Rafiki zangu wengi wenye umri wa miaka 35 mpaka 37 ndoa zao zimevunjika nyingine zipo ICU

Rafiki zangu wengi wenye umri wa miaka 35 mpaka 37 ndoa zao zimevunjika nyingine zipo ICU

Azoge Ze Blind Baga

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2019
Posts
442
Reaction score
1,655
Kama mada inavyojieleza
Hii hali imenishangaza sana. Nina marafiki wengi wa kike na kiume wenye umri unaocheza miaka 35 mpaka 37 wengi wao ndoa zao zimevunjika na nyingine zipo ICU

Wengi wa marafiki hawa walioa baada ya kumaliza vyuo tena kwa mbwembwe nyingi leo hii ndo zimesambaratika na wengi wamegeuka maadui dhidi ya watalaka wao.

Wanawake nao wamegeuka masingle mother na wadangaji

Katika uchunguzi wangu mdogo nimegundua hawa marafiki zangu walikurupuka kuoa mara tu walipopata kazi na kuingiza hela za mishahara wakakimbilia kuoa tena harusi za gharama

Leo wengi wanajuta kuoa hasa wale waliooa wanawake zao wa chuo. Maana baadhi ya marafiki hawana kazi maalumu ya kuingiza kipato ila wake zao waliajiriwa mapema so ndoa zao zimeingia ICU maana mke anavimba ndani ya nyumba.

Kwa kweli ndoa ni gumu.
 

Attachments

  • 1727271195898.jpg
    1727271195898.jpg
    156.2 KB · Views: 10
Taasisi ya ndoa haishemiwi kama zamani ,ni kazi ya mme kupenda na wajibu wa mke kutii tofauti na hapo ndoa itapitia misukosuko mingi
 
Kwani kwenye ndoa kuna nini hasa wakuu? Rafiki zangu wengi ambao wameoa naona wananitisha sana daily na ukiwaangalia hawana furaha, kila siku ni kulalamika, matusi muda mwingine yaani ilimradi tu kusiwe na utulivu.

Mmoja nilimuonea huruma sana, jamaa huwa anasafiri safiri sana, akiwa safarini alipigiwa simu kwamba shemeji kafumwa mahali mwamba akarudi wakayamaliza akavunga (alikuwa mstari wa mbele kumtetea mkewe).

Juzi tena hapa mkewe kamchapa tukio la maana mpaka wazazi wa jamaa wamemkataa kabisa mwanamke kwamba anawadhalilisha ukizingatia ni koo yenye jina na heshima.

Naamini ndoa ndio msingi bora wa kila kitu ila kuna namna taasisi hii inakufa vibaya sana. Nadhani kuna haja ya kurudi kwenye asili hata kama itaonekana ni Ujima.
 
kataa Ndoa Sasa Wanakuja
Wanachua Points 3 Muhimu Home And AWay
Wanakaa Kileleni Kwenye Msimamo Wa Ligi Oops Kuna Baridi Kali Sana
 
Taasisi ya ndoa inapitia changamoto kubwa. Mtaani kwetu naona asilimia 90 ya ndoa ziko ICU. Si kwa waliooa wasomi au mama wa nyumbani. Kuna mmoja kila mtu anaishi kivyake, mwingine mume kakimbia, nyingine wanalala vyumba tofauti, nyingine mke kakimbia kaenda kupanga. Shida tupu. Mimi mwenyewe yalinishinda. Kuna mwingine mke kapata kichaa sababu ya depression ya kwenye ndoa. List ni ndefu
 
Tatizo wanaume wengi waliooa wanageuka kua wanawake huku wakizani wanawake hawana akili.. wanawake wana akili na hawa ni wakina delila na hawafanyi kitu kwa mwanaume mpaka hajithibitishie anaweza kukushinda na kukutawala kabisa shauri yetu wanaume mfumo ni dume na waambieni hata Mungu aliumba mfumo dume kabla ya kumpa Adamu mwanaume mwezetu yule eva/ hawa

Nb: kama huna akili usioe na wala usidhubutu kuishi na mwanamke ndani
 
Tatizo ni mihemko na kukurupukia ndoa kabla hawajajihoji kwa nini wanaoa/wanaolewa, ndoa ni nini, nani ana sifa za ndoa. sio lazima watu wote waoe au waolewe, kuna ambao ndoa sio fungu lao.
 
Back
Top Bottom