Rais Lazarus Chakwera wa Malawi kuzuru Tanzania

Rais Lazarus Chakwera wa Malawi kuzuru Tanzania

Huyo Raisi mpya wa Malawi ni role model wa Upinzani hususani chadema, na alivyoshinda Uchaguzi alipigiwa debe sana na Upinzani wa Tanzania, ...
Nimesikia Jamaa pia ameandaa hitaji kwa Bunge la Malawi kuomba Kukasimisha baadhi ya Mamlaka yake (Mamlaka ya Raisi kwa Bunge) Sina details sana ila nilipita pita kwenye taarifa zetu humu JF. Sina hakika na Hilo ila kama ni kweli, basi yuko smart sana, Hataweza kupokea ushauri wowote wa ukandamizaji Raia.
 
Maji mu shingo, jamaa anakuja kusaidia kampeni.
 
Bado Msumbiji, Zambia, DRC na Rwanda tukamilishe ngwe....
 
PROF. KABUDI ANAZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU RATIBA YA RAIS LAZARUS CHAKWERA



Rais Lazarus M Chakwera wa Jamhuri ya Malawi kuwasili nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya kikazi (state visit)ya siku 3 kwa mwaliko wa Rais John Pombe Joseph Magufuli. Rais Lazarus Chakwera ni rais wa sita wa Jamhuri ya Malawi na aliingia madarakani mwezi June 2020 baada ya kushinda uchaguzi kupitia chama cha upinzani cha

Atapokelewa na Rais Magufuli kisha atatembelea bandari ya Dar es Salaam na kutembelea kituo cha kuhifadhi mizigo cha Malawi Cargo Centre.

Rais wa Malawi ataweka jiwe la msingi katika kituo cha kimataifa cha mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani kilichopo kiunga cha Mbezi mwisho jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Malawi na Tanzania wana miradi ya pamoja mfano barabara ya kutoka Mtwara mpaka bandari ya Mbamba Bay pia kuna mradi wa kuimarisha usafiri katika ziwa Nyasa katika bandari za Nkata Bay upande wa Malawi n.k
 
Mfahamu Rais Lazarus Chakwera aliyeshinda Urais kupitia chama cha upinzani


Rais wa Malawi Lazarus Chakwera ni mhubiri wa zamani injili ambaye anasema alijiunga na siasa ili kuitia wito wa Mungu.

48874803_101.jpg


Rais wa Jamhuri ya Malawi, Mh. Larazus Chakwera

"Siku moja Mungu alizungumza na moyo wangu na Mungu hakusema ananiondoa kuwa mhubiri, Mungu alikuwa akisema ninatanua kanisa lako ili uwe mhubiri wa taifa zima" alisema Chakwera katika video ya hivi karibuni wakati wa kampeni za uchaguzi.

Kwa miaka saba iliyopita Chakwera mwenye umri wa miaka 65 amekiongoza chama kikongwe zaidi cha siasa nchini Malawi Congress Party (MCP), ambacho kililiongoza taifa hilo la kusini mwa Afrika kwa miongo mitatu tangu mwaka 1964 hadi mwaka 1994 chini ya utawala wa chama kimoja chini ya kiongozi wa kiimla Hastings Kamuzu Banda

Chakwera alikiongoza chama hicho wakati wa uchaguzi wa raia wa mwaka 2014 na kushika nafasi ya pili nyuma ya rais anayeondoka madarakani Peter Mutharika.

Kadhalika aliwania tena kiti cha urais mwaka uliopita na kushindwa lakini uchaguzi huo baadaye ulibatilishwa.

Chama cha MCP kimepoteza chaguzi tano za urais tangu mwaka 1994 lakini Chakwera alifanya kazi kubwa ya kurejesha tena haiba ya chama hicho kwa kujitenga na utawala wa mkono wa chuma wa Banda na kuimrisha tena ngome ya chama hicho.

Uchaguzi wa mwaka 2019 ulikuwa wa tofauti

53936394_101.jpg


Malawi Lilongwe | Neuwahlen | Beamte überprüfen Wählerlisten

Baada ya kushindwa na Mutharika kwa ushindi mwembamba wakati wa uchaguzi wa mwaka uliopita, Chakwera alianzisha kile kilichokuja kufahamika kuwa mchakato wa kihistoria wa kisheria.

Uchaguzi huo ulibatilishwa na mahakama ya juu ya Malawi iliyobaini osari nyingi ikiwemo matumzii ya wino wa kufanyia masahihisho katika karatasi za matokeo.

Uamuzi huo ulilitikisa bara la Afrika ambako ni nadra kwa viongozi walio madarakani kushindwa uchaguzi au kesi katika mahakama za mataifa yao.

Mahakama iliamuru kufanyika kwa uchaguzi wa marudio na kulingana na tume ya uchaguzi Chakwera amepata ushindi wa zaidi ya asilimia 58 ya kura.

"Watu wanataka mabadiliko. Wanahitaji mabadiliko na wanatuona sisi kuwa taswira ya mabadiliko" amesema Chakwera alipozungumza na shirika la habari la AFP.

Wakati wa uchaguzi wa marudio Chakwera alipata uungaji mkono mkubwa kutoka kwa makamu wa rais Saulos Chilima, rais wa zamani Joyce Banda na vyama kadhaa vidogo.

53968320_101.jpg


Malawi Opposition Lazarus Chakwera
Chakwera alizaliwa mjini Lilongwe na mkulima mdogo ambaye watoto wake wawili wa kwanza wa kiume walifariki wakiwa wachanga. Alipewa jina la Lazarus sawa na mtu mmoja aliyetajwa ndani ya biblia kuwa alifufuliwa kutoka wafu.

Alisomea falsafa na theolojia na kuwa rais wa madehebu ya wapentekoste kuanzia mwaka 1989 hadi 2013 alipochukua hatamu za uongozi wa chama cha MCP.

Kwa miaka mingi alikuwa mwanaharakati wa utawala bora katika kamati inayoheshimika nchini Malawi ya masuala ya umma (PAC) ambayo ni mkusanyiko wa asasi za kidini na kiraia.

Mara zote Chakwera alifungua mikutano yake ya kampeni kwa sala.

Chakwera anayezungumza kingereza cha lafudhi ya Marekani anasema anapenda kujisomea, kusikiliza muziki wa asili, miondoko ya country na nyimbo za injili.

Rais Lazarus Chikwera ameoa mke mmoja na ana watoto wanne.

Source kwa hisani kubwa ya : Rais Mteule wa Malawi Lazarus Chakwera ni nani? | DW | 28.06.2020
 
Unaona mlivyowaongo..... Hicho chama chake ndio CCM ya huko
Dada yangu sidhani kama Unafuatilia Vyema siasa; Chama Tawala ni Democratic Progressive Party (DPP); Mwaka jana mwezi wa sita vyama vya upinzani viliungana katika umoja waliouita Tonse Alliance, vikapambana na chama tawala Democratic Progressive Party (DPP) na kufanikiwa kuking'oa madarakani.

Lazarus Chikwira ndo alisimamishwa kwenye umoja huo; Sasa Anakuwaje kama CCM?? Au mie ndo sijakuelewa??
 
Possibly asipewe promo Kubwa sana, Maana ni Mpinzani wa chama cha siasa malawi Aliyeshinda; Nimewaza tuu..
Hatoki cha upinzani chama chake ni kilicholeta Uhuru wa Malawi ndicho kilikuwa chama tawala kabla ya vyama vingi

Wananchi wa Malawi safari walionyesha hasira zao baada ya kuuchoka upinzani wakaamua kukirudisha chama kilicholeta Uhuru wa Malawi madarakani
Hicho chama ni rafiki wa CCM

Karibu Raisi wa Malawi Tanzania
 
Hatoki cha upinzani chama chake ni kilicholeta Uhuru wa Malawi ndicho kilikuwa chama tawala kabla ya vyama vingi
Asante Mkuu Nashukuru; Inamaana Yeye ameshinda kwenye Muungano na Chama zamani, au Baada ya Muungano ni Chama Kipya? I mean Ameshinda na chama chake cha zamani??
Asante
 
Je ziara hii ya kiserikali ya Rais Lazarus Chakwera wa Jamhuri ya Malawi katikati ya mchakato wa kampeni za Uchaguzi Mkuu 2020 itaamsha tamaa ya wanaotaka mabadiliko kupitia Uchaguzi huu wa 2020 Tanzania?

Au itatumika na CCM Mpya kunadi sera yake ya Maendeleo ya Vitu kujinufaisha kisiasa kipindi hiki cha kampeni za 2020?
 
The most celebrated African president from our neighboring country is about to pay the state visit to the Africa's shining star JPM

Chakwera opted to choose Tanzania as his very early state visit as to mining the extraordinary experience in leading his country in prosperity and Panasonic growth as Tanzania

Welcome to the United Republic of Tanzania Mr president 🇹🇿 🇲🇼

View attachment 1590688
The most celebrated African president from our neighboring country is about to pay the state visit to the Africa's shining star JPM

Chakwera opted to choose Tanzania as his very early state visit as to mining the extraordinary experience in leading his country in prosperity and Panasonic growth as Tanzania

Welcome to the United Republic of Tanzania Mr president 🇹🇿 🇲🇼

View attachment 1590688
Point of correction this is not the first foreign visit for Dr Laz since he booted out the man who was endorsed by Magufuli when had visited Lilongwe Babu Munthalika. Dr Laz first had visited Lusaka later did proceed to Harare.Try to be resourceful too pathetic.
Expect mugogoro mku

Chakwera’s first foreign trip to Zambia for bilateral talks
 
28 Jun 2020
Malawi's opposition leader has won the rerun of the presidential election. Lazarus Chakwera got just under 59 percent of the vote. That makes him the first African opposition leader to win power in a court-ordered rerun.
 
Back
Top Bottom