Good Father
JF-Expert Member
- Feb 28, 2014
- 10,321
- 18,574
View attachment 1689777
Rais Magufuli ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa jengo la magonjwa ya dharura Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, akiwa katika eneo hilo ameagiza Madaktari waliohama Hospitali hiyo ya Serikali na kuhamia Hospitali binafsi kwa kigezo cha maslahi wafuatiliwe.
Rais Magufuli amenukuliwa akisema
βMadaktari wanapata mkopo 100% wakiwa Chuoni, halafu tunawapa ajira Serikalini wanakimbia kisa maslahi, si ungekimbia wakati unasoma? Hela yetu umekula halafu unakimbia kwenda Hospitali binafsi kwa kisingizio cha maslahi, ni kukosa uzalendoβ
βMtafuteni huyo Daktari aliyekimbia Hospitali ya Serikali na hiyo Hospitali binafsi aliyokimbilia, ikiwezekana tunamfungia Daktari, tunaifungia na Hospitali aliyoenda, wakati wa kusomesha hawatuchangii, tukishawasomesha wanakwenda kuwaiba, sio sawaβ
Mboga moto ugali moto
Mitano tena[emoji23][emoji23]