Ni vizuri sana kuheshimiana na kuelimishana maana matusi hayajengi bali yanabomoa tu,yanabomoa mahusiano mema na yanabomoa pia ufahamu tulionao ambao ni bado ni uhusiano Mwema tu.
Kwa sababu hata sisi waumini wa hizi dini sasa hivi tukishambuliana Kwa matusi na kejeli utakuja kushangazwa na hekima na mahusiano na heshima waliopeana manabiii na mitume wa zamani Kwa wapagani wa kipindi hicho na kama kulikuwa na visa na Mikasa ya mapambano basi palikuwa na sababu mujarabu Kabisa Kwa nini mapambano yalitokea.
Lakini Kwa dunia ya sasa na maisha tunayoishi yenye mwingiliano mkubwa wa makabila,tamaduni na desturi na Imani za dini mbali mbali si sahihi kutokuwa na heshima na utulivu Kwa sababu mwisho wa siku lazima tuishi Kwa utengamano Kwa kila mmoja kuwa mtulivu pasipo kumkanyaga mwingine pahala popote Kwa kejeli ama matusi ni vyema kama mmoja hajui au anayo maarifa basi akasema tu Mimi maarifa niliyonayo ni haya na watu wakajifunza au wakamkosoa Kwa utaratibu wa bila kuumizana.
Na kama mmoja hana maarifa au maarifa yake ni pungufu ni vyema akakubali kupewa habari sahihi kutoka upande husika wenye weledi mahsusi kuhusu jambo Fulani tunaloelimishana.
Lakini haya mambo ya kurukia tu na kuanza kejeli kama Yesu alikuwa mwizi tu,mara Mtume Muhammad alikuwa mzinzi tu mara Yesu karuhusu mashoga,mara Mtume Muhammad alikuwa ana maswahaba wanaoingiliwa kinyume pasipo kudhibitisha haya tunayoyapayuka Kwa hasira na dhihaka juu.
Kwa hakika hatumkosei Mwenyezi Mungu tu bali pia tunazikosea hata nafsi zetu pia.
Ukifanya jambo baya kwa mtu,ujue umefanya jambo baya kwa nafsi yako na akili yako pia.
Nayo ni nahisi tu kuropoka Hovyo Kwa dharau na kejeli.
Bora wenye hekima wakae pamoja wajitenge na wapumbavu maana upumbavu unaambukiza Kwa haraka sana na madhara yake yanatokea haraka sana.
Wenye kuwaza sawasawa Kwa pande zote mbili au tatu na zaidi, Waislamu,Wakristu,Imani zingine,na wale wasio amini kwenye uwepo wa Mungu lazima wajiheshimu ili waheshimiwe na wajue mipaka Yao inaishia pale mipaka ya wengine inapoishia.
Kama mtu anazo hoja mujarabu kuhusu Imani yake basi atuelimishe pasipo kutoa lugha kashfu.
Kuna muda unafika inakubidi useme mapungufu ya upande wa pili lakini inakugharimu nini kueleza Kwa lugha yenye stara,Kwa maana hapa ni kama Baraza na kwenye Baraza ama Shura ndugu zangu waislamu wanasema panakaa watu wenye utimamu wa akili.
Tumuombe sana Mwenyezi Mungu atuweke salama mpaka mwisho wa safari zetu.
Sent from my TECNO KG5j using
JamiiForums mobile app