Jamani ndege kama hii BOEING 737-9 max ni ndege ya gharama sana achana na ununuzi wake tu bali hata maintenance pia.
Inasikitisha kuona Rais anatumia ndege hii yenye gharama kiasi hiki huku ndege ya Rais ikiwepo bado.
Sitashangaa ikipata hitilafu tukaitelekeza mahali kwa sababu matumizi yake hayakuendana na faida kutokana na ubinafsi wa watu wachache.
View attachment 2914630
Kwenye somo la maintenance kuna makundi sita muhimu
1.Predictive maintenance
2.Preventive maintenance
3.Corrective maintenance
4.Predetermined maintenance
5.Condition based maintenance
6.Reactive maintenance
Tafsiri zake mta google wenyewe
Katika vyombo vya usafiri ndege iko sensitive zaidi ikifuatiwa na Meli
Kwenye ndege lazima hatua hizi sita zipitiwe.Ndege ina sensors nyingi mno ukiona operation manuals za ndege kubwa kama hiyo baada ya kukabidhiwa zinaweza kujaza pickup mbili.Mlishasikia gari au mabasi yana black box?
Msipende kuingiza maongezi ya vijiwe vya kahawa na siasa kwenye taaluma za watu pia msimuingilie mama kwenye maamuzi yake na pia msiingilie maamuzi ya shirika la ndege.
Mnaambiwa alisafiri na Kikwete wote ni viongozi wakubwa ujue wana waandishi wao,makatibu wao na wasemaji wakuu na wengine hivyo ujumbe unakuwa mkubwa ndege ya raisi Gulfstream japo ina viwango vya juu lakini inakuwa ni ndogo unataka wabanane kama wako kwenye Ki HIACE?
Ukae ukijua kuwa ndege ikipata ajali wanaopata tabu sio shirika au nchi husika peke yake bali walioitengeneza,shirika la anga la kimataifa ICAO,dunia nzima,familia za wafiwa kudai fidia na zaidi msichukulie mambo kwa wepesi wake.
Msidhani ndege ni kama gari lako unakwenda unaangalia matairi unabadili oil basi unatamba umefanya service huyooo unachoma zako unakwenda Moshi kula Xmass na kunywa mbege.Ndege inaweza kuwa nzima kabisa lakini ikakatazwa kuruka.
Mimi mwenyewe imeshawahi tokea siku moja ndege yetu wakati inataka tu kuondoka rubani akagundua kuna crack ndogo kwenye kiyoo cha abiria na sijui ni censor gani ilimuambia ukweli ndege haikupaa siku hiyo.Kuna siku ndege yetu iligongana na ndege hawa tunaita ndege mwarabu,ndege John au Marabou Stock haikupata madhara yeyote lakini alikuja injinia kuja kukagua.
Kitu kingine mnajuaje pamoja na kwamba ndege ni ya serikali.Serikali yenyewe imekodisha na italilipa shirika? Ni sawa na wewe una duka au baa yako unakunywa pombe lakini hata siku moja hulipi kwa vyovyote utafilisika.Sitegemei ikulu itakosa fungu la kukodisha hiyo ndege.Magufuli hata yeye alipenda sana kutumia ndege hizi zetu za kiraia tena kwa yeye kwa hapa nchini alikuwa anazamia muda wowote anasafiri na abiria wengine.Hii kwa mama ni safari ya nje ni tofauti.
Muacheni mama mama yuko kazini