Kwa mara ya kwanza Dunia inaenda kushuhudia mkuu wa nchi, Rais akitangaza utalii. Rais anapoamua kutangaza utalii maana yake ni kwamba hilo Taifa analoongoza ni Taifa mfu, ni Taifa lililokufa, ni taifa jipya kabisa chini ya jua na halina raslimali zozote na wala kitu chochote, sasa inabidi atoke mkuu wa nchi aifahamishe Dunia kuwa taifa analoongoza lina sehemu za utalii.
Na Kwanza hata kama taifa halina chochote, siyo kazi ya Rais kutangaza utalii. Zipo strategies za kutangaza utalii, Samatta ni maarufu Duniani kuliko Rais Samia.
Rais anapoenda Location kama msanii wa Bongo movie kutangaza utalii,huo mkosi mzito mno kwa taifa, watalii hawaji Tanzania eti kwa sababu Rais aliwatangazia.
Wanakuja kwa sababu usalama wao utakuwa mkubwa zaidi, huwezi kwenda kutalii kwenye Taifa ambalo kiongozi mkuu wa Chama kikubwa Cha Upinzani ni Gaidi, maana yake ni kwamba hata mawaziri nao ni magaidi.
Kenya inapokea maelfu ya watalii kwa mwaka kuliko Tanzania nani alimwona Rais wa Kenya akienda location kutangaza utalii?
Yaani Serikali nzima yenye wasomi wa kada zote haina strategies za kutangaza utalii hadi Rais aende location?
Mbona ni rahisi mno kutangaza utalii kuliko ilivyo rahisi kunywa maji? Tanzania hii yenye vivutio vyote leo hata Rwanda wameanza kuwazidi kupokea watalii wengi kwa sababu ya strategies.
Rais ataenda Location zote na mtatengeneza filamu zote na watalii hamtawaona kwa sababu hamna strategies.
Nyie strategies zenu ni kuua Upinzani tu haya mengine zero kabisa.
Ni kosa kubwa sana lililofanyika mpaka sasa
1. Rais kutangazaza vivutio vya utalii wakati waziri wa utalii na waziri wa mambo ya nje pamoja na maofisa waandamizi kuendelea kuwepo ofisini
2. Kutangazia ulimwengu kwamba Tanzania ina rasilimali fulani ikiwemo madini kwa kuwapeleka wazungu warekodi wenyewe jikoni (kosa la kiusalama na uchumi)
3. Je, mi kweli wazungu hawafahamu kwamba mlima Kilimanjaro uko Tanzania?
4. Je, wenyeji wa mkoa ambao mlima Kilimanjaro upo ambao pia ni wasomi wazuri na baadhi yao wako nje ya nchi kikazi au kibiashara hawautangazi uko kwao au wenyewe ndio kujitambulisha wako Kenya?
5. Jitihada zilizokuwa zimefanyika za kulinda mgodi wa Mererani na kudhibiti usafirishaji wa madini pasipo kupitia STAMICO umekwamijwa na nini hadi ufanyike mpango kutangaza ulimwenguni?
6. Je, ni kweli kwamba wazungu hawafahamu kwamba Tanzania kuna dhahabu Mwanza, Geita, Shinyanga, Morogoro, Singida na Mara?
7. Je, ni kweli wazungu hawafahamu kwamba Tanzania kuna madini ya Almasi na kwamba yanachimwa Mwadui na Maganzo Shinyanga pamoja kwa wenyewe ndio waanzilishi wa ugunduzi huo kama Dr.John Thoburn Williams msomi wa wa PhD ya jiolojia (raia wa Kanada alizaliwa 1907 na kufariki 1958) akaita mgodi kama Williamson Diamond Mines mwaka 1940 haitoshi kuwa utambulisho thabiti kwamba madini hayo yapo eneo gani Tanzania na kwa kiwango gani Carrat) wakati mpaka kiwanda cha kukatia walisaidia kukijenga huko Iringa (Tancut Almasi). Je, huyu Joseph Temba mtanzania aliyejipatia bonge la Almasi lenye thamani kubwa (
The nation of Tanzania has acquired its latest billionaire after a small-scale miner in Shinyanga region sold his diamonds for about one million dollars four points equivalent to Tsh. 3 billion.
The 512-carat diamond was discovered by small-scale miner Joseph Temba two weeks ago in the Maganzo area in Shinyanga.
Mr. Temba thanked the Ministry of Mines and the Mining Commission for the guidance and management of its Diamonds and the clear sales guidelines) hatangazi ukweli wa uwepo wake Tanzania?
8. Je, ni kweli wazungu hawajui tamaduni za kitanzania kuanzia Zanzibar na Tanzania bara kwa kipindi chote cha miaka 60 iliyopita?
9. Gharama za kutengeneza filamu hiyo na kuitangaza ni kiasi gani, nani atalipia na kwanini wazungu wakodiwe kutengeneza matangazo hayo wakati Tanzania inawataalamu wa kutosha kwa kazi hiyo?
10 Mji mkongwe wa Mikindani Mtwara ndio ulitakiwa utangazwe sana pamoja na kuwa walioujenga ni wajerumani na waarabu kwa nyakati tofauti
11. Mapango ya Amboni Tanga kulikoje?
TANBIHI: Wajerumani wana kumbukumbu ya kila mali iliyokuwepo Tanzania (ramani wanazo) zikionesha madini, maliasili (Selous) ambako hadi sasa kuna gari lililoharibika ambalo alilitumia mwindaji maarufu Fredrick Selous lipo limehifadhiwa nje ya geti la kuingilia hapo Mtemere. Morogoro mjini kuna dhahabu lakini watu wamekatazwa kuchimba kwa kisingizio wanachafua maji bwawa la Mindu kwa sumu ya Zebaki (milima Mindu na Mguuwandege Mkundi) yote ina madini ya dhahabu.