Rais Dkt. Hussein Mwinyi kumuwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye mkutano wa Wakuu wa nchi SADC

Rais Dkt. Hussein Mwinyi kumuwakilisha Rais Samia Suluhu kwenye mkutano wa Wakuu wa nchi SADC

Naona Mama kaamua Mwinyi aende ili Yeye amalizie Kupanga Safu yake mpya ya Wakuu wa Mikoa na wa Wilaya ambayo ( za chini chini japo hajizathibitishwa ) zinasema Siku si nyingi ataiweka hadharani.
 
Kwani Rais wa Zanzibar ana cheo/wadhifa gani katika serikali ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania kama isemavyo katiba...???
Na kama katiba inamtambua katika serikali ya Muungano basi ni haki yake kuagizwa kwenda huko
Ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri la JMT.
 
Sawa, lakini Mwinyi ni mkuu wa serikali ya Zanzibar ambayo si mwanachama wa SADCC. Kama alitaka kumtuma mzanzibari wapo wengi tu kwenye serikali ya muungano.

Kamba kaachiwa ndefu sana naona akienda kujinyonga mwenyewe.
Rais wa Zanzibar ni mjumbe wa baraza la mawaziri la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 
Ni sahihi Rais Mwinyi kwenda, anajua mambo mengi ya nchi. Nadhani wataongelea swala la ulinzi na mwinyi amekuwa waziri wa ulinzi kwa miaka mingi atajua cha kufanya.
 
Mwinyi hana kazi za kufanya huko Znz? au ndio wameanza kufanya kazi kishkaji hawa waswahili?

Kwani Dr. Mpango ana kazi gani? naona hii nchi sasa inaanza kujiendea tu kama gari bovu mtaroni.
Mlikuwa mnawakilishwa na Prof wa Jalalani na ilikuwa sawa tu. Mwinyi kuwakilisha ni sawa.
 
Angeenda pia mngelalamika.
Acha uboya we jinga
Huyu tunajua anajua kuongea english
Yule alikuwa hajui kuongea english
Sasa huyukilichomfanya asiende ni nini na english anajua
 
Huyu alikuwa waziri wa ulinzi wa JMT kumbuka na wanalokwenda kulizungumza ni usalama wa ukanda huu, mi sioni tatizo
I think wewe umejibu sahihi 💯. Ila nimefurahi anafuata utaalamu.
 
Ameenda kama nani? Waziri asiekuwa na Wizara Maalumu ama? Tanzania ndio ipo SADC na sio Zanzibar, kwaio alitakiwa aende mtu aliepo kwenye Serikali ya Muungano na kama ni yeye basi ni Waziri asiekuwa na Wizara Maalumu. Ivi vyeo vingine bana. Watu wamevuruga stucture ya Muungano
 
Kwani Dr. Mpango ana kazi gani? naona hii nchi sasa inaanza kujiendea tu kama gari bovu mtaroni.
Mpango anajikaza tu kwani ile corona iliyompiga huwa inaathiri ubongo pia!! Uroho wa cheo tu lakini Afya yake ni wanting!
 
Ni mjumbe wa baraza la mawaziri wa JMT

Back
Top Bottom