Black Sniper
JF-Expert Member
- Dec 10, 2013
- 32,406
- 55,148
Nimekuelewa sana mkuu. Najua kwa Afrika ni nadra sana mwanamke atoke nyumbani, kama yuko peke yake na asitupiwe maneno na wanaume. Ila hili ni tofauti. Wewe una rafiki na mnaheshiana sana na pengine hata kwenye shida mnasaidiana. Umepata safari una unaporudi unaambiwa alikuja nyumbani kwako anamhangaisha mke wako. Na siyo mara moja. Haki lazima uwe mtu wa ajabu sana kama utamkaripia mkeo ni kwa nini amekuambia! Tena atadhani ni wewe ulimtuma na pengine mna tabia ya kuchangia wake zenu. Nachosisitiza mimi ni hili la mtu kama rafiki au jirani kujua kabisa huyu ni mke wa mtu na ankujua halafu akawa anamsumbua mke wako wakiti anajua hali halisi.
Hili nalo ni kweli
Binadamu ni wa ajabu sana
Nami nimekuelewa na wa hivyo ni mbaya zaidi
Na sio kumkaripia Mkuu bali ni kueleweshana tu
Hata kama unamtegemea kwa mambo mengi Basi urafiki ufe kwani yeye sio mgawa riziki