Rais ambaye hajawahi kugombea, ilitokea Marekani, itatokea tena huku

Rais ambaye hajawahi kugombea, ilitokea Marekani, itatokea tena huku

Tetesi zipo kitambo mbona, ila currently nadhani kambi itakuwa sambamba na ujenzi wa bandari ya Bagamoyo.

Inasemekana kuwa kwenye bandari hapo hapo ndo itakuwapo base yao (Navy) hivyo vitu kama ku-repair meli zao za kivita nk vitafanyika hapo.

Pia tetesi zinasema kuna gesi wanailenga (probably maeneo hayo kuna gesi au ile ya kusini).

Kiufupi kuna mambo mengi kwenye hiyo bandari ambayo watu hawayasemi.
Kumbe ndiyo maana kuna kauli mbilimbili..!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hv wadau kama anachosema mtoa mada ni kweli hv ni nan katika nchi hii ni engineer wa kupanga hii mipango wakati Rais ndo top. Kuanzia mkurugenzi wa usalama wa taifa na vyombo vingine vya usalama wote wanaripoti kwake. Au kuna mtu mwngine nje ya mfumo Mwenye uwezo wa kuwaendesha hawa watendaj wengine bila rais kufaham?
Nina mashaka sana na hata kujiuzulu kwa mwalimu nyerere.....itakuwa alilazimishwa....kuna invisible institute kwenye hii nchi inafanya hizi sarakasi
 
Ni taasisi ambayo huwa ipo ndani ya serikali kwa Siri yaani hiyo taasisi inakuwa haijulikani kuwa ipo


Hata raisi wanchi anaweza asijue kuwa ipo !? Au akawa anajua lakini Taasisi hiyo inakuwa na mfumo imara ambao hauruhusu taasisi hiyo kuingiliwa na kiongozi yeyote yule wa Nchi kwaajili ya kulinda maslahi yake .Taasisi hiyo kazi yake Dhumuni la uwepo wake ni kulilinda taifa husika at any cost
Hahaha angalia drama ya jumong....kuna gereza babaake jumong ...haemuso alifungwa bila mfalme kujua hilo gereza na waziri mkuu pia hakujua
 
Wakuu,

Mwaka 1973 Spiro Agnew alijiuzulu nafasi ya makamu wa Rais wa Marekani kufuatia skendo ya rushwa na matumizi mabaya ya ofisi ikiwemo kukwepa kodi alikofanya wakati ni governor wa Maryland. Rais Richard Nixon akamteua Gerald Ford kuchukua nafasi yake.

August ya mwaka 1974, Rais Richard Nixon alijiuzulu kufuatia skendo ya Watergate. Hapo ikabidi makamu wa Rais, bwana Gerald Ford aapishwe kuwa Rais wa Marekani.

Unaweza kuona jinsi Ford alivyokuwa na bahati. Hakuwahi kugombea umakamu wa Rais au Urais wenyewe lakini alishika vyeo vyote hivyo kwa nyakati tofauti zinazofuatana.

Nimeandika hii habari kuonyesha yanayokuja soon.

Endelea kusubiri!
Uzi huu naweka kumbu kumbu. Kuna jambo nyuma ya pazia watu wanaona sana.
 
Back
Top Bottom