Rafiki yangu kampa kadi ya benki mke wake na akipata mshahara wote anampa mkewe. Yuko sawa kweli?

Rafiki yangu kampa kadi ya benki mke wake na akipata mshahara wote anampa mkewe. Yuko sawa kweli?

Mnapenda mapoyoyo kama hao.
Ene wei, ni vizuri maana pesa ya familia inakua salama. Sisi wanaume hua tuna mambo mengi. Shida huja mnapokua na upendeleo, mnafanya ya upande wa kwenu tu. Likitokea tatizo kwetu mnachuna kwamba hamna pesa ila likitokea kwenu mnalishughulika chap.
Mimi sipo hivyo, kabisa kwanza familia ya ukweni ndiyo ntaipa kipaumbele
 
Wakuu,

Hivi hii imekaaje?

Nina rafiki yangu ambaye tulisoma nae pamoja na kwa sasa anafanya kazi kwenye moja ya taasisi kubwa sana hapa nchini.

Jamaa take home ni around ya 1.5 Million kwa mwezi na ajira yake ni ya uhakika maana hiyo taasisi anayofanyia kazi ina muingiliano na masuala ya Serikali.

Lakini juzi wakati tunaongea kuna kitu aliniambia kikanishtua wakuu.

Huyu jamaa kumbe kadi ya benki ambayo anaingiziwa mshahara kamuachia mwanamke wake. Yaani akipata hela, mwanamke ndo huwa anapanga itumike vipi, wapi n.k

Mshahara ukiingia mwanamke anapewa taarifa na yeye ndo atapanga kila kitu cha humo ndani na hata mwamba akitaka chochote basi ni lazima ruhusa na matumizi itoke kwa mkewe.

Kilichonifanya nilete hii mada hapa ni kwamba, kuna rafiki yetu mwingine yeye anaumwa na nilimpigia jamaa kumpa update na kumuuliza kuhusu mchango maana tulikubaliana wote tutoe kabla huyo rafiki yetu hajatoka hospitali.

Jamaa ndo akaniambia ngoja aongee na mkewe maana ndo ana kadi yake ya benki. Kumuuliza ndo akaniambia huo ndo utaratibu wao. Akipata hela yote anapeleka kwa mkewe. Mkewe ndo atapanga iende au isiende


Sasa naomba kuwauliza humu hasa mlioko huko ndoani? Huyu jamaa yuko sawa kweli? Au ndio utaratibu ulivyo kwenye hizo ndoa wakuu? Kadi ya benki?
Wakati nahamia, Dodoma, nilipanga, chumba, Kodi, anapokea mke wa, jamaa, mumewe ni Fundi,gereji, sasa, siku moja, huyo dada akanitambulisha kwa mumewe, ili, ajue kuna mpangaji mpya,nikawa navigation nae story, jamaaa ananiambia, mkewe ndio kama Mkurungenzi, mtendaji wa familia, anapanga uwekezaji, wote,watoto wasome wapi, biashara gani, ianzishwe, viwanja wanunue wapi, zijengwe flem wapi, za, kupangisha, kwa hiyo jamaa, akitoka kwenye mihangsiko yake gereji, akija na, pesa, anampa mke wake, wife anatoa kidogo, anampa jamaa, ya, supu na bia, jamaa anapiga bia sio mchezo(mangis wananielewa),
Hiyo familia, wapo mbali Sana, walitoka Moshi, bila kitu,wakaanza, na biashara ya, kuu za, duka,Leo, hii wapo mbali, Sana,
Jamaa ana tafuta pesa, mama apange mipango, LA msingi maendeleo,
Kama mke, akili, zipo, hakuna, shida, lakini, kama, mke ni wale wa kujivunia ukubwa wa makalio, na, sio brain power, hapo, ni shida.
 
Ndiyo, kuanzia August tunaweka akiba tujenge vibanda vya kujisitiri na usafiri tusiweke foleni mwendokasi
 
Mume na mke wakikubaliana na kufunga ndoa,wanakuwa mwili mmoja hawafanyi mambo yao kwa siri.Mume akimpa mshara mkewe kwa matumizi yao ni nafuu kuliko mume kubaki nazo mfukoni ebu jaribu wewe.Angalizo.kwa kuwa mume ndiyo kichwa yapendeza panapotokea sitafahamu basi maamuzi ya mume yanapasa kuwa maamuzi ya wote wawili na mke ayaheshimu
Hii ninafanya kazi mwanamke akiwa na uwezo mkubwa kiakili na utendaji. Staff mwenzangu yeye kadi ya benki ya mshahara kampa mke wake alafu yeye anaishi kwa posho za safari, vikao, na posho za overtime. Kwa kweli wamepiga hatua kubwa sana kiuchumi.
 
Back
Top Bottom