Rafiki yangu alimrusha mtu mwaka 2017/2018: Anamtafuta amwombe msamaha na kumlipa akikubali

Mungu ni mlipaji pekee mzuri
 
Dah aisee..... Sema hata hivyo sio mbaya sana mwengine angezima na simu kabisa asee
 
Dah aisee..... Sema hata hivyo sio mbaya sana mwengine angezima na simu kabisa asee
Sure.

Toka siku hiyo jamaa anaamini yule mtu alikuwa ni tajiri mwenye uwezo wa kifedha maana 50K ya Mkapa ilikuwa siyo hela ya mchezo pia kipindi kile simu walimiliki wenye ahueni kimaisha pangu pakavu wamiliki simu hawakuwa wengi kama leo.
 
Niliwahi kutuma hela kimakosa, hela dogo sana kimuonekano (16,000) lkn kubwa sana kimajukumu, ikapokelewa na hawa ndg zenu wa Kaskazini, nilimnasihi sana na kumweleza mazingira ya hela yenyewe huwezi amini akaniambia " unayo nyengine uniongezee aisee"
Nilichoka nikalazimika kutafuta nyengine.
 
2020 nilikosea kumtumia mtu 206,000. Ilikuwa ni malipo ya hela ya Chakula cha vibarua kwenye site yangu.

Nilikuwa busy kidogo, ilipofika tu jamaa niliyemtumia hela akapiga. Nikamuandikia ujumbe kuwa tayari nimeshatuma. Niliamini ni fundi anauliza. Jamaa, akaniandikia pokea mara moja.

Akapiga lakini niligundua si sauti ya fundi. Akaniambia kuna fedha nimemtumia ila anaomba asirudishe. Nilipanick kidogo, jamaa akanielezea story ya magumu anayopitia. Anaomba sana nimuachie kiasi kile cha hela. Akaniambia kama sitaridhia atarudisha kiasi hicho punde baada ya kukata simu.

Lakini kwa magumu yale, niliridhia kumuachia kiasi hicho cha pesa. Ukweli ni kuwa niliokoa maisha ya mwanae. Na maombi yake yalijibiwa kupitia mimi. Nilifanya alternative nyingine kuwesesha kule site.

Jioni nilipata dili zuri mno. Nikajua tu ni Mungu ananilipa kwa Sadaka yangu ya asubuhi.
 
Huwa najiuliza, hivi wanaojisifu kudhulumu hela za mikopo ya hizi apps kama tala na branch wanatoa wapi ujasiri? Hivi hela uchukue bure na mwenye hela aridhike tu? Tafakari
Mbaya sana
 
Kuna niliyemtumia kupitia NBC mobile banking ,nilipompigia alisema pesa kaziweka kwenye kilimo.Alinushia kidogo Kisha akaacha.Kwa madai yake alikuwa anaishi Singida.
 
Mimi kuna mtu nilimuahidi kumchangia Harusi halafu sikumchangia... kiukweli roho iliniuma Sana kila ninapo kutana nae...
Kama ningejua ningemchangia tu...
Imeniumiza kuliko hela ambayo ningemchangia
Unaweza Kumchangia hata sasa, Mfuate na umwambie kipindi umepanga Kumchangia mambo hayakwenda kama yalivyopangiliwa, ila sasa walau yanaenda hivyo Kamata hiki kiasi kama zawadi yangu kwenu, mtanunua kitu chochote ama kufanyia chochote kunikumbuka.
 
Sadaka yako ilikua ya kweli.

Sadaka zinapaswa ziwe zinatolewa kwa watu wenye uhitaji kama huyo, na sio sehwmu zisizo sahihi ambapo kuwafikia walengwa huwa ni tatizo.
 
Kuna day moja nipo safarini natoka chuga nazama naenda singida kidogo naona Ela imeingia kwa ndamba ya mtu binafsi baada ya apo sms ya matumizi ikafata sindo nikamsanua kuwa umerong number alihisi kuchanganyikiwa sema nilimwambia asipige simu kuomba irudishwe nitamrudishia mwenyewe tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…