Habari wa ndugu.
Ni kijana wenu mpya. Sikuwa member lakini nilikuwa nahudhuria humu now imeshindikana hivyo imenipasa kujiunga rasmi. Mnipokee.
Ndugu, mimi ni muhitimu wa diploma ya uhasibu TIA 2022.
Nna rafiki yangu ambaye babake ni shekhe wa mkoa fulani TZ bara. Juzi amenipigia simu kuwa ameajirwa kwenye moja ya taasisi nyeti. Hakufanya interview wala kuomba nafasi.
Ameitwa utumishi kufata barua tu ya ajira.
Nnachojiuliza, inawezekanaje hadi viongozi wa dini kuwa na nguvu ya kupenyeza watu?? Nafikiria uwingi wa makanisa Kama kila mchungaji mkubwa akipeleka mtoto wake. Ajira zinazidi kuwa finyu kwa sie kajamba nani