Radi iliyopiga juzi Dar imeacha hasara ya kutosha

Nimesikitika sana baada ya kusoma comments za baadhi ya wadau wakisema Eti earth road inaokoa vifaa vya umeme visipigwe na Radi 😂, huu ni uongo wa Hali ya juu, kinachoweza kulindaa vifaa vyako dhiki ya Radi (lightning) ni Residual Current Circuit Breaker (RCCB) au Residual Current Device (RCD), hizi ni aina ya circuit breaker ambazo ikitokea Radi hujizima automatic, nunua RCCB kampuni ya EUROTRIX utakuja kunishukuru badae.
 
Mkuu Rudi shule, hujajua kazi ya earthing system bado, kama hujui kitu bora unyamaze kuliko kutoa elimu ya uongo.
 
Zilikua zinakunjika lakini sio sasa, nakuthibitishia bado zinakunjika vizuri
 
= earth rod.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga?
Kukosea kuandika sio ujinga ni makosa ya uandishi
Kukosea kuielezea-kutoitumia pindi inapotakiwa huo ndio ujinga

Mala nyingi mjinga hajuagi ujinga wake
Mimi ni mjinga
Je wewe sio mjinga?
 
Hoja kwa hoja, tuepuke kashfa kiongozi wangu, tuko hapa kujifunza. Hebu mkosoe huyu kiongozi kwa hoja ili na Mimi nielimike kupitia Hilo.
Ndio
Itatakiwa anisahihishe kwa maelezo yakinifu
 
Haya toa wewe iyo elimu nijifunze

Nko hapa nakusikiliza mkuu
Kifaa kinacholinda mfumo wako wa umeme dhidi ya Radi ni aina hizi mbili za circuit breaker
1. Residual Current Circuit Breaker (RCCB)
2. Residual Current Device (RCD)
Radi (lightning) inapopiga circuit breaker hizi hu trip (huzima mfumo wote wa umeme), hivi ndio inavyolinda sakiti yako.
Note; binafsi naikubali RCCB kampuni ya EUROTRIX.

Kazi ya earthing system ni;

1. Kumlinda mtu asipigwe na shock ya umeme.
Mfano. Waya wenye umeme (live wire) unapogusa bati la friji, maana ake mtu akigusa lile bati la friji atapigwa na shock ya umeme, badala yake sasa endapo mfumo wako ukiwa na earthing basi umeme wote uliovuja kwenye bati la friji hupelekwa chini ya ardhi, hivyo basi hata mtu akigusa lile bati hatapigwa na shock ya umeme kwa maana umeme tayari unaelekea chini.

2. Kulinda kifaa kisiungue dhidi ya umeme unaovuja.
Mfano. Kama umeme utavuja, yaani waya ukagusa bati la friji kama hujafanya earthing kwenye sakiti yako basi kuna uwezekano wa friji lako kuungua endapo waya mwingine wenye potential tofauti ukagusa bati hilo la friji, endapo utafanya earthing basi umeme wote hupelekwa chini na friji lako litabaki salama.

Note; Earthing system hailindi kifaa dhidi ya Radi (lightning)
 
Mkuu uko sahihi 100
Ila kuna some additional unatakiwa kuzijua pia

Umeme wa radi ni kama maji yaliyomwagwa aridhini
Hayana uelekeo
Umeme una kiwango chake kikizidi ndipo cct breaker inafyatuka
Ikiwa haitafyatuka itaunguza vitu
Ikiwa mfumo wa earth uko sawa umeme huo utaenda aridhini pengine bila ya kuzima cct au bila ya kuunguza vitu
Thus baadhi ya nyumba watu hu link ma paa yao na mfumo wa earth
 
pole ila huo ndio mwanzo tu itaungua hadi nyumba kwa ubahili wa kuweka vitu vya bei nafuu
 
Uko sahihi Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…