Rais kutumia ndege ya abiria badala ya ndege yake binafsi, nani mshauri wake?

Rais hata mtanzania yoyote anaweza kuikodi ndege akasafiri nayo. NACHOHOFIA NI KUTOLIPWA PESA YA KUKODISHIWA NDEGE HIYO. HII ITAUA TENA SHIRIKA KAMA MWANZO ZILIVYOKUWA ZINASAFIRI BURE KWA AJILI YA ABIRIA VIONGOZI WALIOKUWA HAWAJITOKeZI HUKU WAMEzuia nafasi na ndege kuondoka bila abiria. Hapa nashauri ATCL WAHAKIKISHE KULIPWA KABLA YA KUTOA NDEGE AU KUWEKEA MTU NAFASI ili abiria aspojitokeza shirika lisipate hasara. Hizo ndege tulinunua kwa ajili ya biashara. Kuna viongozi wengi sana wa nchi mbalimbali wanatumia ndege za biashara kama KLM, BA, EMIRATES nk kusafirishia viongozi wao safari mbalimbali.
 
Umeongea sahihi sana Mkuu

Wasipofanya hayo, tuhesabu baada ya miaka kadhaa kuingia hasara kubwa kutokana na Shirika kushindwa kujiendesha
 
JF kila mtu mpanda ndege. Hongereni
Gharama za kusafiri na ndege Kwa safari za ndani sio kubwa sana ukiamua.

Roughly ina range 265,000 hadi 900,000 kulingana na tarehe ya safari yako.

Hata hivyo wengine husafirishwa na Ofisi Mkuu.
 
Kwenye somo la maintenance kuna makundi sita muhimu

1.Predictive maintenance

2.Preventive maintenance

3.Corrective maintenance

4.Predetermined maintenance

5.Condition based maintenance

6.Reactive maintenance

Tafsiri zake mta google wenyewe

Katika vyombo vya usafiri ndege iko sensitive zaidi ikifuatiwa na Meli

Kwenye ndege lazima hatua hizi sita zipitiwe.Ndege ina sensors nyingi mno ukiona operation manuals za ndege kubwa kama hiyo baada ya kukabidhiwa zinaweza kujaza pickup mbili.Mlishasikia gari au mabasi yana black box?

Msipende kuingiza maongezi ya vijiwe vya kahawa na siasa kwenye taaluma za watu pia msimuingilie mama kwenye maamuzi yake na pia msiingilie maamuzi ya shirika la ndege.

Mnaambiwa alisafiri na Kikwete wote ni viongozi wakubwa ujue wana waandishi wao,makatibu wao na wasemaji wakuu na wengine hivyo ujumbe unakuwa mkubwa ndege ya raisi Gulfstream japo ina viwango vya juu lakini inakuwa ni ndogo unataka wabanane kama wako kwenye Ki HIACE?

Ukae ukijua kuwa ndege ikipata ajali wanaopata tabu sio shirika au nchi husika peke yake bali walioitengeneza,shirika la anga la kimataifa ICAO,dunia nzima,familia za wafiwa kudai fidia na zaidi msichukulie mambo kwa wepesi wake.

Msidhani ndege ni kama gari lako unakwenda unaangalia matairi unabadili oil basi unatamba umefanya service huyooo unachoma zako unakwenda Moshi kula Xmass na kunywa mbege.Ndege inaweza kuwa nzima kabisa lakini ikakatazwa kuruka.

Mimi mwenyewe imeshawahi tokea siku moja ndege yetu wakati inataka tu kuondoka rubani akagundua kuna crack ndogo kwenye kiyoo cha abiria na sijui ni censor gani ilimuambia ukweli ndege haikupaa siku hiyo.Kuna siku ndege yetu iligongana na ndege hawa tunaita ndege mwarabu,ndege John au Marabou Stock haikupata madhara yeyote lakini alikuja injinia kuja kukagua.

Kitu kingine mnajuaje pamoja na kwamba ndege ni ya serikali.Serikali yenyewe imekodisha na italilipa shirika? Ni sawa na wewe una duka au baa yako unakunywa pombe lakini hata siku moja hulipi kwa vyovyote utafilisika.Sitegemei ikulu itakosa fungu la kukodisha hiyo ndege.Magufuli hata yeye alipenda sana kutumia ndege hizi zetu za kiraia tena kwa yeye kwa hapa nchini alikuwa anazamia muda wowote anasafiri na abiria wengine.Hii kwa mama ni safari ya nje ni tofauti.

Muacheni mama mama yuko kazini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…