Rafiki yangu kanipa kesi, kisa nimemsaidia mtoto wake mwenyewe

Mtafute rafiki yake mwingine amfikishie ujumbe wa mtoto wake kuteswa kabla ya kikao chenu. Ikifanyika hivi na huku amekubali kuwepo kikaoni, itakuwa rahisi kwako kumfikishia ujumbe kwa mapana yake. Lakini mkimshitukiza kikaoni, kuna uwezekano akaanzisha fujo nyingine, ambayo haitakuwa na afya kwenye nia yako ya maridhiano.

Kila la kheli..!!
 

Kuna theory inasema abuser hawezi kuacha abuse hadi anakufa, na abuser hawezi kulenga mtoto tu hata huyo bwana I believe huko ndani anapitia mazito, wanaume wa kiafrika hatunaga ujasiri wa kujitokeza kusema na kujifanya tupo stoic sana na hasa akiwa mke mzuri wa sura au ana kipato zaidi. Lazima kila rangi humo ndani anakutana nayo na bahati mbaya sana watoto ndio huwa wanakuwa victims kutoka kwa parties zote. So naamini hatapata ushirikiano wowote kutoka kwa home boy na pia huyo mama anamjua sana bwana wake ndio maana alifanya alichofanya ili jamaa aondoke kwenye maisha yao.
 
Ni kweli, lakini abuser wengine huwa hivyo kwa kukosa information fulani. Na kwa msingi huu ndo nimeona kabla ya kikao, homeboy apewe taarifa na rafiki mwingine. Ili kama kuna kukataa, basi atakataa hata kuwepo kikaoni, na hapo ndipo jamaa msamalia mwema atatakiwa kuachana na jambo hili. Au la kama anaweza, jamaa yetu awatonye watu wa dawati.
 
Huko unapoishi hakuna social welfare departments?

Nenda karipoti anonymously
 
D
Dudumizi mwambie akupe weye umlee dogo akikataa ndio mpatie kichambo chake kama anateswa sana.
 
Meseji nimeipata hapo kuwa wanawake asilimia kubwa ya wanawake wana uwezo mdogo wa kuchanganua mambo yanayokuja mbeleni. Sasa hapo kaenda kujinunulia nguo ili aseme umemuhonga wakati ipo siku itafamika kwamba alidanganya na hapo muwe wake ataoneka mke wake ni mfitinishaji wa kiwango cha tp mazembe.
 
Hii inajenga picha mbaya na kuvunja moyo watu wenye nia ya kuwasaidia watoto wanaopata shida mbali mbali.

Unaweza kupita njiani na gari ukamkuta mtoto anatoka shule huku kanyeshewa na mvua ukashindwa kumsaidia kwa kuhofia kujiletea matatizo mwenyewe. Wazazi haswa wanaume wanatakiwa wasiwe na mioyo ya kukimbilia kuhukumu mtu aliemsaidia mwanae bila ushahidi wa kueleweka.
 
Tuliopitia maisha ya mama wa kambo tunakuelewa...Wanaume sijui tunakwamaga wapi sijui ni madawa au mapenzi ya kupitiliza
Nahisi ni mapenzi tu. Jamaa akikunwa kunwa gololi zake, anacheka cheka tu na kusahau kufuatilia jinsi mtoto wake anavyoishi na mama yake wa kambo.
 
Hukujipanga vizuri, huyo ungempangia mkakati na kumdhibiti asingekuwa na hiyo jeuri kabisa ya kuleta uchonganishi, hapo ndo utaona kwanini inasisitizwa akili katika kuishi na mwanamke, sasa umejiongezea mlima wa kutatua huo mgogoro
Kumdhibiti namna gani mkuu?
 
Wewe nae jau acha kujipa umuhimu kwenye maisha ya watu pmbav.
Huyu ni binadam kama ulivyo wewe au mimi. Kumsaidia binadam mwenzako tena mtoto mdogo kabisa asiekuwa na hatia sio kosa.

Kosa ni kumsaidia mtu mzima ambae anao uwezo wa kujisaidia yeye mwenyewe. Leo unaweza kumsaidia huyu, kesho na wewe wa kwako akasaidiwa pindi utapokuwa umekufa au haupo karibu yake.
 
Mwanamke atakayemtesa/kuwatesa wanangu namuacha mara moja
Na haya ndio maamuzi ambayo mwanaume thabiti anatakiwa kuyachukua. So kuendelea kumbembeleza mwanamk katili mwisho wa siku anakuja kuuwa na wewe mwenyewe.
 
Sijui huwa na mioyo ya namna gani hawa viumbe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…