Rais hamuamini Makamu wake?

kwani ccm wanatambua uwepo wa hiyo Katiba? Subiria waandae mtaala wa twisheni!
 
Kwa uelewa wangu Rais akiwa nje ya nchi amekwenda kwa majukumu muhimu, ambayo yanahitaji aweke mawazo na akili yake yote kwenye alichokiendea.

Sioni kama kutakuwa na ufanisi kama ataendelea pia kushughulikia masuala ya nyumbani, ambayo yangeweza kusubiri arudi au yafanywe na mtu aliyekasimu mamlaka kwake.
 
Kwa weledi, uchaji wa Mungu na AKILI NYINGI za Dr. Mpango, ni kazi kubwa kufanya kazi na SAMIA
 
bas sawa kama ni kwa uelewa wako.

hayawezi kusubiri hadi arudi yuko ofisini kazini ndio maana mambo yanafanyika na kusonga mathalani teuzi na tenguzi kila mara awepo ndani au nje ya nchi.

Makamu ni Principal assistant tu hana difined responsibility zaidi ya ili muhimu ya kua Rais pale ambapo Rais alieko mamlakani hawezi tena kutekeleza majukumu yake kwasabb za kiafya, kufariki n.k

Tofauti na hapo Makamu wa Rais atafanya yale tu atakayo elekezwa na Rais afanye.
 
kwahiyo alivyosafiri hajamkaimisha mtu madaraka yakuongoza nchi?.anatembea namadaraka ya uonhozi wa nchi hadi nje ya nchi?.Kama ni hivyo mmmmmh
 
Sijawahi ona VP akisaini barua ya Uteuzi Toka Tzn iundwe
 
Onesha hiyo barua alosaini Rais upate milioni moja ya Kenya.
Kenge wewe
 
kwahiyo alivyosafiri hajamkaimisha mtu madaraka yakuongoza nchi?.anatembea namadaraka ya uonhozi wa nchi hadi nje ya nchi?.Kama ni hivyo mmmmmh
sio madaraka tu na mamlaka Kamili ya Urais ndio maana anapokelewa kwa heshima na salute ya utii na heshima ya Rais huko aliko.

Anakasimisha nadharia tu,
kwamba ndugu yangu Makamu wa rais, ninasafiri kidogo ninakwenda nitarudi kaeni salama.
Ikiwa kuna jambo lisilo la kawaida msisite kunishirikisha na kuniarifu niwaelekeze cha kufanya.

CDF, big up sana nakuaminia, IGP unafanya kazi nzuri,endelea nenda nao taratibu siasa ndivyo ilivyo. Lazima wakulalamikie na wakulaumu sana.

Waziri mkuu na naibu waziri mkuu, tafadhali mtamuarifu speaker natoka kidogo. Endeleeni kuchapa kazi mkayasimamie tuliyokubaliana..

Jaji mkuu, mwende mkafanye kazi ya kusimamia haki kwa weledi. Nikirudi kuna jambo nahitaj tuliweke sawa. Tutafanya kikao kidogo.

Haya jaman mimi nakwenda.........
Kisha mama anaingia kwenye gari kuelekea uwanja wa ndege kukwea pipa huyo ughaibuni.

Kwenye ofisi yake sasa ndani ya BOING, anamuita Zuhura Yunusi na katibu Mkuu kiongozi,

Hebu ñjooni na lile faili la mapendekezo ya teuzi za wakuu wa wilaya na Wakurugenzi. Kazi inaendelea.....

Hadi anafika Dubai tayari pdf la teuzi lipo tayari na Zuhura yunusi kaisha upload na kuliposti katika kila page ya ikulu........

vivyohivyo wakat wa kurud nyumbani kazi inaendelea......
 
Hivi Katibu Kiongozi kazi yake nini?
Kama hawezi kusaini hata barua ya mteuliwa hadi Rais asaini akiwa ughaibuni kuna haja ya kuwa pale?
 
Hivi Katibu Kiongozi kazi yake nini?
Kama hawezi kusaini hata barua ya mteuliwa hadi Rais asaini akiwa ughaibuni kuna haja ya kuwa pale?
ni afisa masuhuli Ikulu ya Rais,
majuku yake kwa kiasi yanashabihiana na makatibu wakuu wa wizara na kwingineko.
Ni mtendaji mkuu ikulu,
wanachopanga katibu mkuu, na maafisa wengine ikulu na Rais ndicho hutangazwa na Zuhura Yunusi
 
Ndgu, rejea kifungu hapo juu" kama ataagizwa"
Simply tu hawezi fanya kama ataagizwa. Aliagizwa ndipo kifungu kidogo"c"kitakuwa na nguvu.
 
Je, ni kweli kuwa Makamu hajawahi kumuwakilisha Rais mikutano ya nje ya nchi? Au uliamua kuruka sarakasi na taulo?
Sijasema kuwa huwa haendi! Hata wakati wa JPM, karibia Safari za nje zote alikuwa anawakilishwa na Makamu wake na si Rais wa Zenji!
 
Labda katiba ndiyo iepitwa na wakati, kwani kwa mazingira ya sasa, rais anafanya kazi au vikao akiwa popote pale.
Hicho kipengele inabidi kiseme Makamu wa rais atafanya kazi kwa maagizo au atakapotumwa na rais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…