Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Dah umetangaza vita na huyo mkongo walivyo wachawi sasa, huyo mtoto anateseka sana
 
Ningekuwa mimi ningepiga ngumi kali sana huyo jamaa tena ningempasua ili aende polisi alafu tukifika polisi ndo kila kitu kitajulikana hapo ningeelezea sababu ya mimi kufanya hivyo ni kwa maslahi ya mtoto ningeomba watuhumiwa tuwe wawili mm na mke wa jamaa kama vp aitwe mtoto atoe ushahidi kama vp haujachelewa subiri siku huyo mama wa kambo anamtesa mwambie wife wako arekodi video kwa siri alafu we nenda kakate ufunue huyo mama lazima akimbilie polisi huko unakwenda kumwaga ushahidi hata kama utakaa ndani usijari haizidi masaa 24 mkeo aende polisi awape ela ya blashi na awaonyeshe ushahidi utakuwa umemsaidia sana huyo dogo vinginevyo dogo ataendelea kutubu kwa huyo mama wa kambo.
 
Wewe nae mjinga, kuongea na mshikaji wako kuhusu hali ya mtoto wake huwezi, ila kumnunulia nguo mtoto wake na kupeleka umeweza, la kwanza ni rahisi kuliko la pili.
 
Pole sana pia pole kwa huyo mtoto.
Hili la mtoto linanikumbusha maumivu sijui kwanini mpaka saivi namkumbuka yule mtoto.
Kwa kifupi yule mtoto alikufa kutokana na mateso ya mama yake mzazi.
Huyo mama alikuja kuolewa na mzee mmoja mtaani kwetu akiwa na mtoto huyo. Ila alipo zaa mtoto mwingine na mume wake mpya akaanza kumyima chakula na kumpiga sana mtoto kwa kukadilia mtoto alikuwa na miaka kama minne au mitano.
Wana Mtaa walivyo jua hivyo wakaanza kumpa chakula ila mama yake akaanza kuwatukana na kuanza kumfungia mtoto ndani, baada ya mtoto kutokuonekana kwa muda wakamuuliza akasema wamempeleka kwa baba yake lakini haikuwa hivyo.
Mwisho woto wa lika lake wakamuona na kutoa taarifa ndipo wana Mtaa wakaenda kumtoa mtoto kwa nguvu kupitia mwenyekiti wa mtaa ila walikuwa wemechelewa mtoto alikuwa tayari kadhoofika.
mtoto baada ya miezi kazaa akaaga Dunia, sijui kilicho endelea kisheria maana nilikuwa nina kama miaka kumi wakati ule ila baba wa kambo na mama aliendelea kudunda mtaani.
 
Popote alipo, Gwajima ni mfano tu wa authority areport tu kwa child protection services huyo mtoto ana haki ya kuwa mtoto na kukua kwa wazazi wake km watoto wengine na kama Hawako responsible wapo wanaoweza
Ni kweli mkuu, sheria za hapa kama mzazi ameshindwa kumlea mtoto wake basi amkabidhi kwa mamlaka wamsaidie kulea. Lakini sasa sina uhakika kama baba mtoto anajua kinachoendelea kwa mtoto wake.

Nangoja jamaa akitukutanisha nae nimwambie kila kitu kinachoendelea kwa mwanae. Halaf akishupaza shingo, ndo niangalie njia nyingine za kisheria za ku deal nae.
 
Dah aisee inaumiza sana kuona binadam mwenzako, tena malaika asiejua chochote akiteswa na mtu ambae ana dhamana ya kumlea na kumtunza. Huu unyama sijui utaisha lini. Halaf upo kila mahali.
 
Shukran sana mkuu kwa ushauri wako 🙏
 
Aisee, pole sana. Ni kawaida kuwa hata wema una gharama zake (maumivu)
Zingatia ushauri wa mtu wa 3 (rafiki yenu), naamini Mungu atamfungua macho na atajua ukweli. Sasa hapo aibu kwake; sijui atakuombaje msamaha!
Nahisi atajiona mjinga, na mpumbavu sana kwa kunitusi mtu ambae napigania uhai wa mtoto wake. Ilitakiwa aje aniulize kiume ili kuujua ukweli kabla ya kukimbilia kuropoka mbele ya watu.
 
Dah aisee inaumiza sana kuona binadam mwenzako, tena malaika asiejua chochote akiteswa na mtu ambae ana dhamana ya kumlea na kumtunza. Huu unyama sijui utaisha lini. Halaf upo kila mahali.
Ingekuwa saivi ninge-report kwenye vyombo husika na mtoto ningemsaidia kulingana na mahitaji yake.
Ila mpaka saivi sijajua yule mama alikumbwa na nini mpaka amfanyie mtoto wake wa kuzaa unyama ule.
Mungu awarehemu wote maana wametangulia mbele za haki.
 
Nahisi atajiona mjinga, na mpumbavu sana kwa kunitusi mtu ambae napigania uhai wa mtoto wake. Ilitakiwa aje aniulize kiume ili kuujua ukweli kabla ya kukimbilia kuropoka mbele ya watu.
Hawezi kujiona mjinga ,maana hajui na kashapigwa rimbwata,haelewi chochote.Dawa aburuzwe ustawi wa jamii tu
 
Ni kweli hapo ndo nilipokosea, ila nilihisi kama ningemwambia labda jamaa asingenielewa na pengine angemuuliza mkewe na kusababisha matatizo zaidi kwa mtoto. So nikaona mimi kama mzazi ambae nina watoto kama huyu nifanye kile ninachoona kinafaa kimya kimya.

Kwa bahati mbaya ndo hivyo nimejiletea janga kubwa kwa jamaa.
 
Mama wa kambo wengi wana roho ya chuma. Why umtese mtoto wenzio. Next time unamchoma ustawi wa jamii wa deal naye perpendicularly.
Mtu anashindwa kufikiria kwamba anapotesa watoto wa mwenzake, na yeye kesho akifa pia wa kwake watateswa. Sijui wanakuaga na akili na moyo gani hawa viumbe.
 
Fanya hivyo mkuu...ripoti haraka ustawi wa jamii huyo mama sio
Huyu ni mshenzi na muuaji. Halaf huenda ni lichawi na lishirikina, cause haiwezekani mpaka leo mshikaji hajashtuka tu kama mwanae anateswa. Inafikirisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…