Rais ana Mafua? - Nimemsikia anakohoakohoa wakati anahutubia Wafanyakazi

Rais ana Mafua? - Nimemsikia anakohoakohoa wakati anahutubia Wafanyakazi

Sasa wewe ni Muhindi?
Wamatumbi kwa kujifaraghua hamjambo.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwamba kwa vile wale ni wahindi? Kwamba mmatumbi ni superior race kwenye Corona? Kwa utafiti ipi?

Acheni hadithi za saluni kwenye mambo nyeti.

Kwani kule Marekani, wamarekani weusi walikuwa na nafuu yoyote na ugonjwa huu dhidi ya wale wa rangi zingine?

Huu ugonjwa unasema na mapafu ambayo kwa bahati mbaya ni kuwa mapafu yote yana rangi moja kwa wote wamatumbi, wahindi, wachina, nk.

Si suala la wamatumbi dhidi ya yeyote jombi. Dhana hiyo ni dhana mfu.

Usisahau wale machampioni wa nyungu, sasa hivi ni kama unavyowaona hapa

2721819_Jafo.png


na wengine tayari wamesha rest in peace.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Ilianza hivi hivi kwa hayati Magufuli katika hotuba yake ya mwisho alionekana akikohoa sana na hatimaye hakuonekana tena baadae.Usalama wa rais unafanya kazi gani?
Kazi ya kulinda dhidi ya risasi na CDM
 
Leo Rais wakati anahutubia wafanyakazi, ameonekana ana mafua, Sauti yake imesikika kama imeathiriwa na Mafua huku akikohoa hapa na pale!

Ninamshauri Rais aongeze juhudi za Kujilinda ili asipate Covid-19 na kulilinda Taifa dhidi ya ugonjwa huo.

Kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa Huu ugonjwa unakuja kwa mawimbi, Ni dhahiri kuwa ni busara achukue jitihada za kutosha kulilinda Taifa dhidi ya Mawimbi mbalimbali ya Covid-19

Haitoshi tu kutoa kauli za hapa na pale dhidi ya Covid-19 bali serikali yake iwe kiongozi wa kuonyesha mfano kwenye mapambano dhidi ya Covid-19. Viongozi wa serikali wavae barakoa kwenye public!

Sasa hivi India inapigika kwelikweli na Covid-19, nao walikuwa wanaamini wameshashinda hii vita, lakini hii kitu ilipogeuka imekuwa balaa kubwa!

Kwa hiyo rais asikohoe?
 
Kwa kile kipimo kipya cha covid19 toka china, ukiwa kama daktari wa rais unamshaurije umchukue kipimo kuona kama ana maambukizi ya covid 19.
 
Itakuwa ni hali ya hewa!
AC ya dream liner na land cruiser,plus ratiba ngumu ya kiti chake,na huenda hafanyi mazoezi,kumbuka Jana alikuwa na wanakijiji kibao pale kikwete convention center,Sasa inakuwaje.
 
Maisha yangu mpaka umri huu mafua kila mwaka hata mara 2 na vifua leo imekuwa kama ugonjwa wa ajabu mafua, corona hii imeleta msiba kweli ndio maana siku hizi sioni mtu kuumwa mafua wa kukohoa barabarani sasa sijui siri ni nini?
 
Kwa hiyo "daktari wa Rais" umeshajua kuwa rais wetu ana Covid? Sawa mheshimiwa daktari!


Acha kutisha watu. Leo kuna video imerekodiwa India, watu wanaendelea na activities zao kama kawaida. Punguza kumeza sumu za media bila kutafiti. Hiyo panic ipo kwenye media na wasaidizi wao kwenye kusambaza kama wewe.



Acheni kuwatisha watu. Kama Korona inatisha kiwango hicho acheni watu waone na siyo kutunga vitu ambavyo havipo kuchochea hofu!
Mawaka wa shetani na mabeberu wapo kila kona, wengine wanaonekana wengine hawaonekani
 
Tumeshakua kama wapuuzi fulani! Kwani kukohoa kumezuiliwa lini? Kwa hiyo kila anayekohoa ana virus vya Corona? Tuache hizo!
 
Kwa usafi anaoufanya kwenye hii nyumba ya vumbi ana haki kupata mafua, ila atapona. Mungu hawezi kutupiga.
 
Leo Rais wakati anahutubia wafanyakazi, ameonekana ana mafua, Sauti yake imesikika kama imeathiriwa na Mafua huku akikohoa hapa na pale!

Ninamshauri Rais aongeze juhudi za Kujilinda ili asipate Covid-19 na kulilinda Taifa dhidi ya ugonjwa huo.

Kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa Huu ugonjwa unakuja kwa mawimbi, Ni dhahiri kuwa ni busara achukue jitihada za kutosha kulilinda Taifa dhidi ya Mawimbi mbalimbali ya Covid-19

Haitoshi tu kutoa kauli za hapa na pale dhidi ya Covid-19 bali serikali yake iwe kiongozi wa kuonyesha mfano kwenye mapambano dhidi ya Covid-19. Viongozi wa serikali wavae barakoa kwenye public!

Sasa hivi India inapigika kwelikweli na Covid-19, nao walikuwa wanaamini wameshashinda hii vita, lakini hii kitu ilipogeuka imekuwa balaa kubwa!
Hiyo ni hali ya kawaida kwa kipindi hiki kila mwaka! Manabii wa uovu msianze zenu hapa.
 
Kwamba kwa vile wale ni wahindi? Kwamba mmatumbi ni superior race kwenye Corona? Kwa utafiti ipi?

Acheni hadithi za saluni kwenye mambo nyeti.

Kwani kule Marekani, wamarekani weusi walikuwa na nafuu yoyote na ugonjwa huu dhidi ya wale wa rangi zingine?

Huu ugonjwa unasema na mapafu ambayo kwa bahati mbaya ni kuwa mapafu yote yana rangi moja kwa wote wamatumbi, wahindi, wachina, nk.

Si suala la wamatumbi dhidi ya yeyote jombi. Dhana hiyo ni dhana mfu.

Usisahau wale machampioni wa nyungu, sasa hivi ni kama unavyowaona hapa

View attachment 1770054

na wengine tayari wamesha rest in peace.

Au nasema uongo ndugu zangu?
Tangu Corona iingie Tz, kwenye familia yako wameshakufa wangapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom