Rula ya Mafisadi
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 404
- 852
==
Leo Ezekiah Wenje mjumbe wa Kamati Kuu CC anakuja kutuambia eti Mh LISSU hajachangia chochote kile akiwa mbunge kwenye bunge la 11.
Tujiuluze, bunge la kumi na Moja (11) lilikuwa mwaka 2015-2020 Lissu alikuwa Bungeni?
Nani asiyejua kipindi Mh LISSU alipigwa risasi na baadae Ubunge wake kutenguliwa atawezaje kuchangia wakati hakuwa na Mishahara?
Huyu Wenje hayuko sawa kiakili kabisaa sijui kwanini na sijui kawezaje kuwa mkiti wa Kanda na mjumbe wa Kamati Kuu huyu mtu,
Mtu huyu ni hatari na hana huruma kabisaa baya zaidi ni Muongo na mfitini sana.
Pia soma Wenje: Lissu mpaka anamaliza bunge la 11 hajachangia hata tsh.100 CHADEMA
Wenje anaona aitumie kisiasa hii itampa unafuu? Aiseee Wenje hana hata aibu kudai mgonjwa achangie,tunathamini uhai wake na tunashukuru Mungu kuturejeshea uhai wa Mh LISSU kumbe Wenje anataka mgonjwa kama LISSU kipindi kile eti achangie michango aibu sana
Wenje hana huruma hafai kuwa kiongozi kabisaa,sijui yupo kamati kuu kwa uwezo gani alionao.