Rais hamuamini Makamu wake?

Rais hamuamini Makamu wake?

Ibara ya 47 ya Katiba inasema, kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.

Sasa nashangaa hata barua tu ya uteuzi hadi isainiwe na Rais mwenyewe tena nje ya nchi, kuna ulazima gani wa Rais kusaini nje ya nchi, kama kazi ndogo kama hiyo makamu haaminiwi ni kipi sasa kidogo atakachoaminiwa?

Wajuvi wa protokali ikoje hii.
Hebu tuaonyeshe hapa hiyo barua aliyosaini Rais Samia
 
Hao ni wazanzibari hao ni wa bara,

nisaidieni ule usemi wa mwalimu Nyerere
 
Na sikuwahi kuona Raisi akienda na makamu wake huko Dubai kwa wajomba zake anaotaka kuwapa Bandari zetu kwakisingizio cha uwekezaji.
Tutajie Rais yeyote ambaye huwa anaongozana na Makamu wake nje ya nchi
 
Ibara ya 47 ya Katiba inasema, kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.

Sasa nashangaa hata barua tu ya uteuzi hadi isainiwe na Rais mwenyewe tena nje ya nchi, kuna ulazima gani wa Rais kusaini nje ya nchi, kama kazi ndogo kama hiyo makamu haaminiwi ni kipi sasa kidogo atakachoaminiwa?

Wajuvi wa protokali ikoje hii.
Ibara ya 47 ya Katiba inasema, kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.!

Alishasema katiba ni kitabu tuu.... (Tafsiri pana sana hii, yaani si lazima kuiheshimu)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuki lalamika mnatuona wajinga.
Tanzania swala la makamu wa raisi ni kupoteza pesa tu.
Hakitoka raisi anakuja waziri mkuu akikosa waziri mkuu ni spika wa bunge.
Wakikosea wote mkuu wa majeshi au jaji mkuu basi labda kunatatizo
Ni kweli, hata mama alikuwa waziri mkuu kipindi cha magu
 
Rais siyo mtu tu, ni taasisi na ndiyo sababu akiwa nje ya nchi shughuli zake zinaendelea nchini mwake.
Haya ya kuandika anuani za nje ya nchi sidhani kama ni sawa.
Kama ikiwa sawa, hata Marais waliofurushwa nchini mwao (waliopinduliwa), wangeendelea kuteua wakiwa ughaibuni.
 
Mzandiki mkubwa wewe, hujawahi kuona au kusikia Makamu akimuwakilisha Rais mikutano ya nje, au ndo ile philosophy ya "ukitaka kumuua mbwa, mpatie jina baya".

Hasidi hana sababu.
Mkuu, kama nimekukera, naomba unisamehe. Halikuwa lengo langu kukuudhi!
 
Ibara ya 47 ya Katiba inasema, kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.

Sasa nashangaa hata barua tu ya uteuzi hadi isainiwe na Rais mwenyewe tena nje ya nchi, kuna ulazima gani wa Rais kusaini nje ya nchi, kama kazi ndogo kama hiyo makamu haaminiwi ni kipi sasa kidogo atakachoaminiwa?

Wajuvi wa protokali ikoje hii.
Makaimu atakaimu mengine lakini sio uteuzi.

Kama rais mgonjwa au hajiwezi kwa namna yoyote kwa muda mrefu hiyo inaweza kutokea lkn sio hii ya kukaimu uteuzi akiwa safarini.
 
Mzandiki mkubwa wewe, hujawahi kuona au kusikia Makamu akimuwakilisha Rais mikutano ya nje, au ndo ile philosophy ya "ukitaka kumuua mbwa, mpatie jina baya".

Hasidi hana sababu.
Awamu hii mtapasuka kwa kutema nyongo, kazi bado mbichi tulia ndg yangu
 
Makamu is very composed. Hataki kujiingiza kwenye ujinga ujinga unaoendelea. Bora akaangalie mito na miti inavyokatwa kwa mshangao, kuliko kujiingiza kwenye udalali haramu wa mali za watanzania
 
Tuwekee hapa hizo barua alizosaini akiwa nje
Weka hiyo barua aloyosaini !
Tuoneshe hiyo barua ya uteuzi uisemayo.
Onesha hiyo barua alosaini Rais upate milioni moja ya Kenya.
Kenge wewe
A896479C-1170-46FE-BD0B-FAAD01B39C8C.jpeg
 
Kuna kipindi aliyekuwa Makamu wa Rais Bilal kazi yake kuu ilikuwa kukata utepe wakashauri awe anatembea na mkasi mfukoni.
Hizo zilikuwa fitina za mkwere na inferiority complex yake dhidi ya Dr. Bilal aliyekuwa more enlightened kuliko yeye!
 
Ibara ya 47 ya Katiba inasema, kutakuwa na Makamu wa Rais ambaye atafanya kazi zote za Rais kama Rais hayuko kazini au yuko nje ya nchi.

Sasa nashangaa hata barua tu ya uteuzi hadi isainiwe na Rais mwenyewe tena nje ya nchi, kuna ulazima gani wa Rais kusaini nje ya nchi, kama kazi ndogo kama hiyo makamu haaminiwi ni kipi sasa kidogo atakachoaminiwa?

Wajuvi wa protokali ikoje hii.
Anamuamini....

Atafanya pale ambapo Rais hawezi kufanya.....Katiba haijatamka kuwa akiwa nje hawezi KUFANYA....

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Siku hizi kuna technology dinia imekua kijiji popote unaweza akasaini barua na kufanya mawasiliano sio kile kipindi cha 1977 wakati katiba inategenezwa, kazi ya makamu wa raisi siku hizi ni kutembelea ni kuzindua miradi ya serikali kwa niamba ya raisi uko mawolayani.
Hewalaaaa[emoji2956][emoji2956]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom