Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Nimecheka sana 🤣🤣🤣
 
Basi kama na yeye ametangulia huenda wamekutana na sasa ana kesi ya kuijibu roho ya huyo mtoto kwa kuisababisha itoke kabla ya wakati wake.

Mungu mjuzi wa yote atamhukumu kila mtu sawa na uzito wa kosa lake. Ila huyo mama alizingua, labda alihisi akimchukua mwanae ndo atapendwa zaidi na mumewe.
 
Mtoto akikukana utafanyaje? Kuna matukio mtoto katestify uongo kwa maelekezo ya wazazi mhusika anajikuta kwenye aibu. Anadanganywa na vi icecream na vipipi unashangaa mtoto anakuwa upande wa wazazi wake unaingia aibu.

Mshkaji alitakiwa awasiliane na baba mtoto ambae ni rafiki yake na amueleze kuwa kuna mzigo atampa shemeji.

Sasa ananunua zawadi, anampelekea mke wa rafiki yake huku rafiki yake hana habari ilihali anajua kabisa mkewe ana roho mbaya.

Na wanawake walivyosmart akijua bado mnamfatilia na akataka kuharibu zaidi hii miezi kadhaa mtoto anaweza pendwa kinafiki, siku mnamuita huyo rafiki yenu anawaona wote mnamtamani mkewe.
 
Uchawi upo lkn sikuona njia nyingine ya kumsaidia huyu mtoto zaidi ya hii niliyofanya mkuu au wewe unaonaje?
Hukujipanga vizuri, huyo ungempangia mkakati na kumdhibiti asingekuwa na hiyo jeuri kabisa ya kuleta uchonganishi, hapo ndo utaona kwanini inasisitizwa akili katika kuishi na mwanamke, sasa umejiongezea mlima wa kutatua huo mgogoro
 


CHAI
 
Wewe nae jau acha kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu pmbav.
 
Dk Gwajima hausiki hapa jamaa anaishi South
 
Kuna wanawake hata shetani hua anakuja kujifunza roho mbaya kwao .Kuna jirani mtoto wake aliteswa aliumizwa na mama wa kambo ambaye nae ana watoto wawili amekuja nao kwa mmewe huyu jirani.Yaan hawa watoto wake ndo wamekua kama nyumba yao wao ni kula bata tu.Sisi majirani hatukutaka kuharibu ndoa ya jirani .. wanawake zetu walifanya kikao wakaja na jawabu la kumtafuta bibi wa mtoto upande wa mama yake na wakafanikiwa mtoto kachukuliwa na bibi yake sasa jirani analea dam si yake watoto wa kufikia wakati damu yake iko kwa bibi mzaa mama.Yule mwanamke hata salam yake hua naitikia tu ila nikimuona hua naona kama nimekutana na Msaidizi wa shetani.Mungu awalaani wote mnaotesa watoto na laana hii iwakumbe mpate magonjwa ya kuwatesa hadi mjinyee shenzi nyie ...
 
Hukutakiwa kuingilia mambo ya watu, ungeenda tu kutoa taarifa ustawi wa jamii, then wewe unaendelea na mambo yako.
 
Mtu anashindwa kufikiria kwamba anapotesa watoto wa mwenzake, na yeye kesho akifa pia wa kwake watateswa. Sijui wanakuaga na akili na moyo gani hawa viumbe.
Huwa wanawaza ya leo sio kesho ndo maana wana roho za kikatili. Kiukweli mtu anayemtesa mtoto wa kambo huwa simuelewi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…