Rafiki yangu anawaza kuvunja ndoa, lakini nyumba yake alijenga kwenye kiwanja cha wakwe, afanye nini?

... hata kama ni uwanja wako, masuala ya kuvunja ndoa lazima yalambe mali!
INABIDI USAMEHE MALI USONGE MBELE!
 
Niko katika age of 40+ ni mwalimu,siwezi gombana na mke wangu na kudai kugawana, namuacha naenda anzisha maisha yangu.

Sikuzaliwa na nguo, Leo hii Nina nguo,sikuzaliwa nikiwa na nyumba Leo hii Nina nyumba,sikuwa na chombo cha usafiri,Leo hii Nina vyombo.

Kikubwa uzima, harafu mtu lazima atambue Kila Mmoja wetu hapa duniani yuko kwa kazi maalumu,Huenda huyo jamaa yako kazi yake kuu duniani ilikuwa kuwanufaisha ukweni,akae kwa kutulia

Mapenzi nyege yakifika mwisho kinachofuata hapo ni majuto. Mwanamume Gani unajenga kwa kiwanja cha wakwe zako?
 
Hakuwa na akili hata chembe kujenga ukweni
 
Umesema ushahidi wote unasoma nyumba siyo yake. Sasa hiyo nyumba ni yake kivipi?
 
Bora dharau za kujenga ukwen,kuliko nijenge halafu dume lingine likae kwwnye nyumba yangu
Dahh, we ukishaondoka unaanza tena kufuatilia nani atakaa pale au utaenda kuanzisha tatizo lako jingine kwenye mji mwingine huko?
 
Alipojenga nyumba eneo la ukweni hakua na Akili kabisa.

Na Sasa analilia nyumba wakati tayari anawatoto wawili, mwambie bado hana akili tena
 
Alirogwa huyo kukubali kujenga kiwanja cha ukweni maana kwa hali ya kawaida mtu huwezi...dawa zimeisha nguvu anaanza jielewa, wawai kumuongezea dozi waliomroga.
 
Hii mbona kama chai yaani mtu ujenge kwenye kiwanja majina yanasoma ya wakwe
Kama kweli huyo jamaa akaanza upya tu kwenye kiwanja cha wakwe wapya
 
Mwambiye achukuwe bag lake la nguo aondoke,, Hana chake hapo.
Asije qkapewa kesi ya kufanya vurugu nyumbani kwa watu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…