Mimi nawashangaa wanaotoa povu hapa, hivi nani anaijua status ya korona hapa nchini? Mmejifanya vichwa ngumu, hampimi, hamjaweka system yoyote inayoeleweka; wagonjwa wa korona nasikia sasa hivi wakipatikana wanaambiwa waende waugulie nyumbani, isije julikana kuna cases hospitali, wanaofariki wanazikwa tu kama kawaida na akifia hospitali unaambiwa beba maiti yako ukazike! Hata ningekuwa mimi ningewawekea pini tu! India na Urusi wanapima, na hao watakokuja watakuwa wamepimwa, hata Marekani na Brazil wanapima, waje tu! Nyinyi hamjielewi, period!
Korona ipo na watu bado wanakufa, hilo halina mjadala; kwamba kesi zimepungua na hivyo ku-achieve herd immunity nalo halina mjadala; lakini, hali halisi iko wapi? Nani anajua???