Umenichekesha sana😁😁aisee hapo utakuwa umewapatia mno
Mimi pia nakumbuka niliwahi kukaa kwa mama angu mkubwa ikatokea akauza hapo nyumba anayokaa kama millioni 30 na upuuzi na mimi ndiyo nilikuwa nimemaliza shule sasa natakiwa kwenda chuo, mzee hana hela wakati huo, nikajua mamkubwa angejiongeza anilipie holaa kaenda kujenga huko morogoro ndani ndani shughuli ya maana unayoweza kufanya huko ni kilimo tu.
Aisee niliambulia tu elf30 ila nikajisemea zangu tu ipo siku tutakutana sisi ni pipo.
Mungu si Athumani nikapata kibarua changu kule watoto wake wakaanza kurudi mjini maisha ya kijijini hawayawezi. Mara naanza kusumbuliwa na watoto wake mara nikopeshe elf30 mara nikopeshe elf50. Mimi nawaambia tu sina mpaka leo hii kila mtu na maisha yake walitumia pesa zimeisha wapo tu wanataabika na mji na mimi sitaki mazoea aisee, ubaya ubwela.