Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

Ulimwengu wa SAsa ni mbaya Sana watu hawaheshimu ndoa, na hata awajui nini maana ya ndoa. Hili janga ni kumuomba Mungu tu azidi kukufunika pazia usiyone ya mwenza wako. Ndoa imekua kama ni kituo tu cha makutano. Na kwa hali ya sasa kujiandaa kisaikolojia ni muhimu Ili upatapo taarifa yeyeto mbaya isiathiri maisha yako, maana kuna wenza mshipa wa aibu ulishakata kitambo.
 
Mi naona umenena vema,tusitawaliwe na hasira.
Kitendo cha mke kutongozwa alafu wewe unachukia kiasi hiki,je kama angefanyiwa kingine zaidi na ukajua si yangetokea yale ya Mwanza?

Jiulize,utawafokea wangapi?
Kuna muda anasafiri nawe haupo je,hao nao utawafokea?

Zaidi mpe mbinu za kuwakatisha tamaa wale wote watakaojaribu kumfata,na zaidi unatakiwa umwombe akushirikishe kila akikutana na vishawishi.Hii itakuwezesha kumsaidia mbinu za kuwapiga chini tena kwa kuwaaibisha!
Wanaume sisi kwa KE ni mafisi!
Issue si kutongozwa, issue kubwa ni kutongozwa na mtu ambae ulijua kuwa rafiki yako tena ni rafiki mkubwa.

Na hii inawezekana hata shemeji ikampelekea kumwambia braza, (mumewe).

Wanawake wana tongozwa sana kama vile wanaume wanavyotongoza, mwanamke hutongozwa na mwanaume hutongoza mwanamke.
 
Ila wanaume wa kibongo unaendaje kwa mwanamke aloolewa mmewe hayupo unatafuta nin?
Na nyie wanaume kwanin mnazoesha marafiki zenu nyumbani kwa wake zenu onaneni bar inatosha kila mtu arudi kwake,mtu keshoa unaenda kwake kufanya nin

Watu wengine hawafuatilii mafunzo hata ya kimila na dini
Labda hawakufunzwa ila watafunzwa na ulimwengu

Mbona kote tumefundishwa hayo
Mke hawezi kumfungulia mtu nyumba kama mume hayupo
Maana mkiwa wawili katikati yenu ni shetani mshawishi

Mimi sithubutu hata nyumba za ndugu zangu wa damu kuingia ndani kama hawapo
Nikae na mke wa mdogo wangu tuongee nini kwa mfano
Kama hayupo nasepa
Sasa itakuwa mtu baki ndio aibu kabisa

Na wanawake pia unamfunguliaje mlango mtu na upo peke yako?
Halafu eti unampikia na chai kabisa au chakula huku kajitanua kwenye makochi?

Aibu tupu kwa wote kama wanakubali hayo
Sio wivu bali ni maadili mema
 
technically huyo mkeo hajampenda rafiki yako
angempenda asingekwambia
hao ndio wanawake
We jamaa naona umeongea ukweli na huyu mleta maada inabidi auzingatie.
Ukweli ni kwamba wake zetu wanatongozwa sana tu. Na huyo mke wa jamaa vilevile anatongozwa huko nje, ni yeye uamuzi wake kuwakubali au kuwakataa. Lakini je, hao wote wanaomtongoza anamjulisha mumewe? Jibu ni hapana. Sasa kwanini atoe taarifa baada ya kutongozwa na shemejie?
 
Sio bongo tu, ni hivyo duniani kote
Ila wanaume wa kibongo unaendaje kwa mwanamke aloolewa mmewe hayupo unatafuta nin?
Na nyie wanaume kwanin mnazoesha marafiki zenu nyumbani kwa wake zenu onaneni bar inatosha kila mtu arudi kwake,mtu keshoa unaenda kwake kufanya nin
 
Ushauri wangu, baada ya kupewa taarifa hiyo ungemjibu kama wengi walivyoshauri humu, kwamba wangapi wanakutongoza na huji kuniambia?? Na umpotezee wife wako.
Then vuta muda mrefu bila kuitembelea familia yako wala kuuliza chochote kama jamaa aliendelea kumfatilia au la.
Then panga siku yako ambayo yeye mkeo hakutarajii. Fika nyumbani usiku bila taarifa then omba simu moja kwa moja. Ikague then uje kutupa feedback.
 
Angalia hiyo isije ikawa kesi Kama ile ya Yusufu na mke wa Pontifa.
 

Attachments

  • download.jpeg
    download.jpeg
    4.5 KB · Views: 14
Ila urafiki hadi kupikiwa chakula?
Huo moyo mnautoaga wapi?
Mke wangu aingie jikoni kisa rafiki?
Sijawa mtumwa hivyo.
 
Huna rafiki hapo Mzee,kwanza nashangaa unaendelea kumuita rafiki yako. Mtuwa namna hiyo kwa tamaa alizonazo Yuko tayari akutie hata uhai hafai
 
Hata kama sijamuwekea ndio aitumie kwa mke wangu? Mbona wanawake wengi sana ambao hawajaolewa
Mimi Mzee wangu Kuna kauli aliwahi kuniambia kuhusu marafiki na kila Mara huwa naprove.."Mwanaume Hana marafiki Ila ana jamaa tu,tena haipendezi kupeleka hao unaowaita marafiki nyumbani unajitengenezea bomu"
 
Ogopa sanaa mkeo kukwambia anatongozwa na fulani hivi huyo mkeo muulize tu ni wanaume wangapi wanakutongoza kila siku je huwa unakuja kuniambia umetongozwa? Achana na huo ujinga mwambie alimalize mwenyewe mbona akitongozwa na wengine haji kukwambia. Potezea huo upumbavu fanya ya msingi
Umeongea jambo jema
 
Mwambie mkeo kuwa yeye ni mtu mzima na anajua namna ya kuenenda kama mke wa mtu.. Na huyo rafiki yako usimwambie chochote, na urafiki wenu uendelee kama hakuna jambo lililo tokea. Kijana, masuala ya mahusiano ya kimapenzi chukulia kama ni nonsense katika maisha yako
 
Usiskilize maneno ya mkeo, ananisingizia tu!
Mimi na wewe forever and for always, mwanamke asifanye tuvunje urafiki wetu
[emoji26][emoji26]
 
Hivi nyie mnaomshauri jamaa apotezee maneno ya mke wake mshafikiria visa vya wanawake ....Yan hapo kutokuchukua hatua unampa point tatu muhimu mke....mke kashakwambia anafuatiliwa...we jamaa ni simple tu ubaya ubaya piga chini huyo rafiki tena mchimbe mkwara wa maana ...
Iwe mwanzo na mwisho kufika kwako naurafiki uishe siku hiyohiyo,..kusudi ikitokea siku wako pamoja utajua wote ni wasaliti na pia itakuwa raisi sana kutake further actions
 
Mtengenezee mtego wa kumkamata ugoni. Ukishamkamata mchaji hela kibao ili iwe funzo kwake na kwa rafiki wengine.
Hilo haliwezi kuwa funzo!!! litakuwa ni kama kosa la barabarani traffic unalipa fine tu yanaisha. Dawa yao hao ni kuchezea linda tu
 
Back
Top Bottom