Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Raia Mwema: Paul Makonda kushtakiwa Mahakamani kwa matumizi mabaya ya madaraka

Wanasheria uchwara bana... kazi kwelikweli!. Issue ya Paul Makonda na Sabaya ni vitu viwili tofauti!. Huo unaosemwa ni uvamizi wa kuvamia Clouds Media, haukuwa uvamizi chochote wala lolote ndio maana Nape alitumbuliwa.

Ili jinai itendeke na kufikishwa mahakamani jinai hiyo ni lazima iripotiwe na uchunguzi ufanyike. Hilo tukio la uvamizi wa Clouds, jee kuna yoyote aliyelalamika popote?.

Naendelea kusisitiza Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .


Na hili gazeti lipuuzwe!.

P
Naona ushakata tamaa ya teuzi baada ya sukuma gang leader kutwaliwa katika maisha haya. Umeishiwa pumzi, hupandishi tena nyuzi kama mwanzo na uzipandishazo unaonekana kituko. Pole sana mayala
 
Unapomuua mwanadamu mwenzio aliapo kwa uchungu usitegemee utakuwa salama Mungu yupo anaona
 
Naona amegundua hasikiki akaamua kujipa promo mpuuzi sana. Nimeuliza kwa majamaa zangu ofisi ya DPP wanasema hakuna hiyo kitu kwao labda io kwingine may be PCCB hukoambao nap walishatoa statement kwamba hawajamdaka na hawana ishu nae .
Wachaaa? Tena??
 
Bashite acha uzuzu kimbilia Rwanda kwa Kagame huyo no mjomba wako hawezi kukutupa..ni kaka ya mwendazake.
ou paup...
Hawa jamaa wanataka kukupa miaka si chini ya 7 hadi 15 ukizubaa..una tuhuma nyingi sana...kalagabaho.
Chaaaa! Fuso jaman acha kumjaza mwenzio uoga kesi ya jinai haikimbiwi acha ahangaike amalize salama mambo ya ishe kama lulu tu alivyofanya
 
Kama ambavyo kichwa cha habari kinaeleza, ni mwendo wa kutafuta haki zilizocheleweshwa kwa muda mrefu. Sasa Bwanamdogo kumfuata jamaa yake Sabaya.

View attachment 2010908
====

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda anatarajiwa kufikishwa mahakamani muda wowote kujibu tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

Taarifa hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Raia Mwema toleo la leo (Novemba 15,2021), ambapo inaelezwa kwamba, maombi ya kumfungulia kesi Paul Makonda, yamepelekwa na Mwanasheria wa kujitegemea ambaye jina lake halijawekwa wazi.

Raia Mwema limeeleza kwamba katika Mwanasheria huyo ameomba kibali cha Mahakama kumshitaki Makonda kutokana na makosa anayodaiwa kuyatenda wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, kinyume cha Sheria namba 96.

Mwanasheria huyo ameomba Makonda afikishwe kortini pia kujibu tuhuma za kuingilia maudhui ya matangazo ya kituo cha televisheni cha Clouds, alipoenda katika ofisi zao, usiku wa Machi 17,2017.

Paul Makonda alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam tangu mwaka 2016 alipoteuliwa na aliyekuwa Rais wakati huo, Hayati Dkt John Pombe Magufuli. Mwaka 2020 Paul Makonda aliondolewa katika nafasi hiyo ikiwa ni baada ya kutangaza nia ya kugombea Ubunge katika jimbo la Kigamboni.

Iwapo Paul Makonda atafikishwa Mahakamani, atakuwa kiongozi wa pili kukabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka katika kipindi cha hivi karibuni, kwani aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya alishafikishwa Mahakamani kwa makosa hayo na kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Hii ni strategy ya ccm kuwaondoa watanzania kwenye mijadala ya msingi ya katiba mpya, ukosefu wa umeme kwa zaidi ya miezi miwili, na hali ya kukosekana maji katika jiji la Dar es Salaam.

Watanzania akili zao ni fupi sana
 
Ila ikitokea kweli Bashite akapigwa miaka kadhaa kutokana na hii ishu basi kuanzia hapo ntaamini kwamba uchawi haupo Tena!
 
Tujikumbushe operation alizoendesha huyo bwana mdogo zilizokuwa zimezungukwa na giza nene
  1. Operation madawa ya kulevya
  2. Operation ya watoto waliotelekezwa
 
Mwananchi la February 11 2017

Mbunge ataja mali mpya za Paul Makonda​


Dodoma. Sakata la mali zinazodaiwa za Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda limeendelea kulitikisa bunge baada ya Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini (Chadema) kuongeza nyingine.

Akichangia taarifa za Kamati za Bunge za Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Selasini alisema Makonda amenunua jengo (apartment), lenye thamani ya Sh600 milioni.

“Makonda amenunua apartment pale Viva Towers kwa Sh600 milioni. Makonda amempa mke wake gari aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya Dola 250,000 za Marekani (Sh550 milioni) kama zawadi ya ‘Birthday’,” alisema Selasini.

Suala la utajiri wa Makonda, liliibuliwa bungeni kwa mara ya kwanza Februari 6 na Mbunge wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Msukuma akitaka mteule huyo wa Rais achunguzwe kwa kujilimbikizia mali.

Kiini cha mbunge huyo kumshukia Makonda ilitokana na hatua yake ya kutangaza majina ya watu aliodai wanajihusisha na biashara ya madawa ya kulevya, huku akidai utajiri wake una shaka.

Msukuma Februari 7, mwaka huu aliomba mwongozo kwa Spika, akitaka Bunge litoe mwongozo kuhusu utajiri huo wa Makonda ndani ya muda mfupi.
Msukuma alisema kuwa katika kipindi cha mwaka mmoja tu wa wadhifa wake kama mkuu wa mkoa, Makonda amejilimbikizia mali likiwamo gari aina ya Lexus, lenye thamani ya Sh400 milioni.

Mbali na mali hizo Msukuma alisema Makonda anamiliki magari mengine ya kifahari aina ya V8, anajenga maghorofa jijini Mwanza na amekarabati ofisi yake kwa Sh400 milioni bila kutumia utaratibu wa sheria ya manunuzi.

Mbali na hilo, Selasini alisema utaratibu unaotumiwa na Makonda kushughulikia tatizo la dawa za kulevya, umetoa mwanya kwa wafanyabiashara wakubwa wa dawa hizo kukimbilia nje ya nchi.

“Kama unawatangaza watu kwa utaratibu huu. Ni mfanyabiashara gani wa dawa za kulevya mjinga amebaki katika hii. Makonda amesaidia kuwakimbiza labda anashirikiana nao,” alisema.

Wakati huo huo Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), ameliomba Bunge kutoa mwongozo kwa kile alichodai ni hatua ya katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah kupingana na maazimio ya Bunge.
 
Uyo Mdau mbuz.i kweli.. yaani Makonda asishtakiye hata kama anahatia na makosa yameonekana waziwazi kisa mfuasi wa magu ndio aachiwe!!! ?

Na akamfungulie mashtaka uyo Kikwete kama anaona anamakosa, aache kulialia
 
Back
Top Bottom