Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

Rafiki yako akimtongoza mke wako umfanye nini?

MChane live kama domo zege MChane kupitia message, bora urafiki ufe.
 
Tumia hekima na busara kwenye hili.Jaribu kuwa mtulivu na jiepushe kutokuwa na mhemko na papara.Fanya uchunguzi wa kutosha kwa umakini mkubwa.Hujawajua wanawake na fitina zao!!!

Tatizo
kama lako liliwahi kunikuta kumbe rafiki yangu aligundua madhaifu makubwa ya mke wangu akapanga kuja kunipa taarifa zote kuhusu hayo madhaifu, bibie akafahamu, ilitengenezwa fitina mpaka uhusiano ukaelekea kuvunjika.Yule rafiki yangu aliniambia kauli moja tu "Jipe muda utaelewa tu, sasa hivi huwezi kunielewa, nakupenda sana rafiki yangu kwani tumetoka mbali sana"!!

Huo muda na majibu yake!!! Nilimuomba Msamaha mara 100.Ndoa ikafa.!!!!!Tuliza akili!!!
Kama mtu anakugombanisha na mama yako itakuwa rafiki yako??? Tumia hekima.
Nb:
Anaweza kuwa mkweli au muongo. Mwanamke kutongozwa si tukio la ajabu na kushangaza.
 
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.
Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa.
Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.
Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie.
Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipiga simu tunaongea vizuri tu.
Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Huyo mlie timing tuu, weka mtego. Mwambie wife aanze kuonyesha ishara za kumkubalia...then mnamsetia ambush matata.
 
Ogopa sanaa mkeo kukwambia anatongozwa na fulani hivi huyo mkeo muulize tu ni wanaume wangapi wanakutongoza kila siku je huwa unakuja kuniambia umetongozwa? Achana na huo ujinga mwambie alimalize mwenyewe mbonaakitongozwa na wengine haji kukwambia. Potezea huo upumbavu fanya ya msingi
Hayo ndo yalikua Mawazo Yangu pia!
 
Ukiona mkeo amekwambia kuwa kuna mtu Fulani anamtongoza wewe lala usingizi mzuri tu coz nachojua mke akitongozwa na akampenda huyo mtu hawezi kukuhadithia. Kunasiku nilishampa wife makavu live baada ya kuniambia kunamtu Fulani anamtongoza, nikamjibu inamaana miaka yote miliwi tunaishi pamoja inamaana huyo tu ndio kakutongoza? Unaowapenda wakikutongoza mbona huniambii? Nikamwambia acha hizo swaga.
😂😂😂
 
Aisee uwe makini saaana katika hili kijana

Yawezekana mkeo luna mishe zake za kidwanzi kafanya na rafiko yako kazijua, ili kuepusha hilo kwani kama mnashibana akaona inshu ni kuwagombanisha na njia nzuri ni kusema anatongozwa.

Unaweza kuta jamaa anakukusanyia data nyingi ili ukija mkae kiume mzungumze na hataki kukupanikisha sasa mkeo kajua na anatafuta namna ya kumkwamisha jamaaa

Note:
Mwanamke wa busara anajua kutongozwa ndio maisha yake ya kila siku, kuanza kuchagua kukueleza ni kutaka kukua au kua ndoa kisaikolojia
Nimelipokea mkuu
 
Tangaza kiama kwani kuua tsh ngapi....huyo sio rafiki tena
Ni adui yako namba moja, ingekuwa sio rafiki yako ungefanyaje. Kill him immediately kabla hajageuka mwiba kwako.
Kuua hapana, labda kumpiga tukio ambalo hatasahau
 
Nimeoa naishi na mke wangu vizuri tu japo changamoto hazikosekani. Nilikuwa nafanya kazi ofisi moja na rafiki yangu ambaye tulikutana kwenye interview na kuajiriwa pamoja.
Nilioa kabla yeye hajaoa, akawa amezoea sana kuja kwangu na shemeji nyingi hata akikuta msosi umeisha atapikiwa.
Miezi miwili iliyopita nilipata uhamisho kwenda mkoa mwingine nikamuacha mke wangu kwani nae ana biashara zake.
Juzi kaniambia rafiki yangu anamtongoza, anasema amejitahidi kuvumilia lakini ameshindwa usumbufu umezidi ameona bora aniambie.
Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipiga simu tunaongea vizuri tu.
Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.

Kusanya ushahidi umtie Mbata
 
Mimi nina Marafiki zangu wa karibu sana tangu walipooa mpaka sasahivi wote wana Watoto wengine wawili mwingine mmoja SIJAWAHI KUFIKA NYUMBANI KWAO.

Sasa nafuata nini? Kama tunakutana kwingine na tunawasiliana kwa simu inatosha

Unaweza kwenda kwake aidha ukamtamani mke wake au Mke wake akakushobokea wewe.

Tuache mazoea ya kwenda kwa watu mpaka kupikiwa chakula. Uswahili wa hovyo huo.
 
Mkuu mbona jibu ni rahisi mpigie simu au kutana nae umwambie laivu kabisa masuala ya kumtongoza mke wangu uache.
atanywea awe mtu wa kutia huruma sana akikitana na mkewe,siku jamaa sasa akimzingua mkewe.mke anaenda kumpa mshikaji mpaka nyuma.

haya mambo ni magumu sana.
 
Ogopa sanaa mkeo kukwambia anatongozwa na fulani hivi huyo mkeo muulize tu ni wanaume wangapi wanakutongoza kila siku je huwa unakuja kuniambia umetongozwa? Achana na huo ujinga mwambie alimalize mwenyewe mbonaakitongozwa na wengine haji kukwambia. Potezea huo upumbavu fanya ya msingi
Mi naona umenena vema,tusitawaliwe na hasira.
Kitendo cha mke kutongozwa alafu wewe unachukia kiasi hiki,je kama angefanyiwa kingine zaidi na ukajua si yangetokea yale ya Mwanza?

Jiulize,utawafokea wangapi?
Kuna muda anasafiri nawe haupo je,hao nao utawafokea?

Zaidi mpe mbinu za kuwakatisha tamaa wale wote watakaojaribu kumfata,na zaidi unatakiwa umwombe akushirikishe kila akikutana na vishawishi.Hii itakuwezesha kumsaidia mbinu za kuwapiga chini tena kwa kuwaaibisha!
Wanaume sisi kwa KE ni mafisi!
 
Jamaa huwa hatumi meseji yeye ni kupiga simu na kuongea live. Nitamwambia aanze kumrekodi
Mwambie shemeji akipiga tena amwambie yupo sehemu ambaya kiasi kwamba hawezi kuonge kwa hiyo basi wawe wanawasiliana kwa arafa (message) kwa muda huo, ili uwe ushaidi wako.
 
Mpaka sasa rafiki yangu sijamwambia chochote na ananipiga simu tunaongea vizuri tu.
Nimfanye nini huyu rafiki? Nimwambie ukweli au nimtege nimkamate au nimwache nianze kumuepuka kimya kimya.
Kama amekusoma na kujua weakness yako atakusumbua sana, njia ya kwanza hapa ni kumtega ajitumbukize kisha muanike atahama kijiji
 
Ila wanaume wa kibongo unaendaje kwa mwanamke aloolewa mmewe hayupo unatafuta nin?
Na nyie wanaume kwanin mnazoesha marafiki zenu nyumbani kwa wake zenu onaneni bar inatosha kila mtu arudi kwake,mtu keshoa unaenda kwake kufanya nin
Uswahili wa kijinga sana huu. Eti unaenda hata kama chakula kimeisha unapikiwa.

Haya ni mambo ya kizamani, simu zipo na kuna sehemu nyingi za kukutana kama wanaume na kula msosi na vinywaji huku mkizungumza.

Mazoea mabaya haya
 
Hizo meseji anazomtumia mkeo. Foward kwake kwa kutumia namba yako halafu kaa kimya. Usimwambie chochote
Mpaka kufika hapa, mkeo anaomba msaada kutoka kwako

Back
Top Bottom