Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Rais Kikwete afanya uteuzi wa Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu watano wapya

Maswi tena!

Mliomchagua Kikwete mmetuponza sana watanzania.

Nakiri kumtopenda huyu raisi kwa kiwango cha juu sana.

Akina Lowassa na Kingunge ndo walimpugania Jk na 2010 Hamis Mgeja ndo alitumwa kumlipia Fedha za Form za Urais Ndugu Jk kwa ushauri wa kingunge na Lowassa unasemaje?
 
Ebu Sasa Tuambieni Wana CCM; Tuseme Kwa Bahati Mbaya Magaufuli Akabahatika Kuupata Urais wa JMT, Je Walioteuliwa Jana na JK

Atarecall uteuzi Huo.Hii Sasa Ni Too Much, Nadhani JK Anajaribu Kucheza na Psychology/Bongo za Wapiga Kura. Wapiga Kura Ebu Jitokezeni

Tuwaonyeshe CCM ya Kwamba Rais Uchaguliwa na Wananchi na Sio Kuteuliwa na Viongozi wa CCM.Kesho Pigeni Kura za hasira

Tujinasue Na Minyororo Hii ya Kujiona Wanyonge kwenye Nchi yetu.


Ninawasiwasi Na Uchaguzi Huu..Tutaweza Kumaliza Vibaya Kwani Kuna Kila Dalili za Wagombea Kutofika salama.../ Uchaguzi Huu Ni

Mkali na Upepo Unavuma Kulekea Upande wa Lowassa/Ukawa. Je Itakuwaje Mh. Lowassa Akishinda, na je atakubali wateule wa jana Waendelee na Nafasi zao.

Kesho sio Mbali Tutajua Mbivu na mbichi...

Unaumwa. Nenda kapate vipimo
 
Usitumie kura za ndiyo kufikiri, tumia na busara utaona kuwa hakuna sana haja ya uteuzi kama huu muda kama huu. Yeye sana sana angesamehe wafungwa wasiokuwa na makosa mazito.
 
busara ipi iliyokiukwa hapo?,,,,tatizo la bavicha bana ni ushabiki uliopitiliza,,,sasa hapa jk amekiuka busara ipi hasa?hebu tufafanulie....



tatizo lingine la bavicha ni wivu wa kike,,,,,

ELungata unaeshabikia mpaka unaboa hata ktk swala lililo wazi!!!. MAGUFULI anaimba mabadiliko, ataanzia wapi ikiwa mpaka sasa JK anapanga safu yake????????!!
 
Omar chambo ni mpiga dili mkuu alikuwa wizara ya uchukuzi akashindwana na mwakyembe Leo kapelekwa kwenye gesi
Alikuwa mkurugenzi wizara hiyo wakati JK akiwa waziri. Anajua michongo yote ya wawekezaji ambao ni kwa manufaa ya JK si ya nchi
 
huyu jamaa ahamini kama kesho anafungasha viragoo//////// hapa makomeo anaenda kuwa bawaba tu ila mlango ni jk

From the look of things this guy does not believe that his time is up!! Inawezekana kabisa kuwa mpaka hivi sasa bado hajahama ikulu; mswahili ni mswahili tu!!!
 
huyu jamaa ahamini kama kesho anafungasha viragoo//////// hapa makomeo anaenda kuwa bawaba tu ila mlango ni jk

Hata yule Mgombea wako ni Bawaba tu, Mlango ni Rostam na Sabodo kwa kushirikiana na Mafisad wengine wa kihindi.
 
Maswi alikuwa na escrow, kupande na home shopping bandarini. Sijui nini hii!
 
Nchi ya mfalme JK hajui kesho kuna uchaguzi wa rais atakayeunda serikali. Anaamini Magufuli atachaguliwa na hatabadirisha uteuzi wake. Ndiyo ya Mfalme juha haya.
 
sasa mmekubaliana na mimi kwamba hata yakibaki masaa mawili bado Kikwete atafanya uteuzi wa mawaziri, hapo bado kuna nafasi atakayoijaza ya Kombani hata kama zitakuwa zimebaki Dakika tano
 
Maswi tena!

Mliomchagua Kikwete mmetuponza sana watanzania.

Nakiri kumtopenda huyu raisi kwa kiwango cha juu sana.

Mkuu hii nchi ni aibu sana sijui kwa nini tulioichagua hili kibambara? Yaani umebakiza wiki 1 uachie ngazi unamteulia rais ajaye watu ambao huna hakika kama ataendelea nao? Katiba yetu inatakiwa kuyazuia haya maujinga mengine! Yote hayo kuwafurahisha marafiki zako? Pumba.aaaaaavu kabisa!

Siyo Maswi tu hata Omari Chambo anarudishwa tena kule kule! Akina Madeni Kipande yaani tabu tupu hili nchi!!
 
Ndiyo maana nasema Ikiwa watarazimisha maguvuli kuwa rahisi basi hatakuwa rais huyo!! atakuwa tv tu remote atakuwa nayo kikwete ha ha ha
 
mtakubaliana na sisi kina gogo la shamba, hapo bado kuna nafasi ya Kombani ataijaza hata kama zitakuwa zimebaki DK tano
 
wataendelea kuwepo,,,unafikiri rais mpya anaanza kuondoa wafanyakazi kazini,,,itachukua kama miaka 2,kabla rais mpya hajaweka watu anaowataka yeye,,sio jambo la kuapishwa leo na kuanza kuondoa makatibu tawala,,etc

Kama ni hivyo hayo mabadiliko ya kweli anayosema Magufuli yatakujaje? Ni laana au ni nini? Hivi hizo nafasi zingebaki wazi kwa wiki kadhaa tu ingekuwaje?
 
Ndio sababu ccm hawataki katiba mpya kwa ajili ya huu upuuzi, inakera sana kwa kweli.
 
Yote yanafanywa kwa mujibu wa sheria.

Sorry. Excellent Yodoki. Hawa UKAWA hawaelewi sheria ndiyo maana walipeleka mahakamani kesi ya kuiomba mahakama eti iridhie mazingira ya ujinga yatakayo hatarisha amani ya nchi wakatimuliwa hadi aibu
 
haa haa ulaji. na maghufuli atafanya hivohivo tena kwa kasi ya ajabu. dawa ni kesho kuchagua lowasa...
Jamani kipande aliyekua Mkurugenzi TPA akafukuzwa na Sitta kwa ufisadi na Maswai wa nishati na madini akatimuliwa kwa kashfa ya ESCROW.Hii ni dhihaka kwa Watanzania.
 
Hata sijui anawaonaje WaTZ? Huyu jamaa amewadharau sana wananchi. Safari zake watu wamesemaaaaaa lakini aliendelea tu hadi juzi.
Imagine nchi zenye demokrasia ya kweli, ambapo mwananchi akitoa malalamiko tu, kiongozi huenda na maji.....Tutafika lini huko?
 
Back
Top Bottom