Rafiki yangu kampa kadi ya benki mke wake na akipata mshahara wote anampa mkewe. Yuko sawa kweli?

Ni mapenzi tuu na ndoa za namna hiyo hudumu sana
 
Huenda jamaa anahisi yeye si mtunzaji na mtumiaji mzuri wa fedha so kaamua kutumia hiyo kama njia ya kulinda kipato chake kwa kuwa anaamini wife ni bora kimahesabu na kimikakati kwa manufaa ya familia.
Hilo hutokea kwa manufaa kama hukuokota mbugila ukaoa.Kuna wanawake wako smart ni hatari mno yaani mme anajivunia kuoa mtu bora kama yeye.
Hata mimi nikiwa nina malengo makubwa mbele savings naifanya kwa bibie maana yupo vizuri katika utunzaji wa fedha japo sijawahi kumkabidhi full control ya kipato changu na sidhani kama nitafanya hivyo kwa kuwa hata mimi nipo vizuri katika matumizi ya fedha
Jamaa yupo sahihi kutegemea family situation yake maana familia zina mengi mno
 
Hayo ndio maisha waliyojiamulia mkuu wala hakuna shida.

Pengine mwanamke ameona udhaifu wa mwanaume katika matumizi na utunzaji wa hela na mwanaume amekubali kudhibitiwa kwa ajili ya ustawi na maslahi mapana ya familia. Kumbuka mkishaoana wote mnakuwa mwili mmoja na lenu wote linakuwa moja.
 
Theories hizo!
 
Kama kweli mwanamke yuko vizuri kwahilo bado busara isingemtuma kufanya hivi wanawake ambao wako vizuri hawakai mbele yamwanaume kwa jambo lolote labda kama me anachangamoto nyingi zausimamizi wafamilia
 
Sasa akakununia kisa nini jamani 🀣 🀣 🀣

Wapo, ila wanahitaji utulivu haswaaaa na wewe uwe mwanamke mwenye akili na wa kuaminika.
Alikuwa ananiletea hasira zake zote miye, si unajua binadamu wakipata pa kumalizia hasira

Hizo akili tu ninazo, huyo future husband ajiandae kuwa bilionea πŸ˜„πŸ˜„
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…