Raila Odinga anaamini Rais Magufuli hashauriwi vizuri

Akijibu kauli za Kiongozi wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga, Mbunge wa Tanzania kutoka chama tawala cha CCM Job Lusinde Kibabaje amesema mfumo ambao Magufuli anautumia katika kukabiliana na Covid -19 ni mfumo umewasaidia sana Watanzania tofauti na Afrika Kusini, Uganda Kenya na Rwanda. ‘’Pengine wanashindwa tu kumuelewa’’, alisema katika mahojiano na BBC.

‘’Rais mfumo alioutumia kwa kukataa kuwaweka watu Lockdown, sisi Watanzania tunafahamiana, kuna watu wengi wanakula chakula cha leo wakitoka...leo ukiwafungia ndani wanaweza kupata matatizo makubwa’’ amesema .

‘’Mi natakaka tu kumuambia mwanasiasa mkongwe Raila kuwa Magufuli anawafahamu Watanzania zaidi na rais ana uchungu zaidi na Watanzania kuhusu uchungu wowote’’alisema Mbunge Kibabaja.

Raila amesema viongozi wa kanda wamekua wakitaka kushauriana na rais John Pombe Magufuli, bila mafanikio.

Chanzo:BBC
Your browser is not able to display this video.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bora hata angeshauriwa vibaya. Hashauriki kabisa hata na hata wanaomshauri kina Kigwangala wamechoka wako twitter wanapost mapenzi na kupiga picha wanavutana na mbwa wakati nchi iko kwenye tetemeko la Ugonjwa hatari. Hashauriki hata kwa dawa.
 
Wanamtafuta kwa maswala binafsi au ya kiofisi? Kama ni masuala ya kiofisi, rais ni taasisi hivyo wawasiliane na ofisi. Tatizo hao wamezichukulia nchi zao kama mali binafsi.
Only God knows if you are not out of your crazy mind!!!
 
Sas aitakuwaje? Urafiki umekwisha?
Magu hataki kw amakusudi kupokea simu
 
Ta Tangu lini jiwe linashaurika!!
 
Nyie mshabikieni tu,mambo ya kiharibika msije geuka tena.
 
Magufuli anajiamimi yeyeye ndiye super human kuwa hakosei. Lakini maamuzi yake yote aliyokwisha fanya maishani ni FAILURES tu. Mfano kidogo huu hapa;
1. Kushika Meli ya wavuvi wa Thailand kulikosababisha tukashindwa kesi
2.Ununuzi wa kivuko cha MV Bagamoyo ambacho kilipaswa kiwe kinasafiri kwa Dak 45 kutoka DSM- Bagamoyo instead kikawa kinatumia masaa 2
3. Uuzaji wa nyumba za Serikali hadi kumuuzia mdogo wake Musa Magufuli na kimada wake
4. Kuwakamata wauzaji wa sukari mwaka 2016 kwa kisingizio cha ukwepaji kodi. Mpaka sasa Sukari imetoka kwenye Tsh 1,800 kwa kilo mwaka 2015 hadi Tsh 3,800 na haipatikani
5. Kuvuruga biashara ya korosho mwaka 2016 kwa kisingizio cha kwamba makampuni yanawanyonya wakulima. Korosho bado haijatengamaa

Haya ni machache tu lakini Magufuli hashauriki na mtu wala hana muda wa kushauriwa. Kimsingi kichwa chake hakina nafasi ya kutunza ushauri. Yeye akiamua anakuwa ndiyo ameamua kwa hiyo akipotea anapotea kweli
 

Mimi niseme tu kuwa Raila yeye kaongea na ameweza kusikika na kuzungumzia kama mimi ninavyoandika hapa na NIMRI wamegundua dawa na pia sukari hamna madukani nayo tutakwenda kuifuata Madagascar na pia lengo la kuifuata si kuwaletea Watanzania,ni kwa ajili ya utafiti na pia si kila kifo ni corona kuna magonjwa mengi ambayo ndiyo hivyo kwani sasa watu hawazikwi usiku tena na tunajifukiza.


*****
 
Rais Magufuri amekwepa kupokes simu za rais wa Afrika Kusini Ceril Ramaphosa,Yoweli Kaguta Museveni,na ya Swaiba Wake mkuu Raila Odinga,ambaye wiki iliyopita akihojiwa na BBC alisema madai ya Magufuri kuwa mashine za kupimia Corona ni mbovu ,sio kweli anaamini rais Magufuri hashauriwi vizuri ,kimbembe toka siku hiyo kila akimpigia simu haipokelewi ,vilevile Ramaphosa na Museveni kulikoni?
 
Kwani ulisikia kuwa mlima ndo umemfuata Mtume au mtume ndo aliufuata mlima?? Mwenye shida naye aje sio kumpigia sim
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…