Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

Mwambie jamaa yako aache tabia ya mazoea na mkeo pia mwambie akiendelea utamuinamisha na urafiki wenu ufike mwisho.
 
Mkuu Fanya hivi....

Muite rafiki yako nyumbani mwambie umepata taarifa amemtongoza mkeo.

mwambie akae mbali na Familia yako kama anataka kuishi. Usiendelee mbali ishia hapo.

ukimaliza mwambie umemaliza aondoke haraka nyumbani kwako maana hautaki kumwona mtu asiye na heshima ndani kwako.

kumbuka mkeo amekuambia ili uchukue hatua usipochukua hatua kijamaa kitaendelea kumtongoza na lolote linaweza kutokea.
Hahahaahaa. Wakuu mnafeli. Hapo mjinga ni mke. Angeweza ihandle situation vizuri sana. Sasa hapo kasababisha shida mbili au tatu. Moja, hajiamini na hawezi tatua mitongozo kwani kuna siku ataliwa na hatasema, Mbili, kashamsababishia mumewe msongo wa mawazo maana kwanza yuko mbali,na kila siku atahitaji updates kama jamaa anaendelea mtongoza au lah, shida kubwa sana hii hata kazini unaeeza anza underperform. Tatu mke anapima kina cha maji, mume atareact vipi!? Anapima upumbavu. Na mwanamke mwenye tabia hizo anakuwa anajihami, hata ikiingia message "i miss u" ujue ni mpuuzi tu yule anayemtongoza mke wangu kumbe wanakulana.
Ushauri wa bure. Muwe makini , type ya mke wa hivyo kuliwa rahisi sana
 
Hivi nyie mnaomshauri jamaa apotezee maneno ya mke wake mshafikiria visa vya wanawake ....Yan hapo kutokuchukua hatua unampa point tatu muhimu mke....mke kashakwambia anafuatiliwa...we jamaa ni simple tu ubaya ubaya piga chini huyo rafiki tena mchimbe mkwara wa maana ...
Iwe mwanzo na mwisho kufika kwako naurafiki uishe siku hiyohiyo,..kusudi ikitokea siku wako pamoja utajua wote ni wasaliti na pia itakuwa raisi sana kutake further actions
Huwajui wanawake mkuu.. Na hivi jamaa yuko mbali amini kuna Kitu cha ovyoo huyo mwanamke wa jamaa kafanya na Mwanamke kaona njia rahisi ya kumfanya rafiki wa jamaa asiseme ni Kuwafitinishaaa... kwenye hii kesi naamini mwanamke kazingua mahali na rafiki wa jamaa kajua asilimi 90.. asilimia 10 inaweza kuwa kweli jamaa anamtongoza.

So jamaa atulize kichwa asiamue hii kesi kwa mihemkooo
 
Humu kuna watu walegevu sana ....bro mkeo anaakili sana,hao wanaokwambia eti umkanye asiwe anakwambia pindi mtu anapomtongoza wamepotea...skia mkuu take it positively...Ikiwa kila mkeo ikitongozwa aje aseme atasema kea wangapi...?mkeo amepima urafiki wenu na pengine kasumbuka sana alieamini we ndio kimbilio...sasa mvae huyo jamaa kwa ukatili ili iwe fundisho..

Ukipuuzia mkeo atatafunwa kimasihara halafu utakuja kulialia humu
Note:hakikisha una solid proof unavomchana jamaa
 
Shekhe wangu,wewe sio wa kuandika hivi,unanidis-appoint mimi shabiki yako. Omba maghfila kwa mola wako.Chunga vidole vyako kabla hujaandika.
Astaghafirullah.. Astaghafirullah, Astaghafirullah 🤲


Ni kweli nimekosea kaka, japo niliandika kama masihara, 😔
 
Mkuu kwanza pole sana mke anauma sana aisee sisi tulio oa ndio tunajua,
We kaa na mkeo ndugu usiache kila siku kumfundisha na kumuonya taratibu taratibu na kum care usiache kumkumbusha mmetoka wapi na mnakokwenda ni wapi,
Halafu wewe cha msingi muite huyo jamaa upate na mtu mwingine umshauri jamaa aache kumtongoza mke wako.
Kuwa makini sana watu wanao kuja kwako halafu wanakuwa na mazoea ya kupitiliza kumuita mkeo shemeji shemeji kaa nao mbali.
Halafu maneno ya vijana wa humu acha nayo maana mengine yatakuumiza.
 
Huwajui wanawake mkuu.. Na hivi jamaa yuko mbali amini kuna Kitu cha ovyoo huyo mwanamke wa jamaa kafanya na Mwanamke kaona njia rahisi ya kumfanya rafiki wa jamaa asiseme ni Kuwafitinishaaa... kwenye hii kesi naamini mwanamke kazingua mahali na rafiki wa jamaa kajua asilimi 90.. asilimia 10 inaweza kuwa kweli jamaa anamtongoza.

So jamaa atulize kichwa asiamue hii kesi kwa mihemkooo
Wanawake tuende nao kwa hekima sana mkuu. Kuna dada mmoja ni rafiki wa karibu sana. Mmewe yuko mbali! Anatongozwa sana. Sasa siku moja alinionyesha mtongozo mmoja kwa simu yake jamaa anamsifia sanaa nikamuuliza sasa,mbona hudelete huu ujinga je mme wako akiona!?? Akasema eti mume wake yuko aware na situation na message anazisoma. Nikasikitika sana nikasema hamna mke humoo.
 
Very wrong advice! Kama hizi ndizo busara za wazee basi tumeliwa. Jamaa amesema kabisa kuwa amemsumbua sana. Kutongozw kwa kawaida kupo ila ukiona rafiki yako anayekuheshimu na anakuja mpaka kwenu halafu anamtongozo mkeo basi ujue huyo rafiki anakudharau na unastahili kumwonyesha kuwa yeye ni mjinga kuliko wewe.

Sasa unafikiri mwanamke anatongozwa na watu wangapi?
Huyo rafiki yeye akiona anapikiwa anadhani anapendwa kimahaba
Elewa kuwa wapo watu wenye tabia za hivyo Yaani kutongoza kila mtu haijalishi ni mke wa nani

Nimeona watu wa hivyo wengi tu
Yeye mke anashindwa hata kumwagia maji tu
Huyo sio rafiki kwani hana heshima
Kama ameisha ambiwa Basi achukue hatua anayoona inafaa
Ila kumbuka anatongozwa na wengi utapiga wote?
 
Mwambie mkeo ampigie simu Kisha amrekodi then umtumie hiyo voice huyo jamaa
Au mwambie mkeo ascreen shot message ambazo huwa anatumia kumtongoza then akurushie halafu ziforward kwa huyo jamaa kupitia namba yako
 
Sio rahisi Mwanamke ataongozwe au aliwe na rafiki yako halafu akuambie,lazima kuna issue kubwa kati ya Mkeo&rafiki yako-kuna kitu hakipo sasa Mkeo anatafuta namna ya kujinasua.
 
sasa mvae huyo jamaa kwa ukatili ili iwe fundisho
Huoni sasa kama hili ni tatizo tayari. Yani mke angeweza muonya jamaa astop na asirudie tena. Unafika huku kuvaana kikatili ili ajeruhi au aue aende jela. Then
 
Ogopa sanaa mkeo kukwambia anatongozwa na fulani hivi huyo mkeo muulize tu ni wanaume wangapi wanakutongoza kila siku je huwa unakuja kuniambia umetongozwa? Achana na huo ujinga mwambie alimalize mwenyewe mbona akitongozwa na wengine haji kukwambia. Potezea huo upumbavu fanya ya msingi
Umejuje kama anatongozwa na wengine?? Acheni kutuoa ushauri wa kipumbavu bana
 
Sasa unafikiri mwanamke anatongozwa na watu wangapi?
Huyo rafiki yeye akiona anapikiwa anadhani anapendwa kimahaba
Elewa kuwa wapo watu wenye tabia za hivyo Yaani kutongoza kila mtu haijalishi ni mke wa nani

Nimeona watu wa hivyo wengi tu
Yeye mke anashindwa hata kumwagia maji tu
Huyo sio rafiki kwani hana heshima
Kama ameisha ambiwa Basi achukue hatua anayoona inafaa
Ila kumbuka anatongozwa na wengi utapiga wote?
Nimekuelewa sana mkuu. Najua kwa Afrika ni nadra sana mwanamke atoke nyumbani, kama yuko peke yake na asitupiwe maneno na wanaume. Ila hili ni tofauti. Wewe una rafiki na mnaheshiana sana na pengine hata kwenye shida mnasaidiana. Umepata safari una unaporudi unaambiwa alikuja nyumbani kwako anamhangaisha mke wako. Na siyo mara moja. Haki lazima uwe mtu wa ajabu sana kama utamkaripia mkeo ni kwa nini amekuambia! Tena atadhani ni wewe ulimtuma na pengine mna tabia ya kuchangia wake zenu. Nachosisitiza mimi ni hili la mtu kama rafiki au jirani kujua kabisa huyu ni mke wa mtu na ankujua halafu akawa anamsumbua mke wako wakiti anajua hali halisi.
 
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.

Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa.
Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.

Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie.
Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipiga simu tunaongea vizuri tu.

Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Hahahaa mwambie wife akutajie na mwingine mmoja ambaye amemtongoza akamkubalia
 
Back
Top Bottom