Radi iliyopiga juzi Dar imeacha hasara ya kutosha

pole ila huo ndio mwanzo tu itaungua hadi nyumba kwa ubahili wa kuweka vitu vya bei nafuu
Mkuu hapo kitu gani ni cha bei nafuu kilichopelekea TV kuungua baada ya radi kupiga. Maana kwenye wiring sikufanya ya kuungaunga ila bado radi imefanya yake
 
Kuna mtu anatumia sign ya COMMON SENSE IS NOT COMMON, we ukiangalia udongo na tofali la kuchoma vinafanana?
 
Mkuu hapo kitu gani ni cha bei nafuu kilichopelekea TV kuungua baada ya radi kupiga. Maana kwenye wiring sikufanya ya kuungaunga ila bado radi imefanya yake
Hiyo TV guard yako ni bei nafuu, kawaida haitakiwi kuwaka kwa sekunde 90 baada ya umeme kurudi kama ulizima , we unasema umeme haukuwa low voltage kwa hiyo ikaunguza TV. lakini OG bila kujali umeme ni low au High inatakiwa kusubiri mda huo ndio iruhusu umeme kupta.
 
True,
Siku za nyuma pia nilishuhudia radi mpka nikakumbuka BUKOBA

KULE RADI ZINAPIGA MCHANA JUA LINAWAKA
 
Best earth rod nunua copper wire 6mm, uvue gamba suka yako kwa size ya kutosha, hii unakuwa na uhakika maana za kununua unaweza pewa feki kwa bei ya og
 
Mkuu hapo kitu gani ni cha bei nafuu kilichopelekea TV kuungua baada ya radi kupiga. Maana kwenye wiring sikufanya ya kuungaunga ila bado radi imefanya yake
huwez ukawa na vifaa og alafu radi izingue
 
Mkuu fridge guard na power stabilizer huwa zinalinda kifaa dhidi ya low voltage, sio high voltage. Ndio maana umeme ukipungua itasubiri hadi urudi sawa ndio inaruhusu umeme upite. Ikiwa high voltage haizuii na hapo kifaa kinaweza ungua kama ilivyotokea radi. Unless kuna guard na stabilizer mpya za majuzi zinazolinda dhidi ya high voltage, sanasana socket breaker ndio inasaidia kwenye high voltage kwa kujizima
 
Kuna mtu anatumia sign ya COMMON SENSE IS NOT COMMON, we ukiangalia udongo na tofali la kuchoma vinafanana?
Kwahiyo tofali la kuchoma sio kipitishi kizuri cha umeme ila udongo ni kipitishi kizuri cha umeme?
 
Ndio maana nikakwambia hicho ndio kimekuponza, mie nimenunua fridge guard hata umeme ukiwa level ukiwasha unasubiri 90 seconds ndio ina kick in. Kawaida ya fridge haitaki mshituko wa umeme maana inatumia moja kwa moja ndio maana guard yake inatakiwa iwe na delay ikitokea umeme umecheza isiwake moja kwa moja. Unatumia fridge guard ya mchongo.
 
Goba imeshakuwa kama marangu tu, ukitembea hatua Tano unakutana na Manka
 
Sasa kwanini huo umeme unaozidi wakati wa radi, Tanesco wasiwe wanaucollect na kuutunza ukatumika kipindi cha mgao, kuliko kupotea ardhini.??
umeme wa radi hauwezi kuvunwa mkuu na hakuna mtaalamu anayeweza pima megawatts zake
 
Siku nyingine zingatia factor muhimu ndio maana hatutumii stabilizer kwenye fridge ikawepo fridge guard. Pia uelewe tofauti stabilizer umeme ukiwa chini inauboost uendelee kutumia, kuna buck-boost conveter ndani yake umeme hata ukizidi inaurudisha level.
 

Attachments

  • fg.png
    20.4 KB · Views: 4

Kwahiyo tofali la kuchoma sio kipitishi kizuri cha umeme ila udongo ni kipitishi kizuri cha umeme?
inachofanya udongo uruhusu umeme kupita n ule umaji maji ndani yake ukiwa mkavu umeme haupiti
 
Ndicho nilichokuambia kuwa hizi fridge guard zinalinda vifaa dhidi ya umeme wa low voltage ambao unaunguzaga sana vitu pia, ila hazilindi dhidi ya high voltage, unless kuna za kisasa zaidi zimetoka majuzi
 
Mkuu toa ushauri Earthrod ipi inashauriwa kwa mziki wa radi za Rukwa maana nipo kwenye ujenzi eneo ambalo radi kwakweli ndio kama nyumbani kwake.
Huko radi nyingi ni za kiutamaduni, mnatengeneza radi zenu wenyewe.
 
Uko sawa lakin kama earthing system haiko vizur hiyo circut breaker itachelewa kusensi kwa haraka hence unaunguza vitu kwahiyo huwa vinategemeana earthing system na circuit breaker
 
radi inapiga thena umeme unaunguza vyombo? Maana yake Radi iliongeza voltage za umeme?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…