Rais Dkt. Mwinyi anafaa kuwa Rais wa Tanzania
1.Wakati Tanzania bara wanafukuza wamachinga hovyo na kuwarudisha nyuma kimaendeleo ,upande wa Zanzibar Rais Mwinyi amewapa vitambulisho na kuwapa uhuru wa kupiga kazi masaa 24.

2. Wakati Tanzania bara Makamba akipandisha bei ya kuunga umeme mpaka zaidi ya laki 9, upande wa Zanzibar Rais Mwinyi ameshusha gharama ya kuunga umeme mpaka laki 2 tu kwa mtu ambaye hana nguzo.

My take.
1. Smartphone zimeondolewa VAT ili zishuke bei na watanzania wengi wanunue na serikali ikate tozo, kwa nini wasishushe bei ya kuunga umeme ili wakate tozo pia?

2. Serikali inatoa elimu bure kwa nini umeme ishindwe?

3. Serikali inatoa mikopo vyuo vikuu?
4. Serikali inakusanya kodi ya majengo kupitia Luku.
Hiyo serikali imewezaje yote hayo alafu ishindwe kushusha bei ya kuunga umeme?

akili ya mtanzania ndio hiyo. kamuona mwinyi anafaa kuwa rais wa tanzania naakuuliza kwani hakuna watu wengine wakuongoza tanzania ila unataka sura hiyohiyo tu ya watoto wa viongozi tuna watu million 70 tanzania sio lazima huyo tu. akili yako kama timu ya simba yaani haijamuona mchezaji africa nzima anafaa ila chama eti mpaka chama ndio timu itapata ushindi
 
Machinga warudi Vijijini wakalime Samia yuko sahihi.
up.gif
 
Kuna maelfu ya watu wameungwa umeme kwa elfu 27 hata mimi nimeunganishiwa umeme kwa elfu 27.

Kumbuka Tanesco wanakusanya rundo la kodi pale unaponunua umeme ya kifupi ni kwamba kuunganishia umeme ilitakiwa iwe bure au bei chini sana kama mtu anapofungua akaunti ya bank au anaponunua laini ya simu
Kwa mara ya kwanza nakuunga mkono hapa Jf juu ya hili, pamoja na kua hua unaachaga ubongo wako kweny shelf za Lumumba.
 
Mapato ya bara si ndio yanapelekwa uko Mwanakwerekwe kuleta maendeleo kwahyo zenji lazima kuwe Kama Dubai.
Mapato gani ya bara au hayo ya mikopo?
Kwa taarifa yako ilpovunjika EAC , pesa Za Zanzibar ziliiibiwa Na Tanganyika Na kuingizwa Benki kuu. Mbona hamjawapa wenyewe mpaka Leo ?
 
Watanzania watu wa ajabu sana, unataka uungiwe umeme kwa elfu 27..gari ya Tanesco iwekwe mafuta, wafanyakazi walipwe na wewe utoe elfu 27..
Hivi ile remote feeder ya units yenyewe tu pesa ngapi?
Na hapo hutaki kusikia deni la taifa linaongezeka..

Machinga anachukua bidhaa anaenda kuuzia mbele ya fremu ya mtu, halipii fremu, halipi VAT, halipi leseni, halipi usafi, halipi Zimamoto, hana bili ya umeme wala maji..na wewe unaona sawa tu hiyo hali iendelee..
Ifike mahali tuwe serious tunataka nini..

Zanzibar wameshusha umeme mpaka laki mbili kwa wale wasio na nguzo na bado unafanya comparison na elfu 27??
Hivi Zanzibar ina watu wangapi?? Kimsingi yote ilipaswa kuwa na umeme toka enzi za Sultan
Gharama za kuunga umeme tanesco wabebe, halafu waziingize kwenye malipo bili ya umeme ya mteja. Shida hata
umeme wenyewe hakuna wataunga giza
 
Hii tabia ya ku import wazanzibar kuongoza Tanganyika ina hitaji review. Mbona sie hatupewi nafasi visiwani? Wizara zisizo za Muungano pia wasipewe Wazanzibar.
 
1.Wakati Tanzania bara wanafukuza wamachinga hovyo na kuwarudisha nyuma kimaendeleo ,upande wa Zanzibar Rais Mwinyi amewapa vitambulisho na kuwapa uhuru wa kupiga kazi masaa 24.

2. Wakati Tanzania bara Makamba akipandisha bei ya kuunga umeme mpaka zaidi ya laki 9, upande wa Zanzibar Rais Mwinyi ameshusha gharama ya kuunga umeme mpaka laki 2 tu kwa mtu ambaye hana nguzo.

My take.
1. Smartphone zimeondolewa VAT ili zishuke bei na watanzania wengi wanunue na serikali ikate tozo, kwa nini wasishushe bei ya kuunga umeme ili wakate tozo pia?

2. Serikali inatoa elimu bure kwa nini umeme ishindwe?

3. Serikali inatoa mikopo vyuo vikuu?
4. Serikali inakusanya kodi ya majengo kupitia Luku.
Hiyo serikali imewezaje yote hayo alafu ishindwe kushusha bei ya kuunga umeme?
Mama kasha sema Raisi ni taasii siyo mtu
 
Hii tabia ya ku import wazanzibar kuongoza Tanganyika ina hitaji review. Mbona sie hatupewi nafasi visiwani? Wizara zisizo za Muungano pia wasipewe Wazanzibar.
Ni kwa kuwa mlituvamia wenyewe Zanzibar Sasa karma inawatesa
 
Back
Top Bottom