Binafsi, naipongeza kazi aliyoifanya RC ya kuanzisha vita dhidi ya madawa ya kulevya.
Lakini, kama kweli amevamia kituo cha habari na kuwalazimisha maaskari kupiga wafanyakazi basi hilo ni kosa na hata akitumbuliwa ni sawa.
Japo, tukumbushane style, hii ya leo inaweza ikawa ya kuonesha kuwa RC hana shida ya vyeti isipokuwa ametumbuliwa kwa kosa la kuvamia kituo cha habari na siyo kwa kosa la vyeti kama ni kweli hana.
Kwa hiyo mbinu ya kuvamia kituo inaweza ikawa imetumiwa kama Waziri wa Mambo ya ndani alvyotumbuliwa kwa mfumo wa " kitwangalization" ya viroba na kuhutubia bungeni.
Ila katika yote, RC amefanya kazi nzuri nyingi mfano ya drug dealers.
Na hapo sijaelewa ubuyu wa kwa Gwajima kama ni mchachu au umetiwa sukari?
Naagiza popcorns , mtoto wa kishua naendelea kumega hadi mwisho wa hii filamu.
Japo, naona starling anaweza akazimia kwenye maua.