Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar, naomba nikukosoe kwa staha; usingilie Mahakama

Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar, naomba nikukosoe kwa staha; usingilie Mahakama

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Udhalilishaji na Madawa ya kulevya ni tatizo kubwa katika nchi yetu, sote tunawajibu wa kuwafichua wadhalilishaji. Natoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini yoyote atakae kamatwa kwa kosa la madawa ya kulevya au udhalilishaji nasisitiza asipewe dhamana.

Ziara: Donge Chechewe

Huu ni ujumbe katika account ya twitter ya Mhe. Hussein Mwinyi, tumekatazwa kumkosoa Rais na baba yetu ila kwa hapa naomba nitimize wajibu wa Kikatiba.

1. Rais Hana mamlaka ya yakuingilia utendaji wa mahakama, dhamana ni haki ya kisheria si haki ya tamko la Rais

2. Zanzibar awazalishi dawa za kulevya, zinaingizwa na wakina nani? Je, wanaoingiza hawafahamiki?

3. Kwa kauli hii Tunaenda kujaza mateja magereza, je hii ndiyo suluhu ya dawa za kulevya? Kwanini asiongeze nguvu kwenye vyombo vya ulinzi wakabaini mtandao nakuufyeka?

Pls Mzee usiturejeshe kwa JPM, tumeona watu wasio na hatia walivyojazwa Magereza. Usiwajaze wasio na hatia Magereza kwa kisingizio cha madawa. JPM alianza kuwahita wahujumu uchumi akawatungia na sheria kumbe lengo nikuwazoba mdomo maasimiu na wabaya wake.

Don't do that pls, iache mahakama ipambane kivyake.
 
Sijui kuhusu, mateja ila nchi hizi zitasimaa kwa JPM mpaka lini? Wananchi wamekuwa kama mwanamke mwenye gubu aisee, ukigeuka huku JPM, kule JPM, tusonge mbele, wahenga walisema.

Kwenye rushwa, anayetoa na anayepokea, wote ni wakosaji; mateja hawana hatia ipi sasa?

Wengi wanajua vifaa vikiibwa kwenye gari yao aende wapi kuvinunua tena, walinzi wa raia na mali zao pekee ndo hawajui taarifa na hawajawahi kuzisikia, wako makambini huko, ni marufuku kwao kujichanganya na raia, hawajui chochote kile masikini, uhalifu umeshamiri, idara ya upelelezi pia iko busy kupeleleza magari yanayodaiwa faini huku wakisisitiza polisi jamii, bahati mbaya sana wana intelijensia ya kudaka taarifa za mikutano ya kisiasa nadhani

TBS, TMDA, n.k wanaenda kukamata bidhaa zisizo na ubora dukani kwa mangi, polisi bagamoyo wanakimbizana na bodaboda zinazobeba mafuta ya kupikia ya magendo tokea baharini, kule kwingine, mafuta yanaibwa kwenye bomba njiani kana kwamba hakuna flow meter za kujua yaliyoshushwa na yanayopaswa kupokelewa, na si mara ya kwanza n.k

Hapo bado unajiuliza madawa yanaingiaje?

Kama hawezu kushtakiwa akiwa madarakani au nje ya madaraka, mahakama ipi sasa anayoiingilia kiutendaji?
 
Udhalilishaji na Madawa ya kulevya ni tatizo kubwa katika nchi yetu, sote tunawajibu wa kuwafichua wadhalilishaji. Natoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini yoyote atakae kamatwa kwa kosa la madawa ya kulevya au udhalilishaji nasisitiza asipewe dhamana.
Uzuri wa Tanzania huu, sheria zipo chini ya rais.
 
Mh. Rais yuko sahihi. Hayo ni makosa yasiyo na dhamana. Amefanya kuwakumbusha watoa haki kufuata misahafu yao.
 
Sheria ya madawa kulevya inasemaje ? Naona Rais amesisitiza tu.
 
"Udhalilishaji na Madawa ya kulevya ni tatizo kubwa katika nchi yetu, sote tunawajibu wa kuwafichua wadhalilishaji. Natoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini yoyote atakae kamatwa kwa kosa la madawa ya kulevya au udhalilishaji nasisitiza asipewe dhamana. " -Mh. Rais Dk Hussein Mwinyi ziarani Donge.

My Take:
Sishabikii unyanyasaji wa kingono Wala mawa ya kulevya. Lakini kupewa dhamana na kitopewa dhamana vipo kwenye kanuni zetu. Sasa wewe unasema kama nani? Hakimu au Jaji? Ndio maana tunahitaji Katiba itakayofuatwa na kuheshimiwa kudhibiti Mamlaka ya Rais.

Kigwangala amesema katiba inaweza kuwa na statement nzuri lakini utekelezwaji ukawa sifuri.

Dk Mwinyi atambue kuwa kauli ya Rais ni kama amri. Ukitamka hovyo ni hatari sana. Tutegemee haki za watuhumiwa kuminywa sasa!
 
Rais Rodrigo Durtete alikwenda mbali zaidi, ALIANZISHA "FIRING SQUAD"

"Firing Squad" haikumsaza "king pin" wa madawa kule UFILIPINO.

UFILIPINO imeoza imeoza kwa madawa ya kulevya na madanguro.

Ni nchi inayoongoza kwa kuwa na WATOTO WENYE BABA WATALII....watalii wanaokwenda kuinjoi visiwani na pia kuinjoi "kula bwimbwi"...."mateja hao" wakiondoka huviacha nyuma vitoto visivyo na "baba mzazi-mlezi"mwishowe navyo hutumbukia UTEJANI huku mama zao wakiendeleza "biashara kongwe".

Mh.Rais Hussein Mwinyi ameongea kwa kuOVERREACT tu, ameumizwa na hali iliyopo.

NB: Kuhusu udhalilishaji na ubakaji, WAZANZIBARI waamue wenyewe KUBADILI TABIA ZA KIMAZOEA za kuwaonea huruma wahalifu hao(inawezekana kubadilika)
 
Tusijaribu kuvunja sheria kwa matamshi, kama tunahitaji kuwekea mkazo kwenye issue fulani ni bora kupandisha bei ya bondi ya dhamana kuwa milioni 600 kwa makosa ya madawa na udhalilishaji, watuhumiwa hawataweza kulipa.
 
Natilia mkazo kweli wasipewe dhamana...hasa hao wabakaji...na nyie kueni mnaojidai rais kalewa madaraka hamjielewi. Kwan ikitokea habar mtu kabaka kitoto cha miaka 2 mnaanza toa povu hapa...hakuna kutetea ujinga waache wasipate dhamana..
 
Kupewa au kutopewa dhana, ni maamuzi ya mahakama, siyo Rais. Mwinyo ameanza kuharibu.

Au shetani akiwa ndani ya mtu, mtu yule akifa, shetani huwa anatoka na kuyafuta makazi mapya?
 
Natilia mkazo kweli wasipewe dhamana...hasa hao wabakaji...na nyie kueni mnaojidai rais kalewa madaraka hamjielewi. Kwan ikitokea habar mtu kabaka kitoto cha miaka 2 mnaanza toa povu hapa...hakuna kutetea ujinga waache wasipate dhamana..
Wewe hujielewi. Hakuna anayeunga mkono uovu, ndiyo maana watu wakati wote wamepinga maovu mbalimbali ya marehemu. Watu wanachukia uovu.

Lakini jambo la muhimu, Rais asiingilie kazi ya muhimili usio wake. Kuingilia kazi ya muhimili mwingine ni uovu, Rais anakuwa mbakaji wa mamlaka ya muhimili mwingine.
 
Na hapo hapo mnampigia kelele Mama aingilie kati suala la Halima Mdee and Co.

Yaani tumepoteana kabisa kabisa kudaaaadeki.

CCM mbele kwa mbeleeeeeee
 
Wewe hujielewi. Hakuna anayeunga mkono uovu, ndiyo maana watu wakati wote wamepinga maovu mbalimbali ya marehemu. Watu wanachukia uovu.

Lakini jambo la muhimu, Rais asiingilie kazi ya muhimili usio wake. Kuingilia kazi ya muhimili mwingine ni uovu, Rais anakuwa mbakaji wa mamlaka ya muhimili mwingine.
Hiyo ni kawaida tu hata sisi raia huku tunatoa hukumu tena ya kifo kwa watuhumiwa wa wizi kabla hajafika polisi wala mahakamani.

Kuna matendo yanakithiri mpaka sheria zilizotungwa mnaziona hazifai.

Kwahiyo rais mpaka kusema hivyo kaona kuna mwanya kupitia dhamana wanazopata watuhumiwa, wakiwa vituo vya polisi.
 
Back
Top Bottom