Crimea
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 25,874
- 36,030
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Raila amesema viongozi wa kanda wamekua wakitaka kushauriana na rais John Pombe Magufuli, bila mafanikio.
Video: SABC
Virusi vya corona: Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga amesema Rais Magufuli ''anashauriwa vibaya'' - BBC News Swahili
Leo best wako umeamua kumpa makavu?
Raila amesema viongozi wa kanda wamekua wakitaka kushauriana na rais John Pombe Magufuli, bila mafanikio.
Video: SABC
Virusi vya corona: Kiongozi wa upinzani wa Kenya Raila Odinga amesema Rais Magufuli ''anashauriwa vibaya'' - BBC News Swahili
"Raila amesema viongozi wa kanda wamekua wakitaka kushauriana na rais John Pombe Magufuli, bila mafanikio."
Hii statement ni fikirishi. Ni kuwa rais ni mkaidi? Rais siyo msikivu? Rais hana cha kujifunza kutoka kwa wengine? Rais hashauriki? Nk nk.
Nani wanaomshauri rais kuwa na msimamo huu? Kina Mbatia ni mmoja wa watu hao?
Nimemsikia ameongea kikubwa Tena kwa masikitiko makubwa kuwa rafiki Yake nchi imemshinda.
Aisee umenenaKumbe huyu naye anatumika na mabeberu
Jr[emoji769]
Alishinda nini na hiyo Acacia imepotea kwenye uso wa dunia IPI, Lumumba?Magufuli hajawahi kushindwa
Hata wakati wa suala la Acacia alibezwa sana,lakini alishikilia uzi hatemaye Acacia ikapotea kwenye uso wa dunia
Raila kwani ndie aliemshauri Kenyatta awapige bakora raia mpaka wengine kuuwawa?
Halafu kuna watu wanmfananisha na Legends wa nchi hii.Kama Kuna siku Jumuia za EAC na SADC zitakuja kusambaratishwa na kuvunjika ni kwa ujeuri,kibri na ubabe wa JPM. Huyu mtu hana kabisa hata chembe moja ya Kidiplomasia. Mwaka wa 5 lakini bado hajapata hata zile ABC za diplomasia ya mahusiano ya Kimataifa. JPM kwa hakika
ni aibu tupu.
Wanaomshauri wanajua hulka yake ya kupenda kunyenyekewa kwahiyo wanatambaa na biti la Kumsifia tu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Katika mahojiano aliyofanya na Shirika la Utangazaji la Afrika ya Kusini, SABC, , Mjumbe Maalum wa Kenya katika Umoja wa Afrika (AU) Raila Odinga ameeleza kuwa anafikiri Rais Magufuli anashauriwa vibaya katika hatua anazochukua/asizochukua kukabiliana na Ugonjwa wa CORONA, ameshangaa kuwa Marais wenzake na hata yeye mwenyewe wamejaribu kuwasiliana naye mara kadhaa bila mafanikio.
Raila Amesema ni vizuri Rais Magufuli akaona umuhimu wa kushirikiana na kushauriana na viongozi wenzake wa Kikanda katika kupambana na Ugonjwa wa CORONA, kuliko kujiweka pembeni peke yake kama ilivyo sasa..
Maoni yangu:
Nadhani Sasa Uvumilivu wa majirani Umefika kikomo...Baada ya Museveni, Ramaphosa, na Sasa Raila, nadhani atakayefuata ni Paul Kagame - na Huyu tumjuavyo, lugha yake itapukutisha hadi majani ya mimea ya kujifukiza katika Kisiwa cha Rubondo, Wacha tuone