu ni mwamba kweli kweli ambae kumlinganisha na bwege mpenda kulia lia kama Netanyahu ni kumkosea heshima Putin. Netanyahu ni mchumba na hawezi kufit kwa Putin hata kwa nusu ya sifa zake.
Putin ni kiongozi makini, mwenye akili kubwa, misimamo thabiti na intelejensia kali kuliko Netanyahu. Kwa kuthibitisha hili angalia uchaguzi wa uraisi wa 2016 alivyoweza kupachika vijana wake katika mifumo ya Marekani ili wamletee raisi anaemtaka yeye. Ni nani mwengine katika dunia ya leo mwenye uwezo wa kufanya kile alichofanya Putin, tena ndani ya ardhi ya Marekani na mifumo imara ya Marekani? Ni nani mungine?
I hope jibu hakuna maana hata China imeshajaribu kutuma mpaka maputo ili na yenyewe ifanye yake lakini yote yakashushwa. So Putin yeye aliweza tena kwa kuingilia mifumo ya ndani ya nchi bila kugundulika mpaka pale mission yake ilipokamilika, ndo alipokuja kushtukiwa ila akawa ashafanikiwa kwa 100%.
Tukija kwenye misimamo thabiti, jamaa amesimamia kile anachoamini yeye tu, bila kujali vitisho, vikwazo na kelele za nchi za magharibi including NATO. Ameingia nchini Ukraine kukamilisha mission zake bila kujali kelele za mtu yoyote. Si Marekani, NATO wala Umoja wa Ulaya aliethubutu kuingiza jeshi lake Ukraine kupambana na uvamizi wa Russia. Sana sana wameishia kutuma visilaha tu ili kujaribu kudhoofisha mission zake bila mafanikio.
Putin hajawahi kulia hadharani kuwa kaishiwa silaha au mbinu za kijeshi, NEVER. Yeye ni kutoa dozi tu na kusonga mbele daima, huku Marekani na washirika wake wakiendelea kuangamiza silaha zao kuipa Ukraine ili iizuie Ruusia kusonga mbele bila mafanikio.
Putin yeye anapambana na nchi kamili yenye raisi wake, serikali yake, jeshi lake (lenye mamilioni ya wanajeshi), silaha zake (za zamani na kisasa), ulinzi wake (juu na ardhini) Lakini bado haoneshi kushindwa wala kurudi nyuma. Nchi yake bado imeendelea kuogopwa hata na nchi zinazojifanya ni watemi wa dunia. Pia maangamizi yake yamekuwa yakiwalenga zaidi adui zake (wanajeshi na viongozi wa serikali) ikitokea raia ameuwawa basi ni kwa bahati mbaya ile tunaita ajali kazini. Ndiomaana toka vita vianze wanajeshi waliouwawa na wengi kuliko raia wa kawaida.
Putin pamoja na kuwa katika vita vinavyoshirikisha mataifa kibao ya Ulaya kuwa upande wa adui yake, lakini bado economic yake ipo imara mno, na ni nchi ya tatu kwa bajeti kubwa ya kijeshi duniani baada ya Marekani na China. Nchi yake haitegemei bajeti ya kijeshi kutoka nchi yoyote ile hapa duniani. Inajisimamia yenyewe miaka yote ya utawala wa Putin.
2. Tukija kwa waziri mkuu Benjamin Netanyahu, huyu kwangu ni mchumba tu mbele ya Putin, kwa sababu maamuzi yake hutegemea misimamo ya magharibi inasemaje. Yani inaonesha wazi kuwa huwa anapewa maelekeza ya nini cha kufanya na wakubwa zake kutoka huko West, na haswa Marekani.
Kila analolifanya Netanyahu sio ni la kwake bali ni la waliomtuma. Ndomaana wanapocheleweshaga kumtumia silaha za kufanikisha mission aliyopewa, hukimbilia katika vyombo vya habari na kuanza kulalamika kuwa wanamtelekeza na kumuacha apambane kivyake bila msaada wao.
Tukiachana na lile tukio la Oktoba 7, huko nyuma kabla ya Oktoba 7 jeshi la Netanyahu lilikuwa linatumika kwenda kuvamia makazi ya raia wasiokuwa na hatia, wala silaha yoyote zaidi ya mawe huko WEST BANK (katika ardhi inayokaliwa kimabavu na Israel) kuwachomoa watu katika nyumba zao, kuwapiga, kuwakata, kuwatesa na wengine kuwaua. Halafu nyumba zilizovamiwa walipewa waisrael waziishi. Sasa kiongozi (Netanyahu) unakuaje mahiri kwa kuongoza jeshi linalovamia tu raia na kuua ua hovyo eti kisa waliovamiwa wameokota mawe kuwarushia ili kupinga uvamizi?
Netanyahu na jeshi lake lenye wanajeshi zaidi ya laki 2, na wengine wa akiba wamekuwa wakitumia vifaru, meli za kivita, ndege zisizokuwa na rubani pamoja na silaha zingine nyingi za kisasa wanazopewa na Marekani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi na Canada kufanya mashambulizi ya kupambana na kundi la vijana elf 20 wa Hamas ambao wanatumia silaha za kawaida zilizoundwa kienyeji na wenyewe ili kujilinda. Lakini mpaka sasa Netanyahu amekuwa akionekana kuua watoto wengi na wanawake wasiokuwa na hatia bila kufikia lengo alilolipanga Netanyahu la kuhakikisha mateka wote wamepatikana katika muda mfupi aliopanga.
Netanyahu bado anategemea hela za bajeti ya jeshi, na uchumi wake zitoke katika mataifa mengine ya Ulaya ili aweze kuwalipa wanajeshi wake, kuongeza baadhi ya silaha na zingine ziishie katika tumbo lake na team yake.
So kumfananisha Putin na Netanyahu ni sawa na kumlinganisha hayati mwl Nyerere na bwana mdogo Pole pole hata kama Pole pole anajaribu kuvaa uhalisia wa mwl Nyerere.
Toa na wewe maoni yako, nikatawakilishe mtaani kwa kuangalia wingi wa comment zinazomkubali mmoja wapo ili tumalize ubishi na kufunga mjadala.
Karibuni sana...
Aisee mkuu mleta mada umemkosea sana Putin kwa kumletea uwiano na Netanyahu.
Netanyahu tulitakiwa tumletee uwiano na Hassan Nasrallah.
Rais Vladimir Putin ni bora kwa sababu zifuatazo;
1)Ni miongoni mwa marais wa Russia walioleta mageuzi ya kiuchumi Russia.Miongoni mwa nyakati Russia imepiga hatua kiuchumi basi ni kipindi cha Vladimir Putin.
2)Ni rais mwenye msimamo na maono makubwa katika sera za kijamii,kiuchumi na kisiasa.
3)Ni rais mwenye msimamo na kile anachokisimamia,sio tu mwenye msimamo lakini pia mwenye kujua nini anasimamia na kwa namna gani atakisimamia.
Mathalan tutizame kupinga kwake kutanuka kwa NATO Ulaya mashariki,hili lilipelekea yeye kuingia vitani na Ukraine ila alisimama na msimamo wake,pia alijua namna ya kuchanga karata zake vizuri mpaka sasa mwaka wa pili yuko vitani na uchumi haujaporomoka na wala hafadhiliwi na mtu licha ya vikwazo vyote alivyowekewa.
4)Vladimir Putin ni rais mbabe mwenye jeshi imara,nahisi labda kwasababu na yeye alikua kamanda wa jeshi.Sote tumeona Russia haipigani tu na Ukraine bali na NATO members.Ila imesimama imara kiasi imeteka mpaka silaha za NATO zilizotumwa na NATO Ukraine.
Pia kwa dunia ya sasa hivi mataifa yenye veto power UN moja wapo ni Russia ukiachana na USA,France,Uk,China.
Pia miongoni mwa mataifa yenye usuper power ukiondoa USA,UK na China basi ni Russia.
Russia pia ni taifa tishio ulimwenguni kijeshi.
Hii haiji bila ya kuwa na raisi mwerevu na mwenye misimamo na sera bora kama VLADIMIR PUTIN.
Netanyahu sijaona ubora wake kwasababu ya madhaifu yake yafuatayo;
1)Ana sera bomovu badala ya jengefu,yani ni mtu wa kuwaza matumizi ya nguvu kuliko diplomasia.
Mfano kipindi Netanyahu anakabiliwa na mashitaka ya rushwa aliyekaimu nafasi yake alikua Yair Lapid,huyu Lapid aliweka sera nzuri zilizowaunganisha wayahudi na wapalestina kiasi waisrael waliwekeza biashara kubwa kubwa Gaza na hakukuwa na vurugu.
Ila aliporudi Netanyahu alirudisha mtindo wa kubomoa makazi ya wapalestina ili kupanua makazi ya walowezi wa kiyahudi,ambayo ndio yamechagiza vita ya oktoba 7 2023.
2)Hana sera nzuri za kijamii,kisiasa na kiuchumi,kijamii mfano ni uenezi wa chuki dhidi ya dini tofauti na uyahudi,mfano wa kisiasa ni kutumia kauli za kibabe azungumzapo na mataifa mengine pale yanapompinga,mfano wa kiuchumi ni kuwa yeye amekua waziri kwa muda mrefu Israel lakini alishindwa kuleta sera za kupunguza utegemezi wa kiuchumi nchi ya USA.
3)Mdini.
4)Mbaguzi wa asili.
Kumfananisha Vladimir ma Netanyahu ni sawa na kufananisha perfume na ushuzi.